AL-AHKAAMUL WAADHIHA
HIZI NI FAT’WA ZA KIONGOZI WA
KIDINI AYATULLAHI AL-UDHMA ALHAJI SHEKH MOHAMMAD FAADHIL LANKARAANIY
( Mundu amrefushie umri)
TAQLIID
Mas’ala 1: Ni wajibu kwa kila
mukallafu ambae hajafikia daraja ya ijtihadi imma kuwa muqallid (kumfua
mujitahidi Fulani katika mas’ala ya kisheria) au kufanya ihtiyaati katika ibada
zake zote na utendaji kazi wake (kama biashara) na mengineyo na katika matendo
yake mengine anayo paswa kuyafanya au kuyaacha. Mas’ala 2: Matendo ya mtu wa
kawaida ayafanyayo bila kufanya taqliid au ihtiyaat hayatoshelezi kisheria
maadamu haijulikani ya kuwa yako sambamba na ukweli au uhakika wa kisheria au
yako sambamba na fat’wa za Mujitahid ambae ilikuwa ni wajibu kwake kumfuata
katika utendaji wake. Mas’ala 3: Taqliidi ni kazi au
tendo lifanyikalo kwa kutegemea kauli ya Mujitahidi Fulani. Kwa hivyo basi
haijuzu na haifai kumfuata au kufanya taqliid ya mtu asie kuwa Mujtahidi. Na
niwajibu kwa mtu asie kuwa Mujtahidi kufanya taqliid ikiwa hakuweza kufanya
ihtiyaat. Mas’ala 4: Kauli yenye nguvu ni
kwamba inawezekana kutosheka tu na kufanya ihtiyaati katika uwanja wa utendaji
au katika matendo hata kama kufanya hivyo italazimu kurudia tendo hilo au mukallaf akaweza kufanya ijtihadi au taqliid. Mas’ala 5: Ni wajibu kufanya
uchunguzi na kumtafuata Mujtahidi alie kuwa Aalam (mwenye elimu zaidi kati ya
Mamujtahidi) ikiwa kuna uwezekano wa kufanya hivyo, kutokana na wajibu wa
kumfuata yeye au kufanya taqlidi yake mahala ambamo kuna ihtimali ya
kutofautiana Mamujitahidi kutokana na kauli iliyo na nguvu zaidi. Na makusudio ya Aaalam ni mwenye
maarifa zaidi ya kanuni na dalili za mas’ala na mwenye kufahamu na kuelewa
zaidi kuliko wenziwe na mwenye kufahamu vyema habari, na mzuri zaidi katika
kufahamu hadithi, na kwa ufupi ni kuwa Aalam ni yule ambae ni mwenye uwezo
mzuri zaidi wa kufanya istinbaat ( uchambuzi na utungaji wa sheria). Na Marejeo
ya kumuainisha na kumthibitisha pia kumfahamu ni kwa ahlul khibrah wataalam wa
mambo hayo na wenye ujuzi wa istimbati na utungaji wa sheria. Mas’ala 6: Hufahamika kuwa huyu
ni mjuzi zaidi kutokana na elimu ya kimaumbile au kitu chochote chenye nafasi kama hiyo kati ya elimu za kawaida au vitu vya kawaida viwezavyo kujulisha hali hiyo, au
kwa kutumia vithibitisho na dalili zisizo pingika au kupingwa, au kwa kuenea
habari ziletazo matumaini na yakini. Mas’ala 7: Ikiwa kutakuwa na
Mamujitahidi wawili na haikuwezekana kupata ujuzu au dalili (uthibitisho) wa
yupi alie mjuzi zaidi kati yao wawili, ikiwa kutakuwa na ihtimali ya kuwa mmoja
wapo ambae ni maalum ni mjuzi zaidi basi hapo itawajibika kumfuata yeye
(kufanya taqlidi yake). Mas’ala 8: Ni sharti Mujtahidi
awe na masharti yafuatayo, awe baaligh (balee) mwenye akili timamu, awe muumini
na muadilifu na awe mwanaume na awe hai, kwa hivyo basi haijuzu kufanya
taqliidi ya maiti kwa mara ya kwanza, na awe amezaliwa kwanjia ya ndoa halali
(Twaharatul mawlid), na awe ni mwenye ujuzi zaidi, na kauli ya ahwat ni kuwa
asiwe ni mwenye kuipenda dunia (asiwe mwenye kufuata mambo ya kidunia)
Mas’ala 9: Makusudio ya uadilifu
ni kuwa awe na uwezo wa kinafsi wa kutekeleza mambo ya wajibu na kuacha
madhambi hasa mambo makubwa yaliyo haramishwa, na utendaji wa mambo ya wajibu
na kuacha ya haramu nje huthibiti kwa kuwepo uwezo wa kinafsi na kupitia murua
wa mtu. Na uadilifu hujulikana na kufahamika kwa husnudh- dhaahir ( kuwa na
dhahiri nzuri asie sifika kwa maovu), na huthibiti kwa ushahidi wa watu wawili
waadilifu na kwa kuenea habari zitoazo ujuzi au yakini na matumaini. Mas’ala 10: Ikiwa Mujtahidi
atatokewa na jambo ambalo litamfanya akose sharti moja wapo kati ya masharti
hayo yaliyo tangulia itakuwa no wajibu kwa muqallid kuhamia kwa Mijtahidi
mwingione. Mas’ala 11: Ikiwa mukallaf
atafanya taqliid na kumfuata mtu ambae hakuwa ametimiza masharti na ukapita
muda Fulani akifanya taqlidi yake atakuwa kama yule ambae hakufanya taqlidi
asilan, ama ikiwa matendo yake aliyo yafanya yatakuwa sambamba na uhakika na
ukweli wa kisheria au yako sambamba na fat’wa za Mujtahidi ambae ilikuwa ni
wajibu kufanya taqlidi yake (ilikuwa ni wajibu kumfuata) wakati akifanya
matendo hayo basi matendo hayo ni sahihi, laa sivyo matendo yake sio sahihi. Mas’ala 12: Ikiwa mukallaf
atamuqallid Mujtahidi ambae anaruhusu na kujuzisha kubakia kwenye taqliid ya
Mujtahidi alie kufa, kisha Mujtahidi huyo akafa haijuzu kubakia kwenye taqlidi
yake hasa kwenye mas’ala haya, bali ni wajibu kurudi na kurejea kwa alie hai
ambae ni Aaalam (mjuzi zaidi) katika mas’ala ya kujuzu kubakia kwa alie kufa au
hapana. Mas’ala 13: Haijuzu kufanya
taqliidi ya maiti (kumfuata Mujtahidi alie kufa) kwa mara ya kwanza, lau kama
mukallaf atamfuata Mujtahidi alie hai kisha akafariki inajuzu kubakia kwenye
taqlidi yake moja kwa moja bila pingamizi ikiwa watalingana kielimu kati ya
alie kufa na yule alie hai, na lau kama alie kufa ni mjuzi zaidi itajuzu
kubakia kwake, na katika mas’ala hayo hakuna tofauto kati ya mtu alie fanya
matendo kwa mujibu wa fat’wa zake au mwingine. Mas’ala 14: Ikiwa kutakuwa na
Mamujitahidi wawili walio lingana kwenye elimu inajuzu kwa mukallaf kumfuata
yeyote kati ya wawili hao na inajuzu kwake baadhi ya mas’ala kuchukua kwa
Mujtahidi huyo na mengine kwa Mujtahidi mwingine. Ama ikiwa mmoja wao ni mwenye
bora zaidi kuliko mwingine katika uadilifu au uchamungu au mfano wa hayo kauli
ya ahwat ya wajibu ni kuwa atamchagua huyo. Mas’ala 15: Inajuzu kuhama baada
ya kuwa mukallaf amefanya taqliid kutoka kwa Mujtahidi alie hai kwenda kwa
Mujtahidi mwingine alie hai na ambae analingana nae kielimu na ni wajibu kuhama
ikiwa wa pili ni mjuzi zaidi. Mas’ala 16: Njia za kufahamu
fat’wa za Mujtahidi ni kama zifuatazo:
1- Kusikia kwa Mujitahidi akisema yeye mwenyewe.
2- Kuambiwa na watu wawili waadilifu, na haitoshi kutosheka na habari za
mtu mmoja muadilifu (yaani kutosheka na habari za mtu mmoja kuna ishkaali),
isipokuwa ikiwa habari yake itatupa matumaini na yakini.
3- Kuwepo kwa fat’wa kwenye risalatul amaliyyah (kitabu chake cha fat’wa)
ikiwa kimeandikwa na yeye mwenyewe au kwa khati yake, au kuzielewa fat’wa zake
zote. Mas’ala 17: Ikiwa mtu atanukuu kimakosa fat’wa ya
Mujtahidi ni wajibu kwake kuwatangazia walio jifunza kwake, vilevile ni
wajibu juu ya Mujtahid kutangaza ikiwa atakosea katika kuibainisha fat’wa yake. Mas’ala 18: Ikiwa mtu atanukuu
fat’wa ya Mujtahidi ikiwa sahihi, kisha rai ya Mujtahidi ikabadilika kuhusiana
na fat’wa hiyo au katika mas’ala hayo kutokana na kauli ya ahwati ni kuwa
niwajibu kwa mtu alie nukuu kumtangazia alie sikia kutoka kwake fat’wa ya
mwamzao. Mas’ala 19: Ikiwa watu wawili
walio nukuu fat’wa watapingana au dalili mbili zikapingana katika kunukuu
fat’wa ya Mujtahidi, mwenye kunukuu na dalili hizo zitaporomoka yaani
hazitakuwa na maana. Na ikiwa alienukuu atapingana na alie sikia kutoka kwa
Mujtahidi mwenyewe atatangulizwa na kupewa kipaumbele alie sikia.Ama ikiwa
atapingana alie sikia au alie nukuu kwa kutoa kitabu cha fat’wa za Mujtahi yule
hapo kitatangulizwa kitabu chake cha fat’wa ikiwa kitabu hicho kimeandikwa kwa
hati yake au ikiwa ni mwenye kuyajua yote yaliyomo kwenye kitabu hicho
kiukamilifu. Mas’ala 20: Muqallid (mwenye
kumfuata Mujtahidi) anayo hiari kati ya kufanya matendo kulingana na ihtiyaati
ya Mujtahidi ambae ni Aalam (mjuzi zaidi)- ikiwa hakuwa na fat’wa kwenye
mas’ala fulani- na kati ya kurejea kwa mwingine, na hapo ata angaliwa mjuzi
zidi kuliko mwingine. Mas’ala 21: Ikiwa Muqallid
atakuwa na shaka juu ya kufariki kwa Mujtahidi au kubadilika rai yake au
kutokea mambo ambayo hayajuzishi kumfuata au kumfanyia taqliid inajuzu kwa mtu
huyo kubakia kwa Mujtahidi huyo mpaka hali yake ibainike vizuri. Mas’ala 22: Hukumu ya Al-haakim
alie timiza masharti haijuzu kuipinga hata kama ni Mujtahidi mwingine, ispokuwa
ikiwa litabainika kosa lake kwenye hukumu hiyo. Mas’ala 23: Ni wajibu kwa mtu wa
kawaida katika muda mbao bado anafanya uchunguzi wa kumtafuta Mujtahidi au
aliekuwa Aalam kufanya ihtiyaati kwenye matendo yake. Mas’ala 24: Ikiwa mukallaf
atafahamu ya kuwa yeye alikuwa akifanya ibada zake bila kufuata fat’wa za
Mujtahidi yaani hakuwa akifanya taqliid kwa muda kadhaa na hakuweza kufahamu
kiasi cha muda huo, ikiwa atafahamu namna zilivyo kuwa zikifanyika ibada zile
na akafahamu ya kuwa zilikuwa sambamba na uhakika wa kisheria au fat’wa za
Mujtahidi ambae ndie aliepewa jukumu la kurejelewa, hapo hakutakuwa na jukumu
lolote juu yake, laa sivyo itamuwajibikia kufanya kadhaa au kulipa kiwango
ambacho anayakini nacho ikiwa kukhalifu huko kunamlazimu kulipa kadhaa
kulingana na mtizamo au rai ya Mujtahid, na kauli ya ahwat ya sunna ni kuwa
atalipa na kufanya kadhaa kiwango ambacho anafahamu yakuwa kwa kufanya hivyo
jukumu lake litakuwa limemuondokea (baraa atudhimmah). Mas’ala 25: Ikiwa utapita muda
tangu muqallid awe baaligh ( balee), na akaingiwa na shaka baadae ya kuwa
matendo yake alikuwa akiyafanya kwa kumfuata Mujtahidi au kwa kufanya taqliid
sahihi au laa, inajuzu kwake kuyajengea matendo yake yaliyo tangulia kuwa ni
sahihi, ama matendo yake yafuatayo ni wajibu juu yake kuyasahihisha kwa wakati
huo kwa kufanya taqliid. Mas’ala 26: Ikiwa rai ya
Mujtahidi itabadilika wakati huo haijuzu kwa muqallid kubakia kwenye rai yake
ya mwanzo ikiwa rai hiyo haiwafikiani na ihtiyaat, laa sivyo itajuzu kubakia
kwake kwa anwani ya kuwa inawafikiana na ihtiyaat si kwa anwani ya taqliid. Mas’ala 27: Ikiwa mukallaf
atamfuata mtu ambae si mwenye uwezo wa kutoa fat’wa kisha akalifahamu hilo ni wajibu juu yake kuhama, na matendo yake aliyoyafanya mwanzo ni sawa na matendo ya
jaahili alie fanya matendo yake bila ya taqliid. Na pia itakuwa ni wajibu
kutokana na kauli yenye nguzu zaidi kuhamia kwa alie kuwa Aalam kwa yule ambae
alikuwa akimfuata asie kuwa Aalam, au alikuwa akimfuata Aalam kisha baadae
mwingine akawa ni Aalam zaidi yake. Mas’ala 28: Ikiwa suala la
Aalamiyya (Mjuzi zaidi) litafungika kwa watu wawili na haikuwezekana
kumuainisha mmoja wapo kuwa ni Aalam zaidi- kwa sababu kwa kila mmojawapo
kunaihtimali ya kuwa ni Aalam- hapa hukumu yake ni kumfuata yeyote kati yao bila kipingamizi, sawa iwezekane kufanya ihtiyaat kati ya kauli mbili za watu hao au
laa. Mas’ala 29: Alie chukuwa uwakala
wa kufanya matendo badala ya mtu mwingine atafanya matendo yale kwa mujibu wa
taqliid ya alie mchukulia uwakala na si kwa mujibu wa taqliid yake ikiwa wanatofautiana
katika Mujtahidi, ama alie usiwa (Wasii) kwa mfano lau kama atakuwa ni mwenye
kuusiwa kukodisha watu wa kusali sala kwa niaba yake hapo ni wajibu matendoyake
yawe sawa au kwa mujibu wa fat’wa za Mujtahidi wake. Mas’ala 30: Mtu alie idhinishwa na
kupewa uwakala na Mujtahidi wa kutumia au kusimamia mali ya waqfu au mali ya
watoto wasio na walii humalizika idhini hiyo au uwakala huo kwa kufariki
Mujtahidi yule, tofauti na mtu alie teuliwa na kupewa jukumu na Mujtahidi la
kusimamia vitu vya waqfu au usimamizi wa watoto au wendawazimu wasio kuwa na
msimamizi( walii), hakika yeye usimamizi wake na uangalizi wake haubatiliki
kwa kauli iliyo dhahiri. Mas’ala 31: Ni wajibu kwa
mukallaf kufahamu sehemu zote za ibada na masharti yake na vizuizi vyake na
vitangulizi vyake hata kama ni kwa sura ya ujumla, kiasi kwamba awe anafahamu
yakuwa ibada yake imetimiza sehemu zote na masharti yote na haina vizuizi. Mas’ala 32: Ikiwa yatamtokea
mukallaf mas’ala fulani ambayo hajui hukumu yake na akiwa katikakati ya sala
inajuzu kwake kufanya tendo lake kwa kufuata upande mmoja wapo kati ya pande
mbili za mas’ala hayo, akikusudia kuuliza hukumu yake baada ya sala na akiwa
ameazimia kuirudia sala hiyo ikiwa haikuwafikiana na ukweli ulivyo wa kisheria,
na lau kama tendo lake litakuwa sambamba na hukumu ya kisheria haitakuwa ni
wajibu kwake kuirudia. Mas’ala 33: Kama ambavyo ni
wajibu kufanya taqliid katika mambo ya wajibu na haraam, pia ni wajibu katika
mambo ya sunna ambayo kunaihtimali ya kuwa ni wajibu, na katika mambo ya
makruuh na mubaha ( si wajibu wala haram) yenye ihtimali ya kuwa yanaulazima wa
kutekelezwa. Mas’ala 34: Tamko ( Ahwat) lililo
tajwa katika kitabu hiki linakusudiwa kwa maana ya ihtiyaat ya sunna ikiwa
limetanguliwa na limefuatiwa na fat’wa, laa sivyo lina maana ya ihtiyati ya
wajibu, na maana yake ni kuwa mukallaf wakati huo anahiari kati ya kufanya
tendo hilo na kati ya kurejea kwa Mujtahidi mwingine pamoja na kuchunga suala
la alie kuwa Aalam (mjuzi zaidi), tofauti na ihtiyaati ya sunna, haijuzu katika
ihtiyaati hiyo kurejea kwa mwinginewe, bali mukallaf ana hiari kati ya kufanya
kwa mujibu wa ihtiyaati hiyo au kufanya kwa mujibu wa fat’wa iliyo tangulia au
ifuatayo. Mas’ala 35: Ikiwa mukallaf
atafunga mkataba au kufanya makubaliano na mtu fulani au akafanya tendo fulani
kwa mijibu wa taqliidi ya Mujtadi anae hukumu ya kuwa mkataba huo na matendo
hayo ni sahihi kisha Mujtahidi huyo akafa, na akamfuata anae sema ya kuwa
mkataba huo ni batili inajuzu kwa mukallaf huyo kujengea kuwa matendo yake
yaliyo tangulia ni sahihi.
KITABU TWAHARA (MLANGO WA TWAHARA)
KATIKA MLANGO HUU KUNA SEHEMU TOFAUTI
SEHEMU YA KWANZA
MGAWANYIKO WA MAJI NA HUKUMU ZAKE
NA KATIKA SEHEMU HII KUNA VIFUNGU KADHAA
KIFUNGU CHA KWANZA
MAJI YAMEGAWANYIKA SEHEMU MBILI
SEHEMU YA KWANZA:
Maji Mutlaq,
hiki ni kitu chenye kutiririka na ambacho huitwa kwa jina la (Maji) bila
kuongeza kitu, kama maji yaliyopo kwenye kisima au mto au bahari. Na tusemapo
maji ya bahari au maji ya mto au maji ya kisima husema hivyo kwa ajili ya
kuyapambanua, si kwa sababu ya kusahihisha matumizi.
SEHEMU YA PILI:
Maji mudhaaf,
ni kitu chenye kutiririka ambacho haifai kuitwa kwa jina la (maji) pekee, bali
huongezewa neno lingine kama ifuatavyo: Maji ya komamanga kwa mfano, au maji ya
waridi kwa kutaja jina lililo dhifiwa kwenye tamko maji. Na pengine huitwa (Maji)
kwa majazi, kwa sababu hii inafaa kuto tumia neno maji kwenye neno hilo.
KIFUNGU CHA
PILI:
MAJI MUTLAQ
(Maji halisi) NA HUKUMU ZAKE
Maji mutlaq
yamegawanyika sehemu zifuatazo: 1-Maji yenye kutiririka. 2- Maji ya
chemchem yasiyo tiririka. 3- Maji ya kisima. 4- Maji ya mvua. 5- Maji ya
kuri moja 6- Maji kidogo (yasiyo fikia kiwango cha kuri moja).
Mas'alal 36: Maji
mutlaq na mgawanyiko wake wote kama hayakuingiwa na najisi ni twahara na ni
yenye kutwahirisha hadathi na khabathi.
Mas'ala 37:Maji
mutlaq na mgawanyiko wake wote hata maji yenye kutiririka ikiwa
yatabadilika na kugeuka moja ya sifa zake tatu kwa kuingiwa na najisi
hunajisika, Na sifa hizo ni rangi ladha na harufu. Na maji kidogo
yananajisika tu kwa kuingiwa na najisi.
Mas'ala 38: Ikiwa
maji yatabadilika na ubadilikaji huo haukuwa ni katika moja kati ya sifa
zake tatu, rangi ladha na harufu, kama yakibadilika uzito wake na mfano wa
hayo, maji hayo hayata najisika ikiwa hayakubadilika na kuwa maji
mudhaafu.
Mas'ala 39: Ikiwa
rangi ya maji itabadilika au ladha yake au harufu yake kwa kukaribiana na
najisi, kama mzoga ukiangukia karibu na maji hayo na mzoga huo ukawa
ukingoni mwa maji hayo hayatanajisika vile vile.
Mas'ala 40: Ikiwa
maji hayakubadilika kwa najisi maji hayo si najisi, kama yakibadilika kwa
kitu kilicho najisika, kama ikiwa yatabadilika na kuwa ya njano au mekundu
kwa kuingiwa na juisi iliyo najisika.
Mas'ala 41: maji
hayanajisiki tu kwa kuingiwa na najisi au kubadilika kwa kuingiwa na najisi
yenyewe, bali ikiwa yataingiwa na kitu chenye najisi au kilicho beba
sehemu na chembe chembe za najisi, au kitu hicho kina chembe chembe za najisi na
maji yale yakabadilika na kugeuka kwa najisi ile, maji hayo yatanajisika
pia.
Mas'ala 42: Inatosha
kunajisika kwa maji kubadilika kwake kwa sababu ya kuingiwa na najisi hata kama
hayakubadilika sifa zake zote, kwa mfano lau kama maji hayo yatabadilika
rangi yake na kuwa rangi ya njano au nyekundu kwa kuingiwa na damu, au yakawa na
harufu iliyo kinyume na harufu ya mkojo na haja kubwa kwa kuangukia najisi hizo
kwenye maji hayo, maji hayo yatakuwa yamenajisika pia.
KIFUNGU CHA TATU
MAJI YENYE KUTIRIRIKA NA HUKUMU ZAKE
Haya ni maji yenye
kutiririka na yaliyo ungana na mada ya ardhini au nyingineyo hata kama hayatoki
na kuchimbuka ardhini.
Mas'ala 43: Maaul
jaariy (maji yenye kutiririka) sawa yawe ni kiasi cha kuri moja au yawe ni kiasi
kidogo kuliko kuri, na sawa utiririkaji wake uwe ni wa kuchupa au kunyunyiza,.
hayanajisiki kwa kuingiwa na najisi kama hayajabadilika sifa zake.
Na huambatanishwa na
maji yenye kutiririka katika hukumu ya kuto najisika kwa kuingiwa na najisi bila
kubadilika, maji yote yachimbukayo ardhini hata kama hayatiririki.
Mas'ala 44: Ikiwa
maji yenye kutiririka juu ya ardhi bila ya kuwa na asili ichimbukayo ardhini
au yenye kunyunyiza, ikiwa majio hayo yatakuwa ni machache zaidi kuliko
kuri ya maji, hakika maji hayo hunajisika kwa kuingiwa tu na najisi.
Ama ikiwa mukallaf
atatia shaka ya kuwa maji hayo yana chimbuko (mada) au laa kauli yenye
nguvu inasema kuwa hayata najisika maji hayo kwa kuingiwa au kukutana na
najisi ikiwa hapo kabla hayakutanguliwa na hali ya kuto kuwa na mada.
Mas'ala 45:
Kizingatiwacho katika kuto najisika maji yatiririkayo ni kuungana kwake na mada
(asili kama chemchem au kuungana na bomba), kwa mfano lau kama mada au asili ya
kutiririka kwa maji hayo iko juu, na mada yenye kutiririsha au
kunyunyiza maji hayo itakuwa ni chini ya kuri moja maji hayo yatanajisika,
ndio ikiwa sehemu inayo nyunyiza au asili ya maji hayo itagusana na najisi maji
hayo hayatanajisika.
Mas'ala 46: Maji
yaliyo tuwama na yaliyo ungana na maji yenye kutiririka hukumu yake ni sawa na
maji yenye kutiririka katika hukumu ya kuto najisika kwake kwa kugusana au
kuingiwa na najisi au kitu kilicho najisika, kwa mfano hodhi lililo ungana na
mto kwa ajili ya umwagiliaji, maji yake hayanajisiki kwa kugusana na najisi,
vile vile kingo za mto hata kama maji yake yametuwama na
hayatiririki.
Mas'ala 57: Ikiwa
baadhi ya sehemu ya maji yenye kutiririka itabadilika na sehemu nyingine
isibadilike, sehemu ya maji hayo iliyo ungana na mada hainajisiki kwa
kuungana au kuingiwa na najisi hata kama maji yake ni machache, na upande
mwingine hukumu yake ni sawa na hukumu ya maji yaliyo tuwama ikiwa maji ya
sehemu hiyo yatabadilika, laa sivyo yatahesabiwa yamenajisika kiwango kilicho
badilika pekee, kwa kuungana yale mengine na mada.
KIFUNGU CHA NNE
MAJI YALIYO TUWAMA NA HUKUMU ZAKE
Mas'ala 48: Maji
yaliyo tuwama bila kuungana na mada ikiwa kiwango chake hakifikii kuri moja
hakika maji hayo yananajisika kwa kuingiwa na najisi, tofauti na ikiwa yanafikia
kuri moja, hakika yakiwa ni kuri moja hayanajisiki kwa kuingiwa au
kukutana na najisi isipokuwa yatakapo badilika moja kati ya sifa zake
tatu.
Mas'ala 49: Kiwango
cha kuri kwa uzito ni sawa na huqqa ya istambuli 280, ama ukubwa wake ni sawa na
shibiri 34 kasoro moja ya tatu, na kwa lita ni sawa na lita 377
takriiban.
Mas'ala 50: Maji
yakiwa ni chini ya kuri moja hata kama ni kwa kiasi kichache hukumu yake ni sawa
na hukumu ya ya maji kidogo.
Mas'ala 51:Ikiwa
najisi itaangukia kwenye kuri na haikujulikana ya kuwa imeangukia humo kabla ya
kufika kuri au baada ya kukamilika kuri, maji hayo yatahukumiwa kuwa ni twahara,
isipokuwa ikiwa itafahamika tarehe ya kuangukia kwake humo na tarehe ya kufikia
kwake kuri haikujulikana.
Mas'ala 52:
Ikiwa imefikia kuri lakini haikujulikana ya kuwa ni maji mutlaq (ni maji halisi)
au mudhaaf, na yakaingiwa na najisi, maji hayo hayata hukumiwa kuwa ni
najisi, isipokuwa itakapo kuwa hali yake ya mwanzo ilikuwa ni mudhaaf na
kukawa na shaka ya kuwa bado ni mudhafu.
Na ikiwa
kunakuri mbili moja ni mutlaq na nyingine ni mudhaaf, na ikafahamika kuingiwa na
najisi moja kati ya kuri hizo mbili lakini haijulikani kuwa ni ipi kati ya
kuri hizo, zote mbili zitahukumiwa kuwa ni twahara pia.
KIFUNGU CHA TANO
MAJI YA MVUA NA HUKUMU ZAKE
Mas'ala 53:
Hukumu ya maji ya mvua wakati ikinyesha ni sawa na hukumu ya maji yenye
kutiririka, hayata najisika kwa kugusana na najisi ikiwa hayajabadilika moja
kati ya sifa zake, hata kama mvua hiyo ni kidogo, sawa maji hayo
yatiririke kwenye mifereji au juu ya ardhi au laa, la muhimu ni kuthibiti kuwa
ni maji ya mvua, na ikiwa yatakusanyika sehemu moja na kikaoshewa ndani
yake kitu kilicho najisika kitu hicho kitatwahirika hata kama maji yale
yatakuwa ni madogo.
Haya yote ni wakati
mvua ikiendelea kunyesha, na ikiwa mvua itakatika na kuacha kunyesha
hukumu yake ni sawa na hukumu ya maji yaliyo tuwama.
Mas'ala 54: Nguo
iliyo najisika na zulia lililo najisika ikiwa vitu viwili hivi
vitanyeshewa na mvua na maji kuingia ndani ya vitu hivyo basi vitu hivyo
vyote vitatwahirika, na haihitaji kukamua au kuosha kwa mara kadhaa, na
ikiwa maji yatafika kwenye baadhi ya sehemu na hayakuenea sehemu zote
itatwahirika sehemu zilizo fikiwa na mvua hiyo na si vinginevyo. Na hukumu
hii inahusika tu ikiwa hakuna najisi yenyewe kwenye vitu hivyo, laa sivyo
havitwahiriki isipokuwa vitakapo nyeshewa tena baada ya kuondoka najisi yenyewe
kwenye vitu hivyo.
Mas'ala 55: Ardhi
iliyo najisika hutwahirika kwa kunyeshewa na mvua kwa sharti kwamba mvua hiyo
iinyeshee moja kwa moja kutoka mawinguni hata kama ni kwa kupeperushwa na
upepo, ama ikiwa mvua hiyo itanyeshea juu ya kitu kingine – kama ambavyo
maji hayo yatatiririkia juu ya ardhi baada ya kuangukia mahali pengine na
kuingiwa na najisi- katika hali kama hii haita twahirika.
Ndio ikiwa mvua
hiyo itanyesha juu ya ardhi kisha maji yake yakatiririkia juu ya paa basi sehemu
hiyo itatwahirika.
Mas'ala 56: Ikiwa
maji ya mvua yataangukia kwenye najisi yenyewe kisha yakadondokea kwenye kitu
kingine, kitu hicho hakita najisika ikiwa maji hayo hayakuwa na chembe chembe za
najisi ndani yake na hayakubadilika kwa najisi.
Mas'ala 57: Mchanga
ulio najisika hutwahirika kwa kunyeshewa na mvua ikiwa mvua hiyo itaingia hadi
ndani ya mchanga huo na kubadilika kuwa udongo.
Mas'ala 58: Jamvi
lililo najisika linatwahirika kwa kunyeshewa na mvua, vilevile zulia lililo
tandikwa juu ya ardhi, na ardhi iliyopo chini ya zulia hilo ikiwa ni najisi
hutwahirika ikifikiwa na maji ya mvua. Ndio ikiwa jamvi au zulia havikuwa
juu ya ardhi au kukawa na utengano, hapo kuna ishkaali katika hukumu ya
kutwahirika kwake kwa kunyeshewa na mvua, kwanza kwa kunyeshea mvua juu ya jamvi
au zulia kisha maji hayo yakadondokea juu ya ardhi.
Mas'ala 59: Chombo
ambaacho nbi najisi kinatwahirika ikiwa maji ya mvua yatafika sehemu zote
zenye najisi katika chombo hicho isipokuwa ikiwa kimenajisika kwa kuliwa na mbwa
ndani yake, katika hali kama hiyo kutwahirika chombo hicho kwa kunyeshewa na
mvua tu bila ya kukisugua au kukiosha kwa mchanga kuna ishkaali, lakini ikiwa
kitanyeshewe na mvua baada ya kukisugua au kukiosha kwa mchanga wakati huo
kitatwahirika bila ya kuhitajia kuosha mara kadhaa.
KIFUNGU CHA SITA
MAJI YA BAFUNI NA HUKUMU YAKE
Mas'ala 60: Maji ya
bafuni ni sawa na maji yenye kutiririka kwa sharti kuwa yawe yameungana na mada,
kwa mfano maji yaliyoko kwenye mahodhi madogo ikiwa yataungana na mada
hayanajisiki kwa kuingiwa na najisi ikiwa maji yaliyoko kwenye hodhi pekee au
kwa kuyaunganisha na yaliyomo kwewnye mada yanafikia kuri.
Mas'ala 61:Ikiwa maji
yaliyomo kwenye mahodhi madogo yatanajisika yanatwahirika kwa kuungana na mada
kwa sharti kwamba maji ya mada yawe ni kuri na yachanganyike pia.
KIFUNGU CHA SABA
MAJI YA KISIMA NA
HUKUMU ZAKE
Mas'ala 62: Hukumu ya
maji ya kisima yenye kuchimbuka ardhini ni sawa na hukumu ya maji yenye
kutiririka katika hukumu ya kuto najisika isipokuwa kwa kubadilika moja kati ya
sifa zake, sawa yawe ni kiasi cha kuri moja au chini ya hapo, na ikiwa
yatabadilika kisha ubadilikaji huo ukaondoka na kutoweka wenyewe maji hayo
yatatwahirika kwa sababu yana mada na yamechanganyika na maji yatokayo kwenye
mada kama chemchem. Ama yakiwa hayana mada yenye kuchimbuka basi itazingatiwa
kiasi cha kuri katika hali ya kutonajisika kwake hata kama kitaitwa
kisima, kama mfano wa visima ambavyo hukusanyika ndani yake maji yasiyo
chimbuka ardhini.
Mas'ala 63:
Maji najisi yaliyo tuwama sawa maji hayo yawe ni kuri au
kidogo yanatwahirika kwa kuungana na maji ya kuri yaliyo twahara au kwa
kuungana na maji yenye kutiririka au maji yenye kuchimbuka ardhini hata kama
hayatiririki na kuchanganyika na maji hayo, na pia hutwahirika kwa kukutana na
kuchanganyika na maji ya mvua, na kauli ya ahwat ni kuwa kutazingatiwa
kuchanganyika kwa maji hayo.
Mas'ala 64: Birika
lililo jazwa maji yaliyo najisika ikiwa litazamishwa kwenye hodhi
hutwahirika baada ya kuchanganyika maji hayo, na si wajibu kuyamwaga maji yake
na kuliosha birika hilo.
KIFUNGU CHA NANE
MAJI YALIYO TUMIKA YAKIWA NI MACHACHE
Mas'ala 65: Maji
yaliyo tumika kutawadhia ni twahara na yanatwahirisha hadathi na khabathi,
vile vile maji yaliyo tumika katika ghusli ya sunna, ama maji yaliyo tumika
katika ghusli ya hadathi kubwa pamoja na kuwa mwili hutwahirika hakuna ishkaali
katika utwahara wa maji hayo na juu uwezekano wa kuyatumia kuondolea
khabathi, na kauli yenye nguvu zaidi ni kuwa inajuzu kuyatumia kuondolea hadathi
pia japokuwa kauli ya ahwati ni kuwa nivema kujiepusha na maji hayo.
Ama maji yaliyo
tumika kuondoa khabathi tofauti na maji yaliyo tumika kustanji haijuzu kuyatumia
katika udhu na ghusli, na kauli yenye nguvu zaidi ni kuwa maji yatumikayo
kuondolea najisi yenyewe ni najisi, bali hata maji yaliyo tumiwa kuoshea yasiyo
ondoa najisi, ama maji ya kustanjia hukumu yake itafuatia.
Mas'ala 66: Hakuna
ishkaali katika matone ambayo hudondokea kwenye chombo wakati wa kuosha hatakama
tutasema ya kuwa haijuzu kutumia maji yaliyo oshewa hadathi kubwa. Na maji
yanayo bakia kwenye nguo baada ya kukamuliwa nguo hiyo ni twahara, ikiwa maji
hayo yatatoka baada ya nguo hiyo kukamuliwa hayata ambatanishwa na hukumu ya
maji yaliyo oshewa.
Na mkono
hutwahirika kwa kufuata kitu kinacho twahirishwa baada ya kukitwahirisha kitu
hicho, kwa hivyo hakuna haja ya kuiosha mikono hiyo, pia chombo ambacho hutumika
kuoshea nguo na mfano wa hivyo.
KIFUNGU CHA TISA
HUKUMU YA MAJI YENYE KUTILIWA SHAKA
Mas'ala 67: Maji
ambayo hutiliwa shaka ya kuwa ni najisi au twahara maji hayo ni twahara ikiwa
haikujulikana ya kuwa hapo kabla yalikuwa ni najisi, ama maji ambayo hutiliwa
shaka ya kuwa ni mutlaq au hapana hayahukumiwi maji hayo kuwa ni mutlaq
isipokuwa ikiwa hapo kabla yalikuwa ni mutlaq.
Ndio, ikiwa maji hayo
ni kuri moja na yakaingiwa na najisi hayatahukumiwa kuwa ni najisi isipokuwa
ikiwa hapo kabla yalikuwa ni maji mudhaaf, ama maji ambayo yanatiliwa shaka ya
kuwa ni mubaha au hapana (maji halali) maji hayo hukumu yake ni kuwa ni mubaha,
aisipokuwa ikiwa hapo kabla yalikuwa ni milki ya mtu mwingine au yalikuwa katika
milki ya mtu mwingine ambae kuna ihtimali kuwa ni maji yake.
Mas'ala 68: Ikiwa
mukallaf atafahamu kwa sura ya ujumla ya kuwa mojawapo kati ya vyombo
viwili ni najisi na kingine ni twahara haitajuzu kutumia chombo moja wapo
kuondolea khabathi au hadathi.
Mas'ala 69: Chombo
kinacho shukiwa kuwa sehemu moja wapo ya chombo hicho imenajisika hakita
hukumiwa kuwa ni najisi isipokuwa hali ya sehemu hiyo ya hapo kabla
itajulikana kuwa ilikuwa ni najisi, lakini kauli ya ahwat inasema kuwa ni bora
kujiepusha na utumiaji wa chombo hicho.
Mas'ala 70: Ikiwa
maji mutlaq yatafanana na mudhaaf itajuzu kuyatumia maji hayo kuondolea khabathi
kwa kutumia moja wapo kati ya maji hayo na kuoshea kwa kutumia maji mengine,
vile vile katika kuondoa hadathi.
Mas'ala 71: Ikiwa
itafahamika kwa sura ya ujumla ya kuwa maji haya ima ni najisi au
ni mudhaaf inajuzu
kuyanywa maji hayo, lakini haijuzu kuyatumia kutawadhia, vile vile ikiwa
itajulikana ya kuwa ima maji hayo ni mudhaaf au ni maghsuub (ya kunyang'anya).
Ama ikiwa
itajulkikana ya kuwa maji hayo ni najisi au ni ya kunyang'anya haitajuzu
kuyanywa, kama ambavyo haitajuzu kuyatumia kutawadhia.
Mas'ala 72: Ikiwa
sehemu au pande zitiliwazo shaka au zenye shubha hazijulikani kidhati, katika
hali kama hii inajuzu kuyatumia maji hayo bila kipingamizi.
KIFUNGU CHA KUMI HUKUMU ZA MAJI MUDHAAF
Mmas'ala 73: Maji
mudhaaf, kama maji ya uwa waridi ni twahara ikiwa hayakuingiwa na najisi, lakini
maji hayo si yenye kutwahirisha hadathi, vilevile si yenye kutwahirisha
khabathi hata katika hali ya dharura.
Mas'ala 74: Maji
mudhaaf yana najisika kwa kuingiwa tu na najisi sawa yawe mengi au kidogo,
isipokuwa yakiwa ni yenye kuchupa kwa nguvu juu ya najisi, hata kama
yanatoka chini kwenda juu kama maji yatokayo kwenye bomba lenye
kunyunyizia na mfano wa hiyo, katika hali kama hii itahukumiwa kuwa ni
najisi sehemu ile tu iliyo gusana na najisi, na haivuki na kuelekea
juu.
Mas'ala 75: Ikiwa
maji mudhaaf yatanajisika hayatatwahirika isipokuwa kwa kuyaweka kwenye
kuri au kwenye maji yenye kutiririka na kutoweka hali ya kuwa kwake maji
mudhafu. Na kutwahirika kwa maji mudhaaf yaliyo najisi kwa
kuyachemsha ( au kuongeza kiwango cha maji hayo) kuna ishkaali.
KIFUNGU CHA KUMI NA
MOJA MABAKI YA CHAKULA
Mas'ala 76: Mabaki ya
chakula yote ni twahara isipokuwa mabaki ya mnyama alie najisi (najisul aini)
kama mbwa Nguruwe na mushrik (kafir) , hakika mabaki yao ni najisi.
Mas'ala 77:
Nimakuruhu kula mabaki ya mnyama asie liwa isipokuwa mabaki ya Muumini na paka
kutokana na kauli ya baadhi ya mujtahidiin.
SEHEMU YA PILI: HUKUMU ZA CHOONI
PIA KUNA VIFUNGU KADHAA
KIFUNGU CHA KWANZA
HUKUMU ZA KWENDA CHOONI
Mas'ala 78: Ni wajibu
wakatio mtu anapokwenda chooni au katika hali ya kujisaidia haja kubwa bali hata
katika hali nyingine tofauti kusitiri uchi (sehemu za siri) – nazo ni sehemu ya
mbele na nyuma na peke mbili- kwa muonaji mwenye kuheshimiwa, isipokuwa mtoto na
mwenda wazimu wasio weza kupambanua, na mke na mume na alie milikiwa kwa mmiliki
wake na alie halalishwa kwa alie halalishiwa, hakika kwa watu hawa inajuzu kwa
kila mmoja wao kuangalia uchi wa mwenziwe.
Mas'ala 79: Hakuna
tofauti katika uharamu wa kuangali kati ya uchi wa Muislaam au kafiri
kutokana na kauli ya ahwat.
Mas'ala 80: Si wajibu
kusitiri mapaja mawili wala matako wala nywele ziotazo pembezoni mwa sehemu za
siri (mavuzi). Ndio, ni sunna kusitiri sehemu zilizoko kati ya kitovu na
magoti.
Mas'ala 81: Haijuzu
kuangalia uchi wa mtu mwingine kwa kutumia kioo na mfano wa hicho, wala kwa
kutumia kioo cha kujitizamia na wala haijuzu kuangalia kwa kutumia maji
yaliyo safi.
Mas'ala 82: Ikiwa mtu
itamlazimu kuangalia uchi wa mtu mwingine kama katika hali ya kumtibu mgonjwa,
kauli ya ahwat ni kuwa ataangalia kupitia kioo kilicho wekwa mbele yake ikiwa
kufanya hivyo kutatosheleza na kuondoa dharura hiyo, laa sivyo hakuna
tatizo kuangalia.
Mas'ala 83: Ni haramu
kwa mwenye kujisaidia haja kubwa – wakati wa kujisaidia- kuelekea Qibla na
kukipa mgongo Qibla kwa kuielekeza sehemu ya mbele ya mwili wake kwenye
Qibla hata kama uchi wake atauelekeza sehemu au upande mwingine tofauti na
sehemu hizo mbili, na kauli ya ahwat ni kuwa ataacha kukielekezea
uchi wake pekee hata kama sehemu za mbele za mwili wake zitaelekea sehemu
hizo mbili, na makusudio ya sehemu za mbele za mwili ni kifua tumbo na magoti
mawili, na ikiwa italazimika kufanya moja wapo atakuwa na hiari japokuwa kauli
ya ahwat ni kuwa atakipa mgongo, na akiwa itamlazimu kufanya kitendo kimoja
wapo kati ya mambo mawili hayo na kuto jisitiri pamoja na kuwepo
muangaliaji mwenye kuheshimiwa itawajibika kwake kujisitiri.
Mas'ala 84: Kauli
yenye nguvu ni kuwa si haramu kukielekea au kukipa mgongo kibla katika hali ya
kufanya istibraa na katika hali ya kustanji japo kuwa kutofanya hivyo ni ahwat
(bora zaidi). Ndio ikiwa atafahamu ya kuwa mkojo utatoka kwa kufanya
istibraa kauli ya ahwat ni kuwa itawajibika kuacha kukielekea au kukipa mgongo
Qibla.
Mas'ala 85: Lau kama
mukallaf atapatwa na shubha katika kukipambanua Qibla hukumu ya kutumia dhanna
haiko mbali pamoja na kuto kuwepo uwezekano wa kukitafuta na kufanya uchunguzi
wa sehemu ya Qibla, na ikiwa kuichelewesha sala kutamsababishia
matatizo.
Mas'ala 86: Ni haramu
kujisaidia haja kubwa kwenye milki ya mtu mwingine isipokuwa kwa idhini yake,
vile vile ni haramu kujisaidia kwenye makaburi ya waumini ikiwa kufanya hivyo ni
kuvunja heshima yao.
Mas'ala 87: Ni haramu
kujisaidia haja kubwa kwenye mashule na mfano wa hayo ikiwa haikufahamika kuwa
sehemu hizo zimewekwa waqfu kwa ajili ya watu wote, na inatosha idhini ya
msimamizi wa waqfu hizo, na kauli iliyo dhahiri ni kutosheka na ada ya
watu ikiwa kufanya kwao kutakupa matumaini ya kuwa ni sehemu ya matumizi
ya watu wote, vile vile hali ni hiyo hiyo kwenye matumizi mengine ya vitu hivyo
vya waqfu.
KIFUNGU CHA PILI
KUSTANJI
Ni wajibu kuosha
sehemu ya kutokea mkojo kwa maji, na inatosha kuosha mara moja japo kuwa kauli
ya ahwat ya sunna ni kuosha mara kadhaa, na haitoshelezi kitu kingine tofauti na
maji, na sehemu ya haja kubwa ikiwa haja itavuka mahali pake na kutapakaa hapo
italazimika kutumia maji pekee kama najisi nyingine, na ikiwa hakikuvuka mahali
pake mukallaf anahiari ya kuosha kwa maji hadi kusafike mahali hapo, na kati ya
kupangusa kwa kutumia mawe au kitambaa au mfano wa hivyo kati ya vitu
vyenye kuondoa najisi, na maji ni bora zaidi, na kutumia vyote ndio
ukamilifu wa twahara.
Mas'ala 88: Je
kupangusa kwa mawe na mfano wa hilo inasababisha kutwahirika mahala hapo au
kusamehewa kwenye sala pekee? Katika kupangusa kuna ishkaali, na kauli ya ahwti
ni ya pili ( yaani ni sababu ya kusamehewa kwenye sala)
Mas'ala 89: Katika
kupangusa huzingatiwa kutumia mawe matatu au mfano wa hayo, au kutumia pande
tatu za jiwe moja na mfano wa hilo japo kuwa kuna uwezekano wa kusafika kwa
kutumia chini ya mawe matatu, na kama hapakusafika mahala hapo kwa mawe matatu
ataongeza mpaka pasafike mahali hapo.
Mas'ala 90: Ni wajibu
mawe yatumikayo au mfano wake yawe twahara.
Mas'ala 91: Ni haramu
kustanji kwa kutumia vitu vyenye kuheshimiwa, vile vile ni haramu kutumia mifupa
na kinyesi. Na lau kama mtu atastanji kwa kutumia vitu hivyo atazingatiwa
kuwa ameasi, na kutwahirika au kusameheka kwa kutumia vitu hivyo kuna
ishkaal.
Mas;ala 92: Ni wajibu
katika hali ya kuosha kwa maji kuondoa najisi yenyewe na athari zake kwa
maana kuwa kuondoa chembe chembe ndogo ambazo hazionekani na kwa kawaida
haziondoki isipokuwa kwa kutumia maji, na si wajibu kuondoa rangi na harufu, na
inatosha katika upangusaji kuondoa najisi yenyewe, na si wajibu kuondoa
athari za najisi, na ikiwa haja kubwa itatoka ikiwa na najisi nyingine isiyo
kuwa hiyo kama damu au mahali pa haja kubwa pakagusana na najisi nyingine kutoka
nje haitatosheleza kuitwahirisha sehemu hiyo ispokuwa kwa kutumia maji, na
lau kama atatia shaka ya kuwa imetwahirika sehemu hiyo au laa atajengea ya kuwa
haikutwahirika na hapa atakuwa na hiayari kati ya kutumia maji mawe na
mfano wa vitu viwili hivyo.
KIFUNGU CHA TATU
ADABU ZA KWENDA CHOONI
Ni sunna kwa mwenye
kujisaidia haja kubwa kujitenga na watu au kwenda sehemu ya mbali ambayo
hatoweza kuonekana, na katika haja ndogo atafute sehemu yenye muinuko, kama
ambavyo ni sunna kwake kufunika kichwa na kufunga kitambaa shingoni, na kufunika
kicha na nyingo kwa kilemba au kitambaa kunatosheleza kufunika kichwa, na
ni sunna kutanguliza mguu wa kulia wakati wa kutoka, na kufanya istibraa, na
kujitegemeza kwenye mguu wake wa kushoto – wkati wa kukaa- na kupanua mguu
wa kulia, na ni makruuhu kujisaidia barabarani, njiani, chini yamiti ya
matunda, na sehemu za kulaaniwa, kama kwenye milango ya majumba na mfano wa
sehemu hizo kati ya sehemu ambazo mwenye kujisaidia sehemu hizo anakuwa
amejisababishia watu kumlaani, na sehemu zilizo andaliwa kwa ajili ya vituo vya
misafara, na kulielekea jua au mwezi kwa utupu wake, na kula na kunywa katika
hali ya kujisaidia, na mengineyo kati ya mambo yaliyo tajwa na maulamaa radhi za
mwenyezi mungu ziwe juu yao, japo kuthibiti kwa baadhi ya mambo yaliyo tajwa
kuwa ni ya sunna au makruuhu kuna ishkaali.
Mas'ala 93: Maji ya
kustanjia ni twahara hata kama yamestanjiwa sehemu ya kutokea mkojo ikiwa
yatatimia masharti haya yafuatayo:
1- Kuto badilika rangi,
ladha na harufu ya maji hayo kwa najisi.
2- Kuto ingiwa na najisi
nyingine kutoka nje tofauti na mkojo.
3- Kuto vuka najisi
itokayo kwenye sehemu yake ya kawaida.
4- Haja kubwa na ndogo
isitoke pamoja na najisi nyingine kama damu, isipokuwa ikiwa itatoka
lakini si yenye kuonekana katika hali hiyo hakuna tatizo.
5- Kusiwe na chembe
chembe za haja kubwa zenye kuonekana kwa kauli ya ahwat.
Kwa kukamilika
masharti haya maji ya kustanjia yanakuwa ni twahara na yanaweza kutumika
kuondolea khabathi, lakini haijuzu kuyatumia kuondolea hadathi wala
kuyatumia kwenye udhu wa sunna na ghusli ya sunna.
KIFUNGU CHA NNE ISTIBRAA
Namna ya kufanya
istibraa ya mkojo ni kama ifuatavyo, kwanza uta pangusa kuanzia kwenye makalio
(yaani mwanzoni mwa sehemu itokeapo haja kubwa) hadi mwanzoni mwa kiungo cha
kiume mara tatu, kisha uta anzia mwanzoni mwa kiungo cha kiume hadi kwenye
kichwa cha uume mara tatu, na mwisho utakikamua kichwa mara tatu.
Na faida ya istibraa
huonekana pale utakapo kuhukumiwa kuwa ni twahara unyevu nyevu
utokao baada ya kufanya istibraa unao shukiwa kuwa ni mkojo au laa, na umaji
maji huo ukitoka si wajibu kutawadha, na lau kama utatoka umaji maji unao
shukiwa kuwa ni mkojo kabla ya kufanya istibraa – hata kama mukallaf aliacha
kufanya istibraa kutokana na dharura na kutoweza kufanya hivyo- atajengea kuwa
ni mkojo, na itawajibika kujitwahirisha kwa kutoka umaji maji huo na
kumlazimu kutawadha.
Na huambatanishwa na
istibraa katika faida zilizo tajwa muda wote ambao anayakini kuwa hakuna chembe
chembe zilizo bakia kwenye mirija itoayo mkojo, na mwanamke hafanyi istibraa, na
umaji maji utokao kwenye sehemu zake za siri unahukumiwa kuwa ni twahara na kuwa
hautengui twahara ikiwa haikutambulika kuwa ni mkojo. Ndio ni bora zaidi kwa
mwanamke kusubiri kidogo- baada ya kukojoa – na kukohoa kohoa na kujikamua utupu
wake (sehemu zake za siri) kwa upana kisha kuiosha kwa maji.
Mas'ala 94: Faida za
kufanya istibraa hupatikana katika istibraa hata kama ni kwa kufanywa na mtu
mwingine kama mkewe au mtu alie milikiwa (mjakazi au mtumwa).
Mas'ala 95: Ikiwa
mukallaf atatia shaka ya kuwa amefanya istibraa au amestanji atajengea kuwa
hakufanya hata kama ni kawaida yake kufanya, na ikiwa atatia shaka mtu ambae
hakufanya istibraa ya kuwa umetoka umajimaji atajengea kuwa haukutoka hata kama
atakuwa anadhania kuwa umetoka umajimaji.
Mas'ala 96: Ikiwa
atafahamu ya kuwa amefanya istibraa au amestanji na akatia shaka ya kuwa
amefanya istibraa au amestanji sawa sawa au laa atajengea kuwa ni
sahihi.
Mas'ala 97: Ikiwa
mukallaf atafahamu ya kuwa ametokwa na madhii na hakufahamu ya kuwa madhii hayo
yalifuatana na chembe chembve za mkojo au hapana atajengea kuwa ni twahara
hata kama hakufanya istibraa, isipokuwa ikithibiti kuwa ni umajimaji unao tiliwa
shaka, na shaka yenyewe iwe katika hali ifuatayo ya kuwa umaji maji huu
uliodhihiri je yote ni madhii au ni mchanganyiko kati ya madhii na
mkojo.
KITABU TWAHARA (MLANGO WA TWAHARA)
KATIKA
MLANGO HUU KUNA SEHEMU TOFAUTI
SEHEMU YA KWANZA
MGAWANYIKO WA MAJI NA HUKUMU ZAKE
NA KATIKA SEHEMU HII KUNA VIFUNGU KADHAA
KIFUNGU CHA KWANZA
MAJI YAMEGAWANYIKA SEHEMU MBILI
SEHEMU YA KWANZA:
Maji Mutlaq,
hiki ni kitu chenye kutiririka na ambacho huitwa kwa jina la (Maji) bila
kuongeza kitu, kama maji yaliyopo kwenye kisima au mto au bahari. Na tusemapo
maji ya bahari au maji ya mto au maji ya kisima husema hivyo kwa ajili ya
kuyapambanua, si kwa sababu ya kusahihisha matumizi.
SEHEMU YA PILI:
Maji mudhaaf,
ni kitu chenye kutiririka ambacho haifai kuitwa kwa jina la (maji) pekee,
bali huongezewa neno lingine kama ifuatavyo: Maji ya komamanga kwa mfano, au
maji ya waridi kwa kutaja jina lililo dhifiwa kwenye tamko maji. Na pengine
huitwa (Maji) kwa majazi, kwa sababu hii inafaa kuto tumia neno maji kwenye neno
hilo.
KIFUNGU CHA
PILI:
MAJI MUTLAQ
(Maji halisi) NA HUKUMU ZAKE
Maji mutlaq
yamegawanyika sehemu zifuatazo: 1-Maji yenye kutiririka. 2- Maji ya
chemchem yasiyo tiririka. 3- Maji ya kisima. 4- Maji ya mvua. 5- Maji ya
kuri moja 6- Maji kidogo (yasiyo fikia kiwango cha kuri moja).
Mas'alal 36: Maji
mutlaq na mgawanyiko wake wote kama hayakuingiwa na najisi ni twahara na ni
yenye kutwahirisha hadathi na khabathi.
Mas'ala 37:Maji
mutlaq na mgawanyiko wake wote hata maji yenye kutiririka ikiwa
yatabadilika na kugeuka moja ya sifa zake tatu kwa kuingiwa na najisi
hunajisika, Na sifa hizo ni rangi ladha na harufu. Na maji kidogo
yananajisika tu kwa kuingiwa na najisi.
Mas'ala 38: Ikiwa
maji yatabadilika na ubadilikaji huo haukuwa ni katika moja kati ya sifa
zake tatu, rangi ladha na harufu, kama yakibadilika uzito wake na mfano wa
hayo, maji hayo hayata najisika ikiwa hayakubadilika na kuwa maji
mudhaafu.
Mas'ala 39: Ikiwa
rangi ya maji itabadilika au ladha yake au harufu yake kwa kukaribiana na
najisi, kama mzoga ukiangukia karibu na maji hayo na mzoga huo ukawa
ukingoni mwa maji hayo hayatanajisika vile vile.
Mas'ala 40: Ikiwa
maji hayakubadilika kwa najisi maji hayo si najisi, kama yakibadilika kwa
kitu kilicho najisika, kama ikiwa yatabadilika na kuwa ya njano au mekundu
kwa kuingiwa na juisi iliyo najisika.
Mas'ala 41: maji
hayanajisiki tu kwa kuingiwa na najisi au kubadilika kwa kuingiwa na najisi
yenyewe, bali ikiwa yataingiwa na kitu chenye najisi au kilicho beba
sehemu na chembe chembe za najisi, au kitu hicho kina chembe chembe za najisi na
maji yale yakabadilika na kugeuka kwa najisi ile, maji hayo yatanajisika
pia.
Mas'ala 42: Inatosha
kunajisika kwa maji kubadilika kwake kwa sababu ya kuingiwa na najisi hata kama
hayakubadilika sifa zake zote, kwa mfano lau kama maji hayo yatabadilika
rangi yake na kuwa rangi ya njano au nyekundu kwa kuingiwa na damu, au yakawa na
harufu iliyo kinyume na harufu ya mkojo na haja kubwa kwa kuangukia najisi hizo
kwenye maji hayo, maji hayo yatakuwa yamenajisika pia.
KIFUNGU CHA TATU
MAJI YENYE KUTIRIRIKA NA HUKUMU ZAKE
Haya ni maji yenye
kutiririka na yaliyo ungana na mada ya ardhini au nyingineyo hata kama hayatoki
na kuchimbuka ardhini.
Mas'ala 43: Maaul
jaariy (maji yenye kutiririka) sawa yawe ni kiasi cha kuri moja au yawe ni kiasi
kidogo kuliko kuri, na sawa utiririkaji wake uwe ni wa kuchupa au kunyunyiza,.
hayanajisiki kwa kuingiwa na najisi kama hayajabadilika sifa zake.
Na huambatanishwa na
maji yenye kutiririka katika hukumu ya kuto najisika kwa kuingiwa na najisi bila
kubadilika, maji yote yachimbukayo ardhini hata kama hayatiririki.
Mas'ala 44: Ikiwa
maji yenye kutiririka juu ya ardhi bila ya kuwa na asili ichimbukayo ardhini
au yenye kunyunyiza, ikiwa majio hayo yatakuwa ni machache zaidi kuliko
kuri ya maji, hakika maji hayo hunajisika kwa kuingiwa tu na najisi.
Ama ikiwa mukallaf
atatia shaka ya kuwa maji hayo yana chimbuko (mada) au laa kauli yenye
nguvu inasema kuwa hayata najisika maji hayo kwa kuingiwa au kukutana na
najisi ikiwa hapo kabla hayakutanguliwa na hali ya kuto kuwa na mada.
Mas'ala 45:
Kizingatiwacho katika kuto najisika maji yatiririkayo ni kuungana kwake na mada
(asili kama chemchem au kuungana na bomba), kwa mfano lau kama mada au asili ya
kutiririka kwa maji hayo iko juu, na mada yenye kutiririsha au
kunyunyiza maji hayo itakuwa ni chini ya kuri moja maji hayo yatanajisika,
ndio ikiwa sehemu inayo nyunyiza au asili ya maji hayo itagusana na najisi maji
hayo hayatanajisika.
Mas'ala 46: Maji
yaliyo tuwama na yaliyo ungana na maji yenye kutiririka hukumu yake ni sawa na
maji yenye kutiririka katika hukumu ya kuto najisika kwake kwa kugusana au
kuingiwa na najisi au kitu kilicho najisika, kwa mfano hodhi lililo ungana na
mto kwa ajili ya umwagiliaji, maji yake hayanajisiki kwa kugusana na najisi,
vile vile kingo za mto hata kama maji yake yametuwama na
hayatiririki.
Mas'ala 57: Ikiwa
baadhi ya sehemu ya maji yenye kutiririka itabadilika na sehemu nyingine
isibadilike, sehemu ya maji hayo iliyo ungana na mada hainajisiki kwa
kuungana au kuingiwa na najisi hata kama maji yake ni machache, na upande
mwingine hukumu yake ni sawa na hukumu ya maji yaliyo tuwama ikiwa maji ya
sehemu hiyo yatabadilika, laa sivyo yatahesabiwa yamenajisika kiwango kilicho
badilika pekee, kwa kuungana yale mengine na mada.
KIFUNGU CHA NNE
MAJI YALIYO TUWAMA NA HUKUMU ZAKE
Mas'ala 48: Maji
yaliyo tuwama bila kuungana na mada ikiwa kiwango chake hakifikii kuri moja
hakika maji hayo yananajisika kwa kuingiwa na najisi, tofauti na ikiwa yanafikia
kuri moja, hakika yakiwa ni kuri moja hayanajisiki kwa kuingiwa au
kukutana na najisi isipokuwa yatakapo badilika moja kati ya sifa zake
tatu.
Mas'ala 49: Kiwango
cha kuri kwa uzito ni sawa na huqqa ya istambuli 280, ama ukubwa wake ni sawa na
shibiri 34 kasoro moja ya tatu, na kwa lita ni sawa na lita 377
takriiban.
Mas'ala 50: Maji
yakiwa ni chini ya kuri moja hata kama ni kwa kiasi kichache hukumu yake ni sawa
na hukumu ya ya maji kidogo.
Mas'ala 51:Ikiwa
najisi itaangukia kwenye kuri na haikujulikana ya kuwa imeangukia humo kabla ya
kufika kuri au baada ya kukamilika kuri, maji hayo yatahukumiwa kuwa ni twahara,
isipokuwa ikiwa itafahamika tarehe ya kuangukia kwake humo na tarehe ya kufikia
kwake kuri haikujulikana.
Mas'ala 52:
Ikiwa imefikia kuri lakini haikujulikana ya kuwa ni maji mutlaq (ni maji halisi)
au mudhaaf, na yakaingiwa na najisi, maji hayo hayata hukumiwa kuwa ni
najisi, isipokuwa itakapo kuwa hali yake ya mwanzo ilikuwa ni mudhaaf na
kukawa na shaka ya kuwa bado ni mudhafu.
Na ikiwa
kunakuri mbili moja ni mutlaq na nyingine ni mudhaaf, na ikafahamika kuingiwa na
najisi moja kati ya kuri hizo mbili lakini haijulikani kuwa ni ipi kati ya
kuri hizo, zote mbili zitahukumiwa kuwa ni twahara pia.
KIFUNGU CHA TANO
MAJI YA MVUA NA HUKUMU ZAKE
Mas'ala 53:
Hukumu ya maji ya mvua wakati ikinyesha ni sawa na hukumu ya maji yenye
kutiririka, hayata najisika kwa kugusana na najisi ikiwa hayajabadilika moja
kati ya sifa zake, hata kama mvua hiyo ni kidogo, sawa maji hayo
yatiririke kwenye mifereji au juu ya ardhi au laa, la muhimu ni kuthibiti kuwa
ni maji ya mvua, na ikiwa yatakusanyika sehemu moja na kikaoshewa ndani
yake kitu kilicho najisika kitu hicho kitatwahirika hata kama maji yale
yatakuwa ni madogo.
Haya yote ni wakati
mvua ikiendelea kunyesha, na ikiwa mvua itakatika na kuacha kunyesha
hukumu yake ni sawa na hukumu ya maji yaliyo tuwama.
Mas'ala 54: Nguo
iliyo najisika na zulia lililo najisika ikiwa vitu viwili hivi
vitanyeshewa na mvua na maji kuingia ndani ya vitu hivyo basi vitu hivyo
vyote vitatwahirika, na haihitaji kukamua au kuosha kwa mara kadhaa, na
ikiwa maji yatafika kwenye baadhi ya sehemu na hayakuenea sehemu zote
itatwahirika sehemu zilizo fikiwa na mvua hiyo na si vinginevyo. Na hukumu
hii inahusika tu ikiwa hakuna najisi yenyewe kwenye vitu hivyo, laa sivyo
havitwahiriki isipokuwa vitakapo nyeshewa tena baada ya kuondoka najisi yenyewe
kwenye vitu hivyo.
Mas'ala 55: Ardhi
iliyo najisika hutwahirika kwa kunyeshewa na mvua kwa sharti kwamba mvua hiyo
iinyeshee moja kwa moja kutoka mawinguni hata kama ni kwa kupeperushwa na
upepo, ama ikiwa mvua hiyo itanyeshea juu ya kitu kingine – kama ambavyo
maji hayo yatatiririkia juu ya ardhi baada ya kuangukia mahali pengine na
kuingiwa na najisi- katika hali kama hii haita twahirika.
Ndio ikiwa mvua
hiyo itanyesha juu ya ardhi kisha maji yake yakatiririkia juu ya paa basi sehemu
hiyo itatwahirika.
Mas'ala 56: Ikiwa
maji ya mvua yataangukia kwenye najisi yenyewe kisha yakadondokea kwenye kitu
kingine, kitu hicho hakita najisika ikiwa maji hayo hayakuwa na chembe chembe za
najisi ndani yake na hayakubadilika kwa najisi.
Mas'ala 57: Mchanga
ulio najisika hutwahirika kwa kunyeshewa na mvua ikiwa mvua hiyo itaingia hadi
ndani ya mchanga huo na kubadilika kuwa udongo.
Mas'ala 58: Jamvi
lililo najisika linatwahirika kwa kunyeshewa na mvua, vilevile zulia lililo
tandikwa juu ya ardhi, na ardhi iliyopo chini ya zulia hilo ikiwa ni najisi
hutwahirika ikifikiwa na maji ya mvua. Ndio ikiwa jamvi au zulia havikuwa
juu ya ardhi au kukawa na utengano, hapo kuna ishkaali katika hukumu ya
kutwahirika kwake kwa kunyeshewa na mvua, kwanza kwa kunyeshea mvua juu ya jamvi
au zulia kisha maji hayo yakadondokea juu ya ardhi.
Mas'ala 59: Chombo
ambaacho nbi najisi kinatwahirika ikiwa maji ya mvua yatafika sehemu zote
zenye najisi katika chombo hicho isipokuwa ikiwa kimenajisika kwa kuliwa na mbwa
ndani yake, katika hali kama hiyo kutwahirika chombo hicho kwa kunyeshewa na
mvua tu bila ya kukisugua au kukiosha kwa mchanga kuna ishkaali, lakini ikiwa
kitanyeshewe na mvua baada ya kukisugua au kukiosha kwa mchanga wakati huo
kitatwahirika bila ya kuhitajia kuosha mara kadhaa.
KIFUNGU CHA SITA
MAJI YA BAFUNI NA HUKUMU YAKE
Mas'ala 60: Maji ya
bafuni ni sawa na maji yenye kutiririka kwa sharti kuwa yawe yameungana na mada,
kwa mfano maji yaliyoko kwenye mahodhi madogo ikiwa yataungana na mada
hayanajisiki kwa kuingiwa na najisi ikiwa maji yaliyoko kwenye hodhi pekee au
kwa kuyaunganisha na yaliyomo kwewnye mada yanafikia kuri.
Mas'ala 61:Ikiwa maji
yaliyomo kwenye mahodhi madogo yatanajisika yanatwahirika kwa kuungana na mada
kwa sharti kwamba maji ya mada yawe ni kuri na yachanganyike pia.
KIFUNGU CHA SABA
MAJI YA KISIMA NA HUKUMU ZAKE
Mas'ala 62: Hukumu ya
maji ya kisima yenye kuchimbuka ardhini ni sawa na hukumu ya maji yenye
kutiririka katika hukumu ya kuto najisika isipokuwa kwa kubadilika moja kati ya
sifa zake, sawa yawe ni kiasi cha kuri moja au chini ya hapo, na ikiwa
yatabadilika kisha ubadilikaji huo ukaondoka na kutoweka wenyewe maji hayo
yatatwahirika kwa sababu yana mada na yamechanganyika na maji yatokayo kwenye
mada kama chemchem. Ama yakiwa hayana mada yenye kuchimbuka basi itazingatiwa
kiasi cha kuri katika hali ya kutonajisika kwake hata kama kitaitwa
kisima, kama mfano wa visima ambavyo hukusanyika ndani yake maji yasiyo
chimbuka ardhini.
Mas'ala 63:
Maji najisi yaliyo tuwama sawa maji hayo yawe ni kuri au
kidogo yanatwahirika kwa kuungana na maji ya kuri yaliyo twahara au kwa
kuungana na maji yenye kutiririka au maji yenye kuchimbuka ardhini hata kama
hayatiririki na kuchanganyika na maji hayo, na pia hutwahirika kwa kukutana na
kuchanganyika na maji ya mvua, na kauli ya ahwat ni kuwa kutazingatiwa
kuchanganyika kwa maji hayo.
Mas'ala 64: Birika
lililo jazwa maji yaliyo najisika ikiwa litazamishwa kwenye hodhi
hutwahirika baada ya kuchanganyika maji hayo, na si wajibu kuyamwaga maji yake
na kuliosha birika hilo.
KIFUNGU CHA NANE
MAJI YALIYO TUMIKA YAKIWA NI MACHACHE
Mas'ala 65: Maji
yaliyo tumika kutawadhia ni twahara na yanatwahirisha hadathi na khabathi,
vile vile maji yaliyo tumika katika ghusli ya sunna, ama maji yaliyo tumika
katika ghusli ya hadathi kubwa pamoja na kuwa mwili hutwahirika hakuna ishkaali
katika utwahara wa maji hayo na juu uwezekano wa kuyatumia kuondolea
khabathi, na kauli yenye nguvu zaidi ni kuwa inajuzu kuyatumia kuondolea hadathi
pia japokuwa kauli ya ahwati ni kuwa nivema kujiepusha na maji hayo.
Ama maji yaliyo
tumika kuondoa khabathi tofauti na maji yaliyo tumika kustanji haijuzu kuyatumia
katika udhu na ghusli, na kauli yenye nguvu zaidi ni kuwa maji yatumikayo
kuondolea najisi yenyewe ni najisi, bali hata maji yaliyo tumiwa kuoshea yasiyo
ondoa najisi, ama maji ya kustanjia hukumu yake itafuatia.
Mas'ala 66: Hakuna
ishkaali katika matone ambayo hudondokea kwenye chombo wakati wa kuosha hatakama
tutasema ya kuwa haijuzu kutumia maji yaliyo oshewa hadathi kubwa. Na maji
yanayo bakia kwenye nguo baada ya kukamuliwa nguo hiyo ni twahara, ikiwa maji
hayo yatatoka baada ya nguo hiyo kukamuliwa hayata ambatanishwa na hukumu ya
maji yaliyo oshewa.
Na mkono
hutwahirika kwa kufuata kitu kinacho twahirishwa baada ya kukitwahirisha kitu
hicho, kwa hivyo hakuna haja ya kuiosha mikono hiyo, pia chombo ambacho hutumika
kuoshea nguo na mfano wa hivyo.
KIFUNGU CHA TISA
HUKUMU YA MAJI YENYE KUTILIWA SHAKA
Mas'ala 67: Maji
ambayo hutiliwa shaka ya kuwa ni najisi au twahara maji hayo ni twahara ikiwa
haikujulikana ya kuwa hapo kabla yalikuwa ni najisi, ama maji ambayo hutiliwa
shaka ya kuwa ni mutlaq au hapana hayahukumiwi maji hayo kuwa ni mutlaq
isipokuwa ikiwa hapo kabla yalikuwa ni mutlaq.
Ndio, ikiwa maji hayo
ni kuri moja na yakaingiwa na najisi hayatahukumiwa kuwa ni najisi isipokuwa
ikiwa hapo kabla yalikuwa ni maji mudhaaf, ama maji ambayo yanatiliwa shaka ya
kuwa ni mubaha au hapana (maji halali) maji hayo hukumu yake ni kuwa ni mubaha,
aisipokuwa ikiwa hapo kabla yalikuwa ni milki ya mtu mwingine au yalikuwa katika
milki ya mtu mwingine ambae kuna ihtimali kuwa ni maji yake.
Mas'ala 68: Ikiwa
mukallaf atafahamu kwa sura ya ujumla ya kuwa mojawapo kati ya vyombo
viwili ni najisi na kingine ni twahara haitajuzu kutumia chombo moja wapo
kuondolea khabathi au hadathi.
Mas'ala 69: Chombo
kinacho shukiwa kuwa sehemu moja wapo ya chombo hicho imenajisika hakita
hukumiwa kuwa ni najisi isipokuwa hali ya sehemu hiyo ya hapo kabla
itajulikana kuwa ilikuwa ni najisi, lakini kauli ya ahwat inasema kuwa ni bora
kujiepusha na utumiaji wa chombo hicho.
Mas'ala 70: Ikiwa
maji mutlaq yatafanana na mudhaaf itajuzu kuyatumia maji hayo kuondolea khabathi
kwa kutumia moja wapo kati ya maji hayo na kuoshea kwa kutumia maji mengine,
vile vile katika kuondoa hadathi.
Mas'ala 71: Ikiwa
itafahamika kwa sura ya ujumla ya kuwa maji haya ima ni najisi au
ni mudhaaf inajuzu
kuyanywa maji hayo, lakini haijuzu kuyatumia kutawadhia, vile vile ikiwa
itajulikana ya kuwa ima maji hayo ni mudhaaf au ni maghsuub (ya kunyang'anya).
Ama ikiwa
itajulkikana ya kuwa maji hayo ni najisi au ni ya kunyang'anya haitajuzu
kuyanywa, kama ambavyo haitajuzu kuyatumia kutawadhia.
Mas'ala 72: Ikiwa
sehemu au pande zitiliwazo shaka au zenye shubha hazijulikani kidhati, katika
hali kama hii inajuzu kuyatumia maji hayo bila kipingamizi.
KIFUNGU CHA KUMI
HUKUMU ZA MAJI MUDHAAF
Mmas'ala 73: Maji
mudhaaf, kama maji ya uwa waridi ni twahara ikiwa hayakuingiwa na najisi, lakini
maji hayo si yenye kutwahirisha hadathi, vilevile si yenye kutwahirisha
khabathi hata katika hali ya dharura.
Mas'ala 74: Maji
mudhaaf yana najisika kwa kuingiwa tu na najisi sawa yawe mengi au kidogo,
isipokuwa yakiwa ni yenye kuchupa kwa nguvu juu ya najisi, hata kama
yanatoka chini kwenda juu kama maji yatokayo kwenye bomba lenye
kunyunyizia na mfano wa hiyo, katika hali kama hii itahukumiwa kuwa ni
najisi sehemu ile tu iliyo gusana na najisi, na haivuki na kuelekea
juu.
Mas'ala 75: Ikiwa
maji mudhaaf yatanajisika hayatatwahirika isipokuwa kwa kuyaweka kwenye
kuri au kwenye maji yenye kutiririka na kutoweka hali ya kuwa kwake maji
mudhafu. Na kutwahirika kwa maji mudhaaf yaliyo najisi kwa
kuyachemsha ( au kuongeza kiwango cha maji hayo) kuna ishkaali.
KIFUNGU CHA
KUMI NA MOJA
MABAKI YA
CHAKULA
Mas'ala 76: Mabaki ya
chakula yote ni twahara isipokuwa mabaki ya mnyama alie najisi (najisul aini)
kama mbwa Nguruwe na mushrik (kafir) , hakika mabaki yao ni najisi.
Mas'ala 77:
Nimakuruhu kula mabaki ya mnyama asie liwa isipokuwa mabaki ya Muumini na paka
kutokana na kauli ya baadhi ya mujtahidiin.
SEHEMU YA PILI: HUKUMU ZA CHOONI
PIA KUNA VIFUNGU KADHAA
KIFUNGU CHA KWANZA
HUKUMU ZA KWENDA CHOONI
Mas'ala 78: Ni wajibu
wakatio mtu anapokwenda chooni au katika hali ya kujisaidia haja kubwa bali hata
katika hali nyingine tofauti kusitiri uchi (sehemu za siri) – nazo ni sehemu ya
mbele na nyuma na peke mbili- kwa muonaji mwenye kuheshimiwa, isipokuwa mtoto na
mwenda wazimu wasio weza kupambanua, na mke na mume na alie milikiwa kwa mmiliki
wake na alie halalishwa kwa alie halalishiwa, hakika kwa watu hawa inajuzu kwa
kila mmoja wao kuangalia uchi wa mwenziwe.
Mas'ala 79: Hakuna
tofauti katika uharamu wa kuangali kati ya uchi wa Muislaam au kafiri
kutokana na kauli ya ahwat.
Mas'ala 80: Si wajibu
kusitiri mapaja mawili wala matako wala nywele ziotazo pembezoni mwa sehemu za
siri (mavuzi). Ndio, ni sunna kusitiri sehemu zilizoko kati ya kitovu na
magoti.
Mas'ala 81: Haijuzu
kuangalia uchi wa mtu mwingine kwa kutumia kioo na mfano wa hicho, wala kwa
kutumia kioo cha kujitizamia na wala haijuzu kuangalia kwa kutumia maji
yaliyo safi.
Mas'ala 82: Ikiwa mtu
itamlazimu kuangalia uchi wa mtu mwingine kama katika hali ya kumtibu mgonjwa,
kauli ya ahwat ni kuwa ataangalia kupitia kioo kilicho wekwa mbele yake ikiwa
kufanya hivyo kutatosheleza na kuondoa dharura hiyo, laa sivyo hakuna
tatizo kuangalia.
Mas'ala 83: Ni haramu
kwa mwenye kujisaidia haja kubwa – wakati wa kujisaidia- kuelekea Qibla na
kukipa mgongo Qibla kwa kuielekeza sehemu ya mbele ya mwili wake kwenye
Qibla hata kama uchi wake atauelekeza sehemu au upande mwingine tofauti na
sehemu hizo mbili, na kauli ya ahwat ni kuwa ataacha kukielekezea
uchi wake pekee hata kama sehemu za mbele za mwili wake zitaelekea sehemu
hizo mbili, na makusudio ya sehemu za mbele za mwili ni kifua tumbo na magoti
mawili, na ikiwa italazimika kufanya moja wapo atakuwa na hiari japokuwa kauli
ya ahwat ni kuwa atakipa mgongo, na akiwa itamlazimu kufanya kitendo kimoja
wapo kati ya mambo mawili hayo na kuto jisitiri pamoja na kuwepo
muangaliaji mwenye kuheshimiwa itawajibika kwake kujisitiri.
Mas'ala 84: Kauli
yenye nguvu ni kuwa si haramu kukielekea au kukipa mgongo kibla katika hali ya
kufanya istibraa na katika hali ya kustanji japo kuwa kutofanya hivyo ni ahwat
(bora zaidi). Ndio ikiwa atafahamu ya kuwa mkojo utatoka kwa kufanya
istibraa kauli ya ahwat ni kuwa itawajibika kuacha kukielekea au kukipa mgongo
Qibla.
Mas'ala 85: Lau kama
mukallaf atapatwa na shubha katika kukipambanua Qibla hukumu ya kutumia dhanna
haiko mbali pamoja na kuto kuwepo uwezekano wa kukitafuta na kufanya uchunguzi
wa sehemu ya Qibla, na ikiwa kuichelewesha sala kutamsababishia
matatizo.
Mas'ala 86: Ni haramu
kujisaidia haja kubwa kwenye milki ya mtu mwingine isipokuwa kwa idhini yake,
vile vile ni haramu kujisaidia kwenye makaburi ya waumini ikiwa kufanya hivyo ni
kuvunja heshima yao.
Mas'ala 87: Ni haramu
kujisaidia haja kubwa kwenye mashule na mfano wa hayo ikiwa haikufahamika kuwa
sehemu hizo zimewekwa waqfu kwa ajili ya watu wote, na inatosha idhini ya
msimamizi wa waqfu hizo, na kauli iliyo dhahiri ni kutosheka na ada ya
watu ikiwa kufanya kwao kutakupa matumaini ya kuwa ni sehemu ya matumizi
ya watu wote, vile vile hali ni hiyo hiyo kwenye matumizi mengine ya vitu hivyo
vya waqfu.
KIFUNGU CHA
PILI
KUSTANJI
Ni wajibu kuosha
sehemu ya kutokea mkojo kwa maji, na inatosha kuosha mara moja japo kuwa kauli
ya ahwat ya sunna ni kuosha mara kadhaa, na haitoshelezi kitu kingine tofauti na
maji, na sehemu ya haja kubwa ikiwa haja itavuka mahali pake na kutapakaa hapo
italazimika kutumia maji pekee kama najisi nyingine, na ikiwa hakikuvuka mahali
pake mukallaf anahiari ya kuosha kwa maji hadi kusafike mahali hapo, na kati ya
kupangusa kwa kutumia mawe au kitambaa au mfano wa hivyo kati ya vitu
vyenye kuondoa najisi, na maji ni bora zaidi, na kutumia vyote ndio
ukamilifu wa twahara.
Mas'ala 88: Je
kupangusa kwa mawe na mfano wa hilo inasababisha kutwahirika mahala hapo au
kusamehewa kwenye sala pekee? Katika kupangusa kuna ishkaali, na kauli ya ahwti
ni ya pili ( yaani ni sababu ya kusamehewa kwenye sala)
Mas'ala 89: Katika
kupangusa huzingatiwa kutumia mawe matatu au mfano wa hayo, au kutumia pande
tatu za jiwe moja na mfano wa hilo japo kuwa kuna uwezekano wa kusafika kwa
kutumia chini ya mawe matatu, na kama hapakusafika mahala hapo kwa mawe matatu
ataongeza mpaka pasafike mahali hapo.
Mas'ala 90: Ni wajibu
mawe yatumikayo au mfano wake yawe twahara.
Mas'ala 91: Ni haramu
kustanji kwa kutumia vitu vyenye kuheshimiwa, vile vile ni haramu kutumia mifupa
na kinyesi. Na lau kama mtu atastanji kwa kutumia vitu hivyo atazingatiwa
kuwa ameasi, na kutwahirika au kusameheka kwa kutumia vitu hivyo kuna
ishkaal.
Mas;ala 92: Ni wajibu
katika hali ya kuosha kwa maji kuondoa najisi yenyewe na athari zake kwa
maana kuwa kuondoa chembe chembe ndogo ambazo hazionekani na kwa kawaida
haziondoki isipokuwa kwa kutumia maji, na si wajibu kuondoa rangi na harufu, na
inatosha katika upangusaji kuondoa najisi yenyewe, na si wajibu kuondoa
athari za najisi, na ikiwa haja kubwa itatoka ikiwa na najisi nyingine isiyo
kuwa hiyo kama damu au mahali pa haja kubwa pakagusana na najisi nyingine kutoka
nje haitatosheleza kuitwahirisha sehemu hiyo ispokuwa kwa kutumia maji, na
lau kama atatia shaka ya kuwa imetwahirika sehemu hiyo au laa atajengea ya kuwa
haikutwahirika na hapa atakuwa na hiayari kati ya kutumia maji mawe na
mfano wa vitu viwili hivyo.
KIFUNGU CHA TATU
ADABU ZA KWENDA CHOONI
Ni sunna kwa mwenye
kujisaidia haja kubwa kujitenga na watu au kwenda sehemu ya mbali ambayo
hatoweza kuonekana, na katika haja ndogo atafute sehemu yenye muinuko, kama
ambavyo ni sunna kwake kufunika kichwa na kufunga kitambaa shingoni, na kufunika
kicha na nyingo kwa kilemba au kitambaa kunatosheleza kufunika kichwa, na
ni sunna kutanguliza mguu wa kulia wakati wa kutoka, na kufanya istibraa, na
kujitegemeza kwenye mguu wake wa kushoto – wkati wa kukaa- na kupanua mguu
wa kulia, na ni makruuhu kujisaidia barabarani, njiani, chini yamiti ya
matunda, na sehemu za kulaaniwa, kama kwenye milango ya majumba na mfano wa
sehemu hizo kati ya sehemu ambazo mwenye kujisaidia sehemu hizo anakuwa
amejisababishia watu kumlaani, na sehemu zilizo andaliwa kwa ajili ya vituo vya
misafara, na kulielekea jua au mwezi kwa utupu wake, na kula na kunywa katika
hali ya kujisaidia, na mengineyo kati ya mambo yaliyo tajwa na maulamaa radhi za
mwenyezi mungu ziwe juu yao, japo kuthibiti kwa baadhi ya mambo yaliyo tajwa
kuwa ni ya sunna au makruuhu kuna ishkaali.
Mas'ala 93: Maji ya
kustanjia ni twahara hata kama yamestanjiwa sehemu ya kutokea mkojo ikiwa
yatatimia masharti haya yafuatayo:
1- Kuto badilika rangi,
ladha na harufu ya maji hayo kwa najisi.
2- Kuto ingiwa na najisi
nyingine kutoka nje tofauti na mkojo.
3- Kuto vuka najisi
itokayo kwenye sehemu yake ya kawaida.
4- Haja kubwa na ndogo
isitoke pamoja na najisi nyingine kama damu, isipokuwa ikiwa itatoka
lakini si yenye kuonekana katika hali hiyo hakuna tatizo.
5- Kusiwe na chembe
chembe za haja kubwa zenye kuonekana kwa kauli ya ahwat.
Kwa kukamilika
masharti haya maji ya kustanjia yanakuwa ni twahara na yanaweza kutumika
kuondolea khabathi, lakini haijuzu kuyatumia kuondolea hadathi wala
kuyatumia kwenye udhu wa sunna na ghusli ya sunna.
KIFUNGU CHA
NNE
ISTIBRAA

|