MUKHTASARI WA MAISHA YA KIONGOZI WA JUU WA KIDINI AYATULLAHIL UDHMAA SHEIKH MOHAMMAD FAADHIL LANKARANI (MUNGU AMJAALIE UHAI MREFU).
بسم الله الرحمن الرحيم
الذ ين يبلغون رسالات الله ويخشونه ولا يخشون
أحدا إلا الله وكفي بالله حسيبا
Tunamshukuru Mwenyeezi Mungu ambae amemuumba mwanaadamu na
akamfundisha kubainisha, na shukurani ni za Mwenyeezi Mungu ambae alifundisha
kwa kalamu, na mfundisha mwanadamu mambo asiyo yajua. Na rehema na amani ziwe
juu ya mbora wa viumbe vyake na hitimisho la mitume wake Mohammad na Aali zake
walio wema na watakatifu wenye kuongoza
na wenye kubarikiwa.
Nilikuwa na matamanio makubwa yalioje – yakuwa
na mimi nipewa jukumu la kuandika kuhusiana na maisha ya mwanazuoni kati ya
wanazuoni wa kiislaam, na marjiu[1] mtukufu kati ya marajiu wa madhehebu ya
kishia , na kuhusiana na mwalimu mkubwa
kati ya walimu wa Hawza (shule) ya kielimu ilioko mji mtukufu wa Qum- basi tusitosheke katika
kuyazungumzia maisha ya kundi fulani la
maulamaa wetu na wanafiqhi wetu katika kuelezea juu ya maisha yao tu na
kuwataja majina yao na nasabu (koo) zao
au kuizungumzia sehemu ya elimu yao na
athari zao, bila ya kuvuka mipaka hiyo na kuzungumzia yanayohusiana na maisha
yao kiimani na juhudi walizozifanya
wakiwa wakwelika katika kujijenga kiroho
na kitabia au kimaadili, na hatua zao za kielimu na mwenendo wao binafsi na
ufahamu wao wa kijamii na kisiasa.
Na
kwa hakika nimegundua ya kuwa historia za wengi wao- radhi za Mwenyezi Mungu
ziwe juu yao- zilikuwa zimejawa na mazingatio mengi na faida nyingi, na zikiwa
zimejitosheleza kutokana na athari walizoziacha, zikiwemo sifa njema na mambo
mengi ya fakhari waliyo yaacha,
na
juhudi kubwa walizo zitoa na ushupavu mkubwa waliouonyesha na misimamo ya
kishujaa waliyokuwa nayo, na kujitolea muhanga waliko kufanya katika njia yenye miba mikali na huku wakikwaruzana na
mashetani wa zama zao, na wakisimama
kidete kwenye rai zao, wakipigana jihadi kupinga upotovu wa aina yoyote ndani
jamii yao, wakiamini ya kuwa maisha ni Itikadi na jihadi, laa sivyo ni
udhalili na aibu duniani na udhalili katika Akherah, kwa hivyo basi hakika
maisha yao yanafaa kuwa ni masomo yenye kutoa faida na kutunufaisha sisi na
yawe ni Ardhi safi kwa kilimo na utoaji wa mavuno mengi.
Kwa
hiyo basi ikiwa tutawazungumzia maulamaa wetu kwa mtizamo kama huo , basi
kuyaelezea maisha yao haitokuwa sawa
na kukielezea kitu kilicho kifu na
kuandika mistari tu na mukhtasari au ishara fupi za maisha yao, bali ni
jitihada ya uwekaji wazi na upekuzi wenye faida kuhusiana na matokeo ya maisha yao kwa kupekua kila kipengele, tunafanya hivyo huku tukiangalia kwa makini
sababu za kuchipuka kwao na malezi yao, malezi ambayo yameunda watu wema na
wanazuoni wenye kumuelewa Mwenyeezi
Mungu (wacha Mungu), bila ya kusahau au kughafilika na kuto zitaja sababu za
kupea kwao kielimu na kimaarifa katika majaribio yao yenye juhudi kubwa za
hatua kwa hatua za kuzifichua elimu za qur’an elimu za Qur ani pamoja na urithi wetu
mwingine, sawa uwe urithi huo ni wa
kielimu au riwaya au rijaali[2]
au historia, ukiongezea mambo ambayo zama zao zilipambika nayo na tamaduni zao ambazo zilikuwa katika
zama zao na matukio mbali mbali na fikra tofauti na athari nyingi nyengine, bali
matatizo yaliyo kuwepo ambayo yalikuwa yakihitajia misimamo ya kisheria isiyo
tetereka na yenye kuhitaji ushupavu na misimamo ya sawa.
Na hatua hii itakuwa ni yenye kusisitiza na
kutilia mkazo zaidi ikiwa tutafahamu ya kuwa
faqihi (mwanazuoni aliyebobea katika elimu ya fiqhi) anapo beba jukumu
na kuchukua cheo cha marjiu, hawi ni mufti tu aulizwae kuhusiana na hukumu za
kisheria na kujibum tu, na kumfuata yeye (kumfanyia taqliid) hakuwi ni kule tu mukallaf[3] kuchukua
risala amaliyyah (kitabu cha fatwa) na kuirejelea pindi anapo ihitajia au
kutatizwa na jambo, bali taqliid (kumfuata mwana chuoni katika hukumu za
kidini) imekuwa ikielezea mfumo mwingine uelezao namna ya kuwa sambamba na kuwa
bega kwa bega na mfumo wa marjiu (mwanachuoni aliyefikia daraja ya ijtihadi)
yule na kuufuata mwenendo wake, na kujifunga na kufuata si tu fat’wa zake bali
ni kuzifuata rai zake na misimamo yake katika nyanja zote sawa iwe ni katika
uwanja wa kiimani au kijamii.
Na
sitakuwa nimevuka mipaka ikiwa nitasema
ya kuwa: Hakika maisha ya mukallaf
yamekuwa ni yenye kuchukua sura ya sera na mfumo wa maisha ya anayemfanyia
takliid (anayemfuata) na wakati huo basi mahitajio yanakuwa ni makubwa zaidi na
ya dharura zaidi katika kuwa sambamba na maisha ya marjiu wa takliid (marjiu
anayefuatwa) ili picha ya maisha yake iweze kubainika kwa muqallid (wafuasi wake na wapenzi wake)
na kuwa rahisi kumfanya kuwa ni kigezo chema katika maisha yao ya kidini na
kijamii, na awe ni dalili na msaidizi wa kuyajenga maisha hayo kulingana na
misimamo yake na fikra zake.
Kwa
hivyo basi sisi tuko mbele ya faqihi aliyebobea katika elimu, na mwanazuoni
mkubwa kati ya wanazuoni wa fiqhi na wanazuoni wa madrasa ya Ahlul bayti wa
mtume (s.a.w.w), ambae amekuwa akinywa
na kuchukua kwenye neema ya elimu zao zilizo pana na chemchem ya maarifa
yao mpaka akafikia kiwango cha juu na kupaa kwenye anga lake la kielimu na kiroho, na hivi leo akawa
ni mwanazuoni mkubwa na mwalimu menye nafasi ya juu na marjiu mmoja wa juu wa kidini kati ya marajiu wa takliid katika
zama zetu hizi.
MAKUZI YAKE.
Baada
ya baba wa sheikh Faadhil Lankarani
(Mwenyeezi Mungu amtakase) ambae ni mwanazuoni mkubwa wa Fiqhi, kuhama kutoka
Qafqaaz, alihamia na kukaa miaka kadhaa katika mji mtukufu wa Mash’had na
katika Hawza ya kielimu ya mjini Zanjaani, kisha akuhamia kwenye mji
mtukufu wa Qum baada Ayatullahi Shekh Abdul kariim Al-haairiy – radhi
za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kusimama na kuanzisha Hawza ya kielimu yenye
baraka, ili aendelee na harakati zake za
elimu ya fiqhi kwenye mji huo na
vilevile kuendeleza harakati zake za ualimu au ufundishaji.
Basi
mnamo mwaka 1350 Hijiria Shamsia. Alizaliwa mheshimiwa shekh Mohammad Faadhil
katika mji mtukufu wa Qum katika familia
ya wanazuoni na katika nyumba moja wapo kati ya nyumba za watu wema na
wachamungu na akiwa chini ya malezi ya baba yake mtukufu, ambae alikuwa akimpa
umuhimu maalum na uangalizi wa aina yake mpaka alipo maliza masomo yake ya
elimu ya msingi, na alikuwa ni mwenye kipaji cha hali ya juu katika hatua zote
za masomo yake, na hakuwa akiwapita marafiki zake tu kimasomo katika madrasa, bali wanafunzi wote
wa mji mtukufu wa Qum.
Mhesimiwa
Shekh hakuendelea na masomo yake ya sekondari baada ya kumaliza masonmo yake ya
elimu ya msingi, bali alikuwa akiuelekeza muelekeo wake na mtazamo wake
kuielekea kwenye Hawza ya kielimu ilioko mji wa Qum, mji ambao yalifahamika
mapenzi ya mwanazuoni huyu kuuelekea mji huo na shauku yake ya kupata elimu
iliyoko kwenye mji huo, na akajiunga na Hawza ya mji huo, na kwa kufanya hivyo
basi ndiyo akawa ameianza safari yake ya kielimu, nae akiwa na umri wa miaka
kumi na tatu, na yeye katika mji huo alikuwa ni mwanafunzi mzuri wa kupigiwa
mfano na ni mwenye mipangilio madhbuti katika fikra zake, mwenye kufuatilia vyema masuala yake ya kielimu.
Mheshimiwa
Shekh alifahamika kwa udadisi wake na umakini wake na juhudi zake na kupenda
kwake masomo yake, kwa kiwango kile kile cha akili alicho kuwa akisifika nacho,
uwezo wake mkubwa na wa kiwango cha juu katika mfumo wa matendo yake ya Hawzah
na harakati zake za kifikra na ufuatiliaji wake wa mambo ya kielimu, kitu
kilicho mfanya kupea na kuwa na nafasi ya juu kuliko wengine na kuwapituka
wengine na kumaliza kwa haraka daraja zake za masomo, ingawaje daraja hizo
zilisifika kwa ugumu na matatizo makubwa, na akaweza kuzitimiza kiukamilifu na
kwa umakini mkubwa, na kukusanya nyenzo zote zihitajikazo kwenye Hawza, hali ya
kuwa ameyafahamu vyema masomo hayo ya
Hawza, na alikuwa ni mwanafunzi aliyenufaika na ni mwalimu aliye wanufaisha
wengi.
Na
alikuwa sifa ambazo alisifika nazo na kusifiwa nazo shakhsia yake na
kumpambanua na wengineo kati ya marafiki zake
walio kuwa kwenye zama zake, sawa sifa ambazo alizipata kwenye malezi
yake ya nyumbani yaliyo patikana
kutokana na juhudi kubwa za malezi ya dhati aliyopewa na mzazi wake, au aliyoyapata
katika kujizatiti kwake kwenye nafsi yake, hali akiishi kwenye mwenendo wa
masomo yake na akihudhuria kwenye masomo ya maulamaa wakubwa wa Hawzah kati ya maulamaa walio
julikana si tu kwa wingi wa elimu yao,
bali kwa malezi yao mazuri, kwa wanafunzi wao na uadabishaji mzuri wa wanafunzi
wao.
Sifa
hizi zilikuwa zikifuatana na maisha ya Shekh wetu mtukufu tangu akiwa
mwanafunzi mdogo katika Hawzah ya kielimu na akipasua na kupambana na hatua
zake zilizo kuwa ngumu kwa neema alizo mpatia Mwenyezi Mungu mtukufu za kiakili
yenye nguvu na ufahamu ulio wazi na uzingatiji wa hali ya juu, mpaka akafikia
hatua ya kukwea na kukaa kwenye kiti cha ufundishaji akizungukwa na kundi la
wanazuoni wakubwa wa Hawzah ya kielimu
na watu wenye fadhila kwenye Hawza hiyo, wakifaidika kutokana na utafiti wake
na rai zake huku wakijipamba na tabia zake na mwenendo wake.
Mheshimiwa
Shekh alifuatana katika masomo yake ya Hawzah na rafiki yake marehemu Shahiid Ayatullah al-haji sayyid Mustafa al-khomainiy, mtoto mkubwa wa mheshimiwa
imamu Khomainiy (Mwenyezi Mungu autakase utajo wake mtukufu), kwani yalikuwa
yakiwaunganisha mahusiano madhubuti
yaliyo kuwepo kati yao na urafiki mkubwa wa kidhati.
Na
walibaki kwa muda mrefu wakikumbushana
na kusoma pamoja masomo yao ya Hawzah na wakifanya
bahthi pamoja kwenye Hawzah hiyo kwa kwa miaka mingi.
Mheshimiwa
Sheikh Faadhil kuhusiana wenye baraka anasema: (Kuwepo kwa rafiki huyu mpenzi,
kulikuwa na athari kubwa na yenye nguvu, nguvu ambayo ilikuwa ikinifunga kwenye
njia ambayo niliamua kuifuata , hakika tulikuwa ni marafiki wawili wenye
kusaidiana tukikumbushana masomo yetu na kufanya bahthi pamoja kwenye masomo
hayo).
Na kwa hakika hii ilikuwa ni sababu moja wapo
ambayo ilimhamasisha mheshimiwa Sheikh kuendelea na masomo yake ya Hawzah, na
miongoni mwa saababu nyengine ni msimamo wa baba yake ambae ndiye mlezi na
msimamizi wake na ambae ndiye aliye kuwa akimtilia umuhimu wa aina ya pekee na
akimpa nafasi na umuhimu mkuwa kuliko ndugu zake wengine watatu, na hasa hima
hiyo ilizidi baada ya kugundua kuwa ni kijana mwenye uwezo na mwenye mapenzi makubwa ya masomo ya
Hawzah, kwa hiyo akazidisha ile hali ya kumfuatilia na kumlea au kumpatia
malezi maalum na kumfundisha, na yote haya yalikuwa na athari kubwa katika kuielekea kwake Hawzah na kuzidi kung’ara
katika marafiki zake na waliyo kuwa wakiishi katika zama zake.
Kama ambavyo kuna sababu mbili muhimu alizo zipata mheshimiwa Sheikh,
hakika Mwenyezi Mungu alimneemesha kwa kumpa akili yenye nguvu ya kushika na
kuwa na uvumilivu (subira) hizi ni sababu mbili ambazo huzihitajia kila
mwanafunzi anaye taka kufikia daraja ya juu ya kielimu na maarifa.
Kwa
hivyo akawa anazisoma elimu za Hawzah
kwa umakini na huku akipambana na matatizo yake na akizivuka daraja na kuingia
daraja nyingine akifanya hivyo kwa makini na kwa muda mfupi, na akawa anazipanda
ngazi za elimu kwa muda mfupi na kwa uvumilivu wa hali ya juu na kwa ufahamu wa
hali ya juu pia, jambo lililo washangaza walimu wake na marafiki zake na wenye
kumpenda.
WALIMU WAKE:
Baada
ya mheshimiwa Sheikh kukamilisha daraja mbili za Muqaddimaat na Sutuuh katika
muda wa miaka sita, akiwa ameiandaa nafsi yake kwa ajili ya daraja nyengine
nayo ni daraja ya (Bahthul khaarij) bahthi ya nje (haya ni masomo ya juu kabisa
katika barnaamiji ya Hawzah) daraja ambayo inakuwa na bahthi za juu kabisa na
akiwa na umri wa miaka kumi na tisa.Na alihudhuria bahthi za Fiqhi na Usuul kwa:
Mheshimiwa Ayatullah al-udhmaa Assayyid
Burujardiy Mwenyezi Mungu amtukuze, akawa akichota elimu yake kutoka kwenye
chemchem ya Sayyid huyu alie kuwa na kipaji cha juu kabisa cha akili na
mwalimu aliye mzuri na Marjiu mkubwa, na
akihudhuria bila ya kukosa kwenye vikao vyake
vya kielimu, akiandika mihadhara
yake ya Fiqhi na Usuul mpaka ikafikia
mihadhara ile kuwa ni mijalladi mitatu mikubwa na yenye milango mingi katika sheria za Sala.
Ama kwa hakika alikuwa ni sikio lenye kuelewa na mwanafunzi mwerevu na mdadisi na aliye kuwa akiuliza
kila alisikialo, jambo lililomstaajabisha mwalimu wake, na akapata hadhi ya
pekee kwa mwalimu wake na nafasi ya juu, nafasi ambayo hakuificha kwa
mwanafunzi wake mwalimu huyo na alimfahamisha mzazi wake bila kificho hali ya
mwanawe.
Na
hebu tuyasikilize aliyo yasema Mheshimiwa Shekh Mohammad Faadhil nae akielezea
historia ya kujiunga na masomo ya sayyid Burujardiy akijiimarisha kwa kuchukua
mfumo wa mheshimiwa Shekh sayyid na
bahthi zake za kina:
Katika
mwaka 1369 hijiria. Shamsia. Nilikuwa na umri wa miaka kumi na tisa, Mwenyezi Mungu
mtukufu alinipa tawfiiq ya kuhudhuria bahthi za mwalimu wetu Burujerdiy, na kwa
shauku kubwa na uchangamfu wa hali ya juu na kwa sababu ya nguvu ya akili
niliyo kuwa nayo nilikuwa nikiandika tukiwa katika hali ya masomo anwani za
bahthi na riwaya zake tu ili nikamilishe kuziandika usiku, na hii ndiyo ilikuwa
njia yangu katika kuandika masomo ya sayyid ustaadhi wetu.
Sayyid
ustaadhi wetu alikuwa ana sifa ya umakini na udadisi katika ibara zake na mfumo wa kina, isipokuwa ni kwamba kuingia kwake
kwenye bahthi na kutoka kwake lilikuwa ni jambo lisilo kosa ugumu wa utambuzi,
na kwa sababu hii kuandika masomo haya
lilikuwa ni jambo zito na gumu pia.
Na
vilevile Mheshimiwa sayyid alikuwa
katika masomo yake ni kama hakimu ambaye hubeba pamoja nae mafaili maalum ya
kila kesi, kwa hivyo katika kila mas’ala kati ya mas’ala ya Fiqhi akihifadhi
faili lake maalum katika kifua chake, na
faili hilo likikusanya au likiwa na riwaya mbali mbali za mas’ala hiyo na kauli
mbali mbali za maulamaa wa kisunni (Al-aamah) na kishia (Al-khaaswa) kwenye
faili hilo, na rai zao zenye kutofautiana kuhusiana na mas’ala hiyo na kuhusiana
na riwaya hiyo moja, na baadae huyabainisha mas’ala hayo yaliyo tajwa kwa uwazi
kabisa na mwisho kumalizia kwa kutoa rai yake kuhusu mas’ala hiyo.
Siku
moja mheshimiwa Sayyid alihudhuria au alikuja kwenye majlisi ya Azaa ya Ahlul
bayti (a.s) iliyo kuwa inafanyika nyumbani kwetu, na baada ya kumaliza majlisi
na watu kutawanyika kiasi kwamba hakukubakia nyumbani mtu yoyote isipokuwa
sisi, baba yangu akasema kumwambia Sayyid ustaadh: Je mnafahamu ya kuwa
mwanangu anaandika masomo na bahthi zako ambazo unazitoa katika masomo yenu nae
ni miongoni mwa watu walio pewa tawfiqi ya kuhudhuri kwenye bahthi hizo? Sayyid
ustaadhi akajibu: Hapana.
Baba
yangu akaniambia: Lete masomo uyaandikayo, na umpatie mheshimiwa Sayyi.
Nikayaleta yale niliyo kuwa nikiyaandika
na kuyaweka mbele yake. Nae akamaliza nusu saa akiyasoma,
kisha akaya tilia ish’kaali juu ya riwaya iliyo nukuliwa kwenye kitabul
-wassaila, kisha akanigeukia na akawa akinihamasisha kuendelea na kazi niliyo
kwisha anza kuifanya, na baada ya hapo
sikuchelewa katika kuyaandika masomo ya sayyid ustaadhi wetu siku anapo
fundisha.
Na
kama sikujaaliwa na kupewa
tawfiiq ya kuyaandika siku ile ile nilikuwa nikiyaandika usiku ufuatao, na
nilikuwa nikimpatia mheshimiwa kila ninacho kiandika nae alikuwa akiyasoma na
akinielekeza sehemu zenye kasoro.
Na
miongoni mwa bahthi nilizo ziandika ni bahthi ya nguo ya sala yenye kutiliwa
shaka na bahthi hii ni miongoni mwa bahthi muhimu sana katika mlango au kitabu
cha sala, na ustaadhi aliyazungumzia
mas’ala haya na kuzielezea pande zake zote za kifiqhi na Usuul, na bahthi hii
niliiandika kwa ukamilifu wake kwenye karatasi maalum peke yake bila
kuichanganya na bahthi nyengine na nilipo maliza nilimpatia mheshimiwa sayyid,
na baada ya kumaliza kuipitia akawa ananihimiza na kunitia moyo na
kunihamasisha kuendelea na kazi ya kuandika, na alinipatia kwa wakati huo tumani mia tano na kilikuwa ni kiwango
kikubwa na ni pesa nyingi katika zama hizo.
Na
nilipo maliza na kuikamilisha juzu ya kwanza nilimpatia na yeye kuisoma kisha
akaamuru ichapishwe. Na alifanya hivyo hivyo pia kwenye juzu ya pili nilipo
maliza kuiandika, na ilibakia kwake kwa muda wa wiki moja, na baada ya kumaliza
kuisoma takriban thuluthi mbili za kitabu hicho. Akaniambia: Sikukuta makosa
ndani yake na hakina tatizo lolote.
Nikamwambia:
je unaniruhusu kukichapisha? Akasema: Nenda
kakichapiche na gharama yake ni juu yangu. Na kitabu hiki kimezungumzia bahthi
za sala, na haya ni matunda ya miaka
kumi na moja ya ufundishaji wa sayyid ustadh wetu. Na mwishoni mwa umri
wake mtukufu alisomesha baadhi ya kitabu cha utoaji hukumu (Kitabul - qadhaa).
Na kwa hakika sayyid ustadhi wetu alikuwa
akikitilia umuhimu wa aina yake kitabu hiki. Na ninakumbuka ya kwamba yeye
katika majlisi moja iliyohudhuriwa na watu wawili au watatu alisema, na
kulipita mazungumzo kadhaa kuhusiana na
kitabu hiki:Akasema Sisi tunatoweka na kuihama dunia na hakuna kinacho bakia
kwetu isipokuwa kitabu ambacho kimetungwa kwa jina letu, nacho ndicho kinacho
bakiza jina letu likiwa hai.
Nyenzo za uchapishaji kwa wakati huo hazikuwa ni
nzuri, na hazikuwa kama nyenzo zipatikanazo kwenye zama zetu hizi ambazo ni
maridadi na ni nyingi, kwa hivyo nilikiandika kitabu changu hiki mara tatu,
mara ya kwanza kikiwa katika hatua ya kwanza na mara ya pili kikiwa
kimesahihishwa, na chapa ya tatu kilichapishwa kila ukurasa upande mmoja, na
kukipeleka kwa ajili ya uchapishaji.
Na kazi hii ilikuwa ni kazi nzito sana, pamoja na
kuwa ilinitaabisha sana, lakini ni kazi niliyo kuwa nikiifurahia kutokana na
kuwa ni matunda ya aina yake aliyo tupa ustadhi wetu, na kwa usaidizi wa Mwenyezi
Mungu na tawfiqi yake kimekamilika na
kumalizika uchapishaji wake.
Na mimi ninaishukuru kamati ya kielimu katika
kituo cha Fiqhul aimmatul at’haar (a.s) ambacho kimeandaa kitabu hiki kwa jili
ya chapa mpya, kwa hiyo ni huduma bora na nzuri kwa Fiqhi ya Ahlul bayti (a.s),
nina muomba Mwenyezi Mungu mtukufu awazidishie baraka katika juhudi zao hizo na
awaneemeshe kwa kuwapa tawfiq na usaidizi.
Yamemalizika mazungumzo ya Sheikh. Na mazungumzo
haya yote nimeyataja kwenye kitabu nilicho kiandika kuhusiana na maisha
ya sayyid Buruujardiy na maisha ya Shekh Faadhil mwanzoni mwa juzu ya kwanza ya
kitabu kiitwacho Nihaaayatu taqriir cha mheshimiwa Ayatulla Shekh Alfaadhil, na
nimeyanukuu hapa kutokana na ulazima ulio kuwepo na kwa ajili ya faid yake.
Ustaadhi sayyid Buruujadiy amesema kuhusiana na
mheshimiwa Shekh baada ya kuona masomo ya ustadhi wake aliyo yaandika na akiwa ameyaandika kwa lugha
safi ya kiarabu: ( Sikuwa nikidhani ya kuwa katika umri mdogo kama huu kuna mtu
anae weza kufahamu alama zilizo fichika
na mambo maalum yaliyoko kwenye masomo yetu, na kuyaandika kwa ibara za kiarabu
kizuri na chenye kufahamika).
Kama ambavyo kuna kauli nyingine ya mheshimiwa sayyid Buruujerdiy, iliyosimuliwa
na mmoja kati ya wanafunzi wake aliyekuwa akihudhuria masomo yake amsema ya
kuwa siku moja sayyid Buruujerdiy
alisema akimuashiaria Shekh Faadhil:
(Hakika huyu ni mujtahid) na kauli hii ilikuwa ni kauli iliyowastaajabisha wengi na kuwatahayarisha
wengine hasa tukiangalia katika umri wake nae akiwa ni kijana mdogo na barobaro
ambae hajavuka miaka ishirini na tano ya umri wake mtukufu.
2- Mheshimiwa Ayatullah al-udhumaa Imam Khomainiy Mwenyezi Mungu autakase utajo wake.
Baada tu ya sayyid Imam Khomainiy kuanza kutoa
bahthi zake za kielimu watu wengi kati
ya wapendao kuwepo kwake na wapendao elimu yake wakaanza kwenda mbio kuhudhuria
mlolongo wa darsa zake, wakichota na kujikusanyia kutoka kwenye elimu yake
iliyo kuwa ni nyingi na kubwa na fikra zake zilizo nyingi na rai zake zenye
kuamsha watu na vipaji vyake vya kiroho
na vya hali ya juu.
Na mheshimiwa Shekh Mohammad Fadhil ni miongoni
mwa watu wa mwanzo na wanafunzi wa mwanzo kuhudhuria kwenye masomo yake, na
akamaliza miaka saba akiwa mbele ya sayyid Imam akihudhuria darsa zake na akiwa
amehitimisha duru (round) kamili ya usuul katika bahthi za (Alfaadh) matamko na
bahthi za kiakili. Kama ambavyo alivyokuwa akihudhuria duru nyingine ya Fiqhi
aliyo kuwa akitoa sayyid imam pamoja na masomo yake ya Usuul.
Na miongoni mwa mambo Aliyo sifika nayo na kuwapita wenziwe Shekh Faadhil ni kuhudhuria
kwake kwenye masomo kusiko katika, na
alikuwa akiandika masomo yote aliyokuwa akihudhuria na alikuwa akiandika kwa
umakini mkubwa na kwa ufahamu wa hali ya juu mpaka masomo yale yakafika kuwa ni
vitabu viwili vikubwa vyenye kukusanya milango tofauti na mingi ya fiqhi.
3- Mheshimiwa Ayatullah sayyid Mohammad Hussein
Twaba twabaiy Mwenyezi Mungu autakase utajo wake.
Pamoja na kuhudhuria masomo yake ya fiqhi na
Usuull Shekh Mohammad Faadhil aliendelea
na kupokea masomo mengine, lakini mara hii alikuwa akiyachukua kutoka kwa Allaamah
na mwanazuoni mtukufu sayyid Twabatwabaiy muandishi wa Tafsirul miizan, na
alisoma kwa mheshiwa sayyid Mwenyezi Mungu autukuze utajo wake masomo ya
Tafsiri na Falsafa na Hekima, na alibahatika kusoma sehemu ya kitabu
Al-Mandhuumah cha Sabziwariy na Asfaar cha Mullah Swadraa Shiiraziy, ukiongezea
kushiriki kwake kwenye mlolongo na
bahthi zingine za Akida na Akhlaaq.
Hakika mheshimiwa Shekh Faadhil aliumaliza muda
wake mrefu wa umri wake akihama kwenye vikao vya walimu wake watukufu, ambao ni
mheshimiwa Ayatulla al-udhmaa Buruujardiy, na mheshimiwa Ayatullah al-udhmaa
Imam Khomainiy, na mheshimiwa Ayatullah Allaamah Twabatwabaiy, na kujichotea
kwenye chemchem za elimu yao iliyo kuwa ni nyingi, na wakimpa na kumwagia mambo mengi kutokana na mifumo yao ya kielimu
na kimalezi, kwa hakika ilikuwa ni mito ya salsabiil hakuwahi kuonja kinywaji kilicho kuwa safi na
chenye kukata kiu yake kuliko kinywaji hicho, mpaka kipindi hiki kilicho jawa
na faida katika maisha yake kuwa ni nguzo za kielimu na kiroho zilizopata
mahala pake kwenye nafsi yake na katika shakhsia yake, na ikaanza kuota mizizi tabia
nzuri na mifumo mizuri na sera thabiti na tabia yenye manufaa, mambo yaliyo
zisaidia hatua zake za kielimu na hata
za kijamii katika kupasua njia yake kwa kuvumilia mitihani yake, na
akifunguliwa katika kila mlango auingiao milango mingine mingi, na kila uwanda
au ukingo hujifungua na kuambatana na kingo zingine zilizo kuwa na kina kirefu
na zenye manufaa mengi.
Na hapa
mbele yetu kuna sifa za walimu wake na bahthi zao alizo ziandika, na mlolongo
wa masomo yake na bahthi zake za kielimu na vitabu vyake alivyo vitunga na
ambavyo mara nyingi akitoka nje ya rai
za walimu wake, na akawa akizihoji baadhi ya rai hizo kwa roho ya kielimu na
kwa hoja madhubuti, hakika hiyo ni dalili juu ya sifa alizokuwa akisifika nazo
mheshimiwa Sheikh kuwa ni mwenye uwezo wa aina ya pekee, na ufahamu wa masomo ulio madhubuti , na uchangamfu
wa hatua kwa hatua na hakueleweka kwa uchovu na uvivu kwani hakuwa akifahamu kulegea wala kushikwa na uvivu.
Na jambo livutialo hapa ni kuwa mheshimiwa Sheikh
kipindi ambacho alikuwa akijishughulisha na masomo yake kwa wanazuoni hawa
wakubwa na kwa wengineo katika Hawzah ya kielimu wakati huo huo alikuwa
akijishughulisha na pia kufundisha, kwa mfano alipokuwa na umri wa miaka kumi
na tano alikuwa ni mwanafunzi alie kuwa amewapita wenzake na kuwazidi kama
ambavyo kipindi hicho hicho alikuwa ni mwalimu mzuri, na hili ni jambo ambalo
ni marachache kupatikana na hupatikana kwa watu wachache tu kati ya wanazuoni
wa Hawzah na waheshimiwa wa Hawzah au as’haabul fadhiila.
Na masomo yake yalikuwa yakihudhuriwa na kiasi cha
wanafunzi thamanini wa Hawzah na walio
kuwa wakilingana naye kwa umri, mpaka harakati zake za kielimu zikaamsha na kuwazindua wengi walio kuwa wakimshuhudia, na haikomei hapo
bali darsa zake zilikuwa zikihudhuriwa na kundi kubwa la watu wazima walio
wakubwa kiumri kuliko kijana huyu mwenye elimu na fat’wa zake na ufahamu wake
ulio mpana na uwezo wake wa kufundisha wa kisasa na wa aina ya pekee na ulio
bora.
Na alipofikia umri wa miaka kumi na tisa darsa
zake zikapanuka zaidi na wahudhuriaji wa darsa hizo kuvuka mamia ya wanafunzi.
Na mheshimiwa baadae akaendelea na
ufundishaji wa kitabu Kifayatul Usuul
cha Muhaqiqi al-khorasaaniy na hicho ni kitabu cha mwisho kisomeshwacho kwenye daraja
ya Sutuuh na kilicho kigumu katika daraja
hiyo. Na kwa hakika alifundisha kitabu hiki na kukikamilisha mara sita kama ambavyo alifundisha kitabu
Al-makaasib pia cha Al-muhaqiq Al-answariy mara tano.
Na hivi ndivyo maisha yake yalivyo kuwa kwa muda
wote akiendelea na harakati zisizo koma na juhudi za kielimu zisizo simama
mpaka akachaguliwa kuwa marjiu na kupewa cheo hicho na kuwa marjiu taqliid, na
kuanzia hapo akawa ni miongoni mwa maraajiu taqliid walio wakubwa wa madhehebu
ya Ahlul bayti na mmoja wapo kati ya wanazuoni wake, kama ambavyo alivyondelea
na kazi ya kufundisha tangu muda mrefu juu ya mimbari ya masomo ya bahthul
khaariji (masomo ya juu kabisa kwenye Hawzah) kama Fiqhi na Usuul, na masomo
yake yakihudhuriwa na kundi kubwa la wanazuoni na watu wenye elimu, kama
ambavyo idhaa ya jamhuri ya kiislaam ilivyokuwa akiviweka vipindi vya masomo
yake ili walio mbali na mji wa Qum
waweze kufaidika na ambae hakupata nafasi ya kuhudhuria masomo ya mheshimiwa
Shekh Mwenyezi Mungu amhifadhi na ampe umri mrefu.
Na baada ya kufariki sayyid Imam Khomainiy Mwenyezi
Mungu autakase utajo wake- ambae alikuwa akitilia mkazo kuwepo kwa mheshimiwa
Shekh Mohammad Faadhil kwenye Hawzah ya
kielimu, na akisisitiza juu ya ulazima wa watu
kufaidika na kuwepo kwake- waumini wengi walirejea na kuhamia kwake
katika taqliid. Na baada ya kufariki Ayatullah al-udhmaa Shekh Arakiy Mwenyezi Mungu
amrehemu hapo Shekh Faadhil alitambulishwa na kupendekezwa rasmi na jopo la
Jaamiatul mudarrisiina la Hawzah ya kielimu
kwa anwani ya kuwa ndiye mtu wa kwanza kati ya maraajiu wakubwa wa
taqliid wa umma wa kiislaam.
Mheshimiwa
Shekh - pamoj na haya ni kuwa- alikuwa akisifika na sifa njema na nzuri, na
miongoni mwa sifa ya wazi kabisa aliyo sifika nayo ni mapenzi yake ya ndani na
ya kweli aliyo kuwa nayo na kumtawalisha kwake mtume (s.a.w) na Ahlul bayti
wake walio safi na elimu zao na tabia zao, kama ambavyo alivyokuwa akisifika na usafi wa nafsi, na kupenda kwake
elimu na wanazuoni, na kunyenyekea kwake kwa waumini, na kutilia kwake umuhimu
wa masuala yote yanayohusiana na waislaamu wote kwa ujumla na hasa hasa
madhehebu ya shia, na juhudi zake alizokuwa akizifanya za kutatua haja na
matatizo ya watu na kuwasaidia kwake wanyonge na wenye matatizo (mafukara).
VITABU VYA MHESHIMIWA AYATULLAH AL-UDHMAA SHEKH MOHAMMAD FAADHIL LANKARANIY
Miongini mwa mambo ambayo inapaswa kujipamba nayo
mwanafunzi au mtafutaji wa elimu ni kukuza uwezo wake wa kuandika, ili aweze
kutunga vitabu na kuandika matokeo ya
elimu yake, kwa mfano historia na
mwenendo wa maulamaa wetu walio wengi ni kuwa wao waliandika yale waliyojifunza
na kuyajua na hawakuficha jambo lolote, na walifanya kazi kubwa na nzuri, kwa
hivyo kuficha elimu ni jambo lililo kemewa, na Mwnyezi Mungu anasema:
( إن الذين يكتمون ما أنزلنا من البينات
والهدي من بعد ما بيناه للناس في الكتاب أولئك يلعنهم الله ويلعنهم الللآعنون)
سورة البقرة: 159
(Hakika wale ambao wanaficha ukweli na uongofu tulio uteremsha baaada ya
kuubainisha kwa watu katika kitabu hao
wanalaaniwa na mwenyezi mungu na wanalaaniwa na wenye kulaani).
(من كتم علما نافعا عنده ألجمه الله يوم
القيامة بلجام من النار)
(Na mwenye
kuficha elimu yenye manufaa aliyo nayo au aliyo ipata Mwenyezi Mungu atamfunga
midomo yake siku ya kiama kwa kamba ya moto).
(ومن كتم علما فكأنه جاهل به)
( Na mwenye kuficha elimu ni kana kwamba yeye ni
jahili si mwenye kuijua elimu hiyo).
Na ili isithibiti kwa mwenye kuitafuta elimu au
mwanafunzi na mwanazuoni ya kuwa ni mwenye kuificha elimu, ni juu yake kufanya
kila njia na juhudi za kuisambaza na kuieneza kwa wengine kwa nyenzo yoyote
anayo weza kuitumia kwa kauli au kuandika na kuihifadhi kwa kuiandika ili
kizazi kijacho kiweze kufaidika nayo.
Na huu ni urithi wetu wa kielimu ambao
tumeurithi kutoka kwa maimamu wetu na
wanazuoni wetu ni ushahidi bora, na urithi huo bado upo na utaendelea kuwa ni
msingi wa elimu zetu zote, kwa hivyo basi umma hauwezi kuishi bila ya kuangalia yaliyo achwa na
wengine kwa ajili ya umma huo.
Na kila umma unahitajia wanazuoni wake wabakie
wakiwa hai kati yao na wawe ni wenye kuishi milele na milele, na inafahamika ya
kuwa wao wenyewe na viwili wili vyao huharibika na kutoweka, kwa hivyo tuishi
nao kwa fikra zao na rai zao na misimamo yao, na yote haya hayawezi kubakia
bila kuhifadhiwa na kuandikwa.
Wanafikra wana maisha mengine ( Maulamaa na
wanazuoni ni wenye kubakia kwa muda wote wa kubakia kwa dunia) na ninaweza
kuyaita maisha ya pili ya kidunia, lakini mara hii huishi kwa urithi wao wa
kielimu na maarifa si kwa viwili wili vyao.
( Hafi mwenye kuihuisha elimu), na hili ndio jambo
liwapambanualo maulamaa na wanazuoni na
watu wengine( Ipateni na itafuteni elimu
yatakupateni maisha), kwa hivyo wale ambao hawajui maisha yao ya kidunia humalizika kwa kufariki kwao na huwa kama
jiwe lililo kuwa juu ya ardhi kisha likawa chini yake.
Na hapa
kuna tashbihi iliyo nzuri ya baba wa
balagha na Faswaha na ubainifu ambaye ni
Amirul muuminiin Imam Ali ( a.s), hakika yeye amemfananisha mjinga ya kuwa
yeye( ni sawa na jiwe kubwa ambalo halitoi maji, na mti ulio mkavu usio chipua,
na ardhi isiyo mea majani)!
Na maana ya maneno haya - kwa mafhumu yake -ni
kuwa mwana zuoni yuko kinyume na vitu hivyo, yeye ni jiwe lile ambalo hupasuka
na kutoa maji au kutiririsha mito ya maji, na yeye ni sawa na ule mti ambao
watu hujikinga kwenye kivuli chake na kunufaika kwa matawi yake....., na
kututolea matunda yenye rangi tofauti, na pia yeye ni sawa na ile ardhi ambayo
imefufuka na kumea na kuotesha kila aina ya mimea.
Kwa hivyo matendo ya maulamaa na athari zao na
vitabu vyao manufaa yake ni ya watu wote, na matunda yake au faida zake ni
nyingi sana, hubakia na kuhama kutoka kizazi kwenda kizazi kingine ili waweze kunufaika nazo
kizazi hadi kizazi kingine, na nyoyo kuyapokea kwa ajili ya kujiadabisha
kupitia elimu hiyo, na mikono kupokezana kwa kupeana elimu hiyo ili waweze
kunufaika na elimu hiyo mpaka imalizike ardhi na wote waliomo kwenye ardhi
hiyo.
Haya ukiachilia mbali faida na manufaa
yapatikanayo ya kidunia kutokana na elimu au urithi huo nafasi tukufu na malipo
mema na makubwa, ( kwa hivyo mwanazuoni ambae watu hunufaika na elimu yake ni
bora kuliko ibada ya watu sabini elfu wenye kufanya ibada), hadithi inasema:( utapimwa wino wa kalamu za wanazuoni na damu
za mashahidi, na wino wa wanazuoni utakuwa ni bora zaidi juu ya damu za
mashahidi).
Kwa ajili ya haya na mengineyo tunawaona wanazuoni
wetu - Mwenyezi Mungu awalipe mema juu ya juhudi zao- ni kwa kiasi gani
wamekiandalia kizazi kijacho urithi wa kielimu, walikesha usiku kucha kwa ajili
yake mpaka wakatupatia urithi huo ukiwa umeandaliwa kwa ajili yetu, kwa hivyo
basi ni juu yetu tuwe ni warithi wao walio wema kwa kuuhifadhi urithi huo, bali
ni juu yetu kuuzidisha na kuuongeza na kuukabidhi kwa kizazi kijacho ili kiweze
kunufaika na urithi huo, na kiweze kizazi hicho kunywa kwenye mito yao ya
rahiiq na maji yao yaliyo safi.
Na Shekh Faadhil ni mmoja wapo kati ya watu hao
ambao waliendelea usiku na mchana wakiwa wamekunja magoti yao na huku wakifanya
juhudi zisizo koma, na akawa akitoa zaka ya elimu yake si kwa wale waishio
kwenye zama zake tu bali kwa wajao pia baada yao, na kwa kufanya hivyo akieneza
na kuusambaza ujumbe wake ambao ni ujumbe wa Ahlul bayti wa mtume walio
watwaharifu (a.s), kama mwanazuoni mkubwa na Faqihi mwenye elimu naye bado
anafundisha na anaelimisha na anaandika na kutunga na kufanya uhakiki kwa
kalamu iliyo wazi na ubainishaji ulio
safi ambao watu wote hufaidika nao,naye alikuwa na bado nimwenye kuendelea na
jambo hilo, na athari zake zimekuwa zikipokelewa na mikono mbali mbali maalum
ya watafutaji wa elimu ya kidini katika Hawzah ya kielimu, ili waweze kufaidika
kutokana na urithi huo na waweze kufaidika na rai makini na madhubuti zilizomo na mifumo yake
isiyo tetereka katika Fiqhi na Usuul....
mpaka vitabu vyake
mheshimiwa vikafikia mujallad 40 au zaidi ya hapo, vikiwa vimejawa na
fikra madhubuti na elimu kubwa na isiyo na kifani kutokana na ubainifu mzuri na
wa wazi.
Na vifuatavyo ni vitabu vyake:
VITABU VILIVYO ANDIKWA NA SHEKH:
1- NIHAYATU
TAQRIIR FI MABAAHITHIS SWALAAT
Kitabu
hiki kina mijalladi mitatu: 1- Juzu ya kwanza inakurasa 516, na katika
utangulizi wake kuna historia ya maisha ya imam sayyid Burujardiy Mwenyezi Mungu
autukuze utajo wake, na mukhtasari wa maisha ya muandishi wake mheshimiwa ayatullah al-udhmaa Shekh Mohammad
Faadhil lankaraniy Mwenyezi Mungu amrefushie umri, kisha baadae unafuatia
utangulizi wa muandishi, na sehemu ya kwanza ya kitabu hiki inahusiana na
utangulizi wa sala.
2-
Juzu ya pili ina kurasa 532, na kitabu hiki kime elezea sehemu ya pili: Sehemu hii inahusiana na matendo ya sala, kisha sehemu ya tatu:
Inahusu mambo yakatayo na kubatilisha sala, na sehemu ya nne: Inazungumzia
kasoro zijitokezazo kwenye sala.
3-Juzu
ya tatu, inakurasa 424, na shekh kwenye sehemu hii anakamilisha sehemu ya nne na baada ya
kuikamilisha anahamia kwenye sehemu ya tano: Inayo husiana na kulipa sala
(kadhaa), kisha sehemu ya sita: Inayohusu sala ya jamaa.
Baada
ya yote haya ameweka vyanzo na masaadir alizo zitegemea kwenye uandishi na
uhakiki wake na mtiririko wa yaliyomo kwenye juzu tatu za kitabu hiki.
Na
kitabu hiki ndiyo kitabu cha mwanzo kati ya vitabu vilivyoandikwa na
mhesimiwa ayatullah al-udhmaa Shekh Faadhil, na vitabu hivyo ni tahriri ya
masomo ya mheshimiwa Ayatullah al-udhmaa sayyid Burujardiy katika bahthi za
faradhi ya sala, aliyo yatoa kwa muda wa miaka kumi na moja aliyo ihudhuria
Shekh Faadhil kwa mheshimiwa Sayyid Burujardiy.
Na
Sayyid mwenyewe alikuwa akifahamu kuandikwa kwa masomo haya kama tulivyoelezea hapo
kabla.
Hakika
mheshimiwa Shekh alipata hadhi kubwa ya kusifiwa na Sayyid huyu kutokana na
kazi aliyo ifanya na juhudi kubwa alizozitoa kwa kufanya kazi hii naye akiwa
katika umri huo wenye baraka, na elimu yake hii iliwastaajabisha wengi kati ya
watu waliokuwa wakiishi kwenye zama zake au walio kuwa wakihudhuria masomo ya
Sayyid.
Na
kituo cha Fiqhul aimmamtul at'haar (a.s) kimesimamia kuzihakiki juzu hizi tatu
na chapa yake ya tatu ilitolewa mwaka 1420 Hijiria.
2-
TAFSWILU SHARIIAH: ( Uchambuzi wa sheria)
Hiki
ni kitabu cha Fiqhi kilichoelezea mambo ya kifiqhi kwa upana na kwa kutoa dalili, na kitabu hiki
ni sharhu au ufafanuzi wa kitabu
Tahriirul wasiilah cha mheshimiwa Ayatullahil udhmaa Sayyid imam Khomainiy
mwenyezi mungu autukuze utajo wake, na ufafanuzi wa istidlaliy ( kutoa ushahidi
na dalili) wa misingi yote ya Usuuli na Kifiqhi ambayo alikuwa akiitegemea
mheshimiwa Sayyid imam katika vitabu vyake huku akiiipinga baadhi na kubakisha na kuikubali mingine.
Na
jambo la kuvutia hapa ni kuwa waheshimiwa hawa wawili yaani muandishi asili wa
kitabu na muandishi wa sharhu wote wawili waliandika vitabu hivi wakiwa
ukimbizini na huku wakivumilia matatizo
na machungu ya ukimbizi, kwani kila mmoja alianza kazi yake yenye
manufaa na faida kubwa akiwa mafichoni, kwa mfano Sayyid imam- radhi za
mwenyezi mungu ziwe juu yake- alianza kutunga kitabu Tahriirul wasilah akiwa
ukimbizini katika nchi ya Uturuki, baada ya utawala uliokuwa ukiitawala Iran na
wanachi wake walio dhulumiwa kumfukuza, na mheshimiwa ameyataja hayo kwenye
mujjalladi wa kwanza au juzu ya kwanza ya kitabu chake Tahriirul wasilah.
Wakati
ambapo msheshimiwa Shekh Faadhil- Mwenyezi Mungu amlinde - alianza kuandika
sharhi ya Tahriirul wasilah iitwayo (
Tafswilu shariiah) naye akiwa ukimbizini kwenye mji wa Yazdi, mji ambao
alipelekwa na utawala muovu ulio kuwepo, na haya ndiyo aliyo yataja mheshimiwa
Shekh lankaraniy katika utangulizi wa kitabu Al-ijtihadi wa taqliid.
Na
kitabu hiki juzu zake nyingi zimechapishwa na zilifikia juzu ishirini, na
huenda zikafikia arobaini ikiwa Mwenyezi Mungu ataurefusha umri wa Shekh
Faadhil, wakati ambapo juzu nyengine ziko tayari kwa ajili ya kuchapishwa. Na
kati ya hivyo vilivyo chapishwa ni kama vifuatavyo:
4- AL-IJTIHAAD WAT
TAQLIID:
Na
hii ni athari moja wapo kubwa na yenye thamani kubwa, aliyo isherehesha
mheshimiwa Shekh Faadhil siku ambazo alikuwa ametolewa na utawala dhalimu na kupelekwa kwenye mji wa
Yazdi akiwa kama ni mkimbizi wa kisiasa. Na alibainisha mas’ala mbali mbali za Taqliid
na hukumu za Ihtiyaat ya mutlaq. Na kitabu hiki kina kurasa 303. Na Shekh
alikimaliza kukiandika siku ya ijumaa tarehe 25 ya mwezi wa Rabiul awal mwaka 1394 Hijiria.
5- ALMIYAAHU: (Maji)
Kitabu
hiki kinaanza kwa kuelezea mgawanyiko wa maji na mas’ala mbali mbali yahusianayo na maji pamoja na kubainisha hali
mbali mbali ikiwa yatachaganyika na
Najisi. Na kinakurasa 276. Na kitabu hiki ni kama kilicho tangulia kwani
Shekh alikisherehesha na kukifafanua katika muda alio kuwa mafichoni au
ukimbizini kwenye mji wa Yazdi. Na kitabu hichi kilikamilika tarehe 17 ya mwezi
wa Muharram mwaka 1395 Hijiria.
6- AHKAAMUL WUDHUU WAT TAKHALLIY:
( Hukumu za udhu na hukumu
za chooni).
Mheshimiwa Shekh alikitunga kitabu hiki akiwa
kwenye mji wa Yazdi mji ambao alipelekwa kama ni mkimbizi. Na ametaja
kwenye kitabu hiki mambo yote au mas’ala yote yahusianayo na mas’ala ya udhu na
istibraa, istinjaa na udhu wa pio pio (Bandeji), kwa misingi yake na fikra zake
za kifiqhi ambazo zilielezewa na mheshimiwa sayyid imam Khomeiniy Mwenyezi Mungu
autukuze utajo wake. Na kitabu hichi kina kurasa 432. Na alimaliza mheshimiwa
Shekh kukisherehesha kitabu hichi mwishoni mwa mwezi wa dhul hajji mwaka 1390
Hijiria.
7-ANNAJAASAATU WA AHKAAMUHA: (Najisi na hukumu zake)
Kitabu hichi kinahusu hukumu za Najisi na namna
vitu vinavyonajisika, kama abavyo kivyonaelezea sehemu za najisi zilizosamehewa katika sala.
Na kitabu hichi kina kurasa 492. Na kilimalizika tarehe 18 ya mwezi
mtukufu wa shaabani mwaka 1397 Hijiria.
Na kituo cha Fiqhul aimmatul at’haar kinasimamia jukumu la kukichapisha kwa
mara nyingine kikiwa kimefanyiwa uhakiki.
8-GHUSLI YA JANABA, TAYAMMUM, NA VITU VITWAHIRISHAVYO:
Kitabu
hichi kina kurasa 723. Na mheshimiwa Shekh
Mwenyzi Mungu amhifadhi alimaliza uandishi wa kitabu hiki mnamo tarehe
18 ya mwezi wa dhul qaadah mwaka 1398 Hijiria. Na mheshimiwa aliashiria
mwishoni mwa kitabu hiki matatizo wanayokumbana nayo wananchi na waislaam wa
Iran na mambo yaliyo fanywa na utawala ulio wakalia kwa mabavu, na matendeo
yake ya kidhalimu kumhusu yeye na kuhusu mali zake na vyanzo vyake vya
kiuchumi, na mheshimiwa aliashiria tukio lililo fanyika kwenye msikiti uitwao
Masjidul jaamiu wa Kirmaan tukio la kushambuliwa na vibaraka wa utawala ule
dhalimu na mashambulizi yaliyo fanywa kwa kundi la watu walio kuwa
wamekusanyika kushiriki kwenye maombolezo ya arobaini ya mashahidi waliouliwa
Tehraan, kwani waliuwawa kwenye mashambulizi hayo idadi kubwa ya walio kuja
kuomboleza, ukiongezea tukio la kuchomwa msikiti na maktaba na vyote vilivyo
kuwamo kama Qur’ani tukufu……
9- ASSALATU: (Sala)
Na
tayari imekwisha chapishwa juzu moja ya kitabu hiki, ambacho kina kurasa 687,
nacho kinazungumzia utangulizi wa sala;
utangulizi wa kwanza unahusu idadi ya faradhi na nyakati zake na sunna
zake, utangulizi wa pili unazungumzia Qibla, wa tatu unahusu kisitiri na chenye
kusitiriwa yaani nguo ya kusalia, na mwishoni mwake ameelezea nguo yenye
kushukiwa, wa nne unahusu sehemu ya kusalia, wa tano unahusu Adhana na iqamah.
Na alimaliza mheshimiwa kukiandika kitabu hiki tarehe 26 ya mwezi wa Rajab
mwaka 1400 Hijiria.
10-AL-HAJJU: ( Hijja)
Juzu
ya kwanza, inakurasa 523, Shekh katika kitabu hiki alizungumzia umuhimu wa
ibada ya Hajji katika uislaam na maana yake ya kilugha na kiistilahi na dalili
za kuwa kwake wajibu na masharti yake …. Na hijja ya Nadhiri, Ahadi, na yamini au kiapo.
Na
mheshimiwa Shekh alimaliza kuandika kitabu hiki Jumaatatu tarehe 13
ya mwezi wa Jamadul Aakhir mwaka
1411 Hijiria.
11-
Juzu ya pili, inakurasa 448, na katika juzu hii amesherehesha ndani yake
kumhijia mtu au kuhiji kwa niaba ya mtu na kuusia kufanyiwa hajji, na masuala
mengine yahusianayo na hijja ya sunna, kisha akazungumzia Umrah na wajibu wa
kufanya Umrah na mgawanyiko wake. Na baada ya hayo alizungumzia mgawanyiko wa
hajji kwa upana zaidi na hajji ya tamatuu ambayo ni moja kati ya aina za hajji.
Na
alimaliza kuandika kitabu hiki tarehe 22 mwezi wa dhul qaadah mwaka 1412
Hijiria.
12-
Juzu ya tatu, inakurasa 472, kitabu hiki kimezungumzia vituo vya kuvalia ihraam
(mawaaqiit) na hukumu zake, na Ihraam na namna ya kuvaa ihraam, kisha
akafafanua mambo yaliyo haramu na yasiyo tendwa baada ya kuvaa ihraam.
Na
Shekh alimaliza kukiandika kitabu hiki tarehe 13 mwezi wa Jumadul Aakhir mwaka
1414 Hijiria.
13-
Juzu ya nne, inakurasa 448, mtunzi alipata nafasi katika kitabu hiki kufanya
bahthi kwa upana zaidi juu ya mambao mengine yaliyo haramu, na baada ya hayo
akahamia na kuzungumzia Twawaf na mambo ya wajibu kwenye twawafu na masharti
yake na hukumu zake.
Na
juzu hii ilikamilika na kumalizika siku ya Jumaa mosi tarehe 27 ya mwezi wa
dhulhajji mwaka 1415 Hijiria.
14-
Juzu ya tano, inakurasa 480, katika juzu hii Shekh alizungumzia: Saa’yi,
kupunguza nywele, na visimamo viwili vya Arafah na muzdalifah, kisha akahamia
kwenye bahthi ya mambo ya wajibu katika Minaa, na mambo yaliyo wajibu baada ya
kumaliza matendo ya Minaa, kisha akazungumzia maudhui ya kulala Minaa na kutupa
mawe kumpiga shetani (Ramyul jimaari Athallth). Na mwishoni alizungumzia maana
ya
(
Aswadd wal Hasri na hukumu ya kila moja kati ya mas’ala hayo).
Na
alimaliza kukiandika kitabu hiki katika kumbukumbu za arobaini ya imam Hussein
(a.s) yaani tarehe 20 ya mwezi wa Safar mwaka 1418 Hijiria.
15- AN-NIKAAH (Ndoa):
Kitabu
hiki kina kurasa 656, na kinazungumzia kanuni za ndoa au Aaadabun nikaah na
sababu za kuharamishwa kuoa na mgawanyiko wa nikaha na hukumu zake, pia hukumu
za watoto na matumizi. Na alimaliza kukiandika kitabu hiki tarehe 23 ya mwezi
wa Ramadhan mwaka 1419 Hijiria. 16- AT-TALAAQ WALL MIIRAATHI: (Talaka na mirathi)
Na
kitabu hiki kina kurasa 535. Na kimeelezea masharti ya talaka na mgawanyiko wa
talaka na hukumu zake…… Na mambo yanayo wajibisha urithi vizuizi vya kurithi, na mafungu ya urithi na
hukumu zake….
Na
alikikamilisha kitabu hiki tarehe 7 ya mwezi wa Rabiuth thaniy mwaka 1420
Hijiria.
17- AL-QADHAA WA
SHAADAAT: (Utoaji hukumu na ushahidi)
Kitabu
hiki kina kurasa 560, na sehemu ya Kadhwa au utoaji hukumu imeelezea masuala
mbali mabli ya kifiqhi kama: sifa za kadhi, namna ya kutoa hukumu,
shahidi na kiapo…. Na bahthi hizi zimechukua kiasi cha kurasa 387, na
kilikamilika kitabu hiki katika mwezi wa Shaaaban mwaka 1419 Hijiria.
Ama
kitubu shahaadaati au sehemu ya ushahidi kimechukua kurasa zilizo bakia za
kitabu hiki kilicho tajwa, na kinaelezea sifa za mtoa ushahidi au shahidi, na
mgawanyiko wa haki, kisha mengineyo, na kilimalizika kitabu hiki katika mwezi
wa Safar mwaka 1420 Hijiria.
Na
vitabu hivi vitatu vya mwisho chapa yake
ya mwanzo ilisimamiwa na Markazul fiqhil aimmatul at’haar (a.s) kituo ambacho
kilisimamia kuvihakiki na kuvichapisha na kuvisambaza.
18- ALQISWAAS (Kisasi):
Kitabu
hiki kina kurasa 463. Kilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1407 Hijiria, na
hii ni chapa yake ya pili, na
kilihakikiwa na kuchapishwa na
kusambazwa na Markazu fiqhul aimmatul At’haar (a.s).
19- AL-HUDUUD:
Kitabu
hiki kiliunganishwa na ufafanuzi wenye kutosheleza wa kila mas’ala ambayo
yanahusiana na kanuni za sheria au (Huduud) na Adhabu za kiutawala, na
alimaliza shekh kukiandika kitabu hiki
na kukisherehesha mwaka 1406. Na kinakurasa 735.
Na
markazu fiqhil aimmatil at’haar
inasimamia tena kuchapishwa kwa kitabu hiki kwa mara ya pili baada ya
kukamilika uhakiki wake na kupangwa upya bahthi zake.
20- ADDIYAAT: ( Faini)
Kitabu
hiki kina kurasa 344, na Shekh alimaliza kukiandika siku ya ijumaa tarehe 16 ya
mwezi wa Jumadal uula mwaka 1418 Hijiria. Ama kuhusu bahthi zake ni kama zifuatazo: Mgawanyiko
wa uuaji, na kiwango cha faini, na mambo yawajibishayo kubeba dhamana…
21- AL-IJAARAH: ( Kukodi)
Ndani
ya kitabu hiki kuna mas’ala yanayohusiana na kukodi au kukodisha na hukumu
zake, na mwishoni mwa kitabu hiki
mheshimiwa Shekh hakuacha kuelezea matukio ya umwagaji damu yaliyotokea mwaka
1357 Hijiri Shamsia, na hiyo ni dalili ya kutilia kwake umuhimu mambo na
matukio yampitiayo na mambo mazito, na
kitabu hiki kina kurasa 441.
MUUTAMADUL USUUL:
Kitabu
hiki ni uandishi wa masomo yaliyo kuwa yakitolewa na mheshimiwa sayyid imam
Khomainiy Mwenyezi Mungu autukuze utajo wake kwa kalamu ya mheshimiwa Shekh
Faadhil Mwenyezi Mungu amrefushie umri, na kilichapishwa kwenye kumbukumbu za
kumalizika miaka mia moja tangu kuzaliwa kwa imam Khomainiy- Mwenyezi Mungu
amuwie radhi - kilichapishwa na kituo
cha (Tandhiim wa Nashri aathari imam Khomaini) mwaka 1420 Hijiria na kitabu
hiki kina juzu mbili:
22-
Juzu ya kwanza imechapishwa, na inakuras 529 na katika kurasa hizo
kumezungumziwa mambo mbalimbali: kama Al-awaamir wa An-nawaahiy, na Al-aam wal
mutlaq.. na hukumu za Al-qat’u na Adhannu na Aslul baraa’a. Haya ni yale
yahusianayo na juzu ya kwanza.
23-
Ama juzu ya pili, imeelezea Tanbiihaatul baraa’a, na Usulul amaliya zingine, na
bahthi zingine kama Taadul wa tarjiih, na Ijtihaad na Taqliid, na kikombioni
kuchapishwa baada ya kukamilika uhakiki wake kwa usimamizi wa kituo cha
aimmatul at’haar (a.s).
24-AL-AHKAAMUL WAADHWIHA:
Hiki
ni kitabu cha mas’ala ya fiqhi au kwa jina lingine ( risaalatul amaliyyah)
kilicho andikwa kwa lugha ya kiarabu. Na kitabu hiki kina kurasa 488, na kina
mas’ala 2042 katika milango tofauti ya fiqhi.
25- RISALATU TAWDHIIHUL MASAAIL:
Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha ya kifarisi
(kiajemi). Na kina kurasa 623, kitabu kimezungumzia mas’ala 2883 ya kifiqhi na
mas’ala mengi yawapatayo mukallafiin katika ibada na muaamalaati (uuzaji na ununuaji). Na
mwishoni mwake kuna muujam (kamusi) wa istilahi za kifiqhi, na kimechapishwa
kitabu hiki mara sitini na hiyo ni dalili ya kuhitajika kwa kitabu hicho.
26- RISAALATU AHKAAMU SHAR’IYYAH TAKHTASU BI SHABAAB:
Kitabu
hiki kimekusanya hukumu zinazo wiana na umri wa vijana katika milango tofauti
ya fiqhi: kama vile Twahara na vitu vinavyo twahirisha, Udhu, Ghusli, na
Tayammam, Sala za wajibu na Sunna, Funga, Khumsi, Zaka, na Muaamalaati (
ununuaji na uuzaji), Vyakula na Vinywaji, na hukumu za ndoa na mas’la
mengineyo. Na kinakurasa 216 na katika
mwaka 1376 ilitoka chapa ya nne ya kitabu hiki.
27- AL-HAWWASHI ALAA Al-URWATUL WUTHQAA:
Cha Ayatullahi Sayyid Mohammad Kaadhi
Twabatwabaiy Al-yazdiy.
Mheshimiwa
Shekh Mohammad Faadhil lankaraniy aliandika ufafanuzi wa kitabu hicho ufafanuzi
ambao ulikuwa ukipinga baadhi ya mambo
na uliokuwa na utafiti wa undani, na kitabu hiki kina kurasa 313
kulingana na utaratibu wa kitabu Al-ur’watul wuthqaa. Na chapa yake ya tatu ilitoka mwaka 1316 Hijiria.
28- MANAASIKIL HAJJI: ( Kwa lugha ya kiajemi)
Na
kitabu hiki kimekusanya maswali 1088 yanayo husiana na faradhi ya hajji na matendo ya ibada, ambayo
anayahitaji mwenye kwenda hijja kwenye sehemu
na mahali patakatifu kwa kulingana na maono na fat’wa za mheshimiwa
Shekh Faadhil Lankaraniy.
29- MADKHALUT TAFSIIR:
Na hiki ni kitabu kizuri sana kinacho elezea
kuhusu tafsiri ya Qur’ani tukufu na kuwa
kwake ni muujiza na usomaji wake na misingi ya kuitafsiri kwake, na kwamba
hakuna ugeuzaji wa aina yoyote uliomo au ulio ifika Qur’ani. Na kina kurasa 296
chapa ya pili ilitoka mwaka 1418 Hijiria.
30- AYATU TATHIIR RUAYATUN
MUBTAKIRATUN:
Kitabu hiki kimeandikwa na mashekhe wawili
watukufu Ayatullah Lankaraniy na Ayatullah Mungu amrehemu Ishraaqiy mkwewe
sayyid Imam Khomeiniy- Mwenyezi Mungu autukuze utajo wake- na asili ya kitabu
hiki kilikuwa kwa lugha ya kiajemi, kisha kikatafsiriwa kwa lugha ya kiarabu,
na ndani yake kuna dalili za wazi juu ya kuwa aya hii iliteremka kwa ajili ya
Ahlul bayti (a.s), ambao walifunikwa na kisaa (Shuka) peke yao na si wengineo.
Na
kwa hivi sasa markazul fiqhil aimmatul at’haar inafanya maandalizi ya kutoa
chapa nyingine mpya na iliyo hakikiwa ya kitabu hiki.
31- AIMMATUL AT’HAAR HAFADHATUL WAHYI FIL QUR’ANI:
Kitabu
hiki kiliandikwa kwa lugha ya kiajemi na kalamu ya kila mmoja
kati ya mashekh hawa wawili, Shekh Faadhil na Ayatullah Ishraaqiy, na kitabu
hiki kinatetea utawala au wilayah na uimamu
kwa dalili za kielimu na zilizo wazi. Chapa ya nne ilitoka mwaka 1376 na
kinakurasa 455.
32- ATTAQIYATUL
MUDAARATIYYAH:
Kitabu
hiki kidogo kimeandikwa kwenye maudhui haya kwa kutegemea misingi yenye manufaa ya kifiqhi ya imam Khomainiy, na hasa katika
umma wetu wenye madhehebu ya aina tofauti na mengi, na kilitoa athari
kubwa na kuzivutia nyoyo nyingi kati ya
wapenzi wa madhehebu haya, baada ya siasa kufanya kazi yake na kuacha cheche
zake na alama zake katika tofauti hizi, na aina hii ya taqiyyah ikawa ni jambo
la lazima bali hata kufikia kuwa wajibu, kwa ajili ya kuhifadhi umoja wa
waislaam.
33- AL-QAWAAIDUL FIQHIYYAH:
Kitabu
hiki – kilicho chapishwa katika mwezi mtukufu
wa Muharram mwka 1416 Hijiria kikiwa na kurasa 550- kinazungumzia kanuni
ishirini muhimu katika fiqhi au sheria
ya kiislaam na kuzihakiki. Na kanuni
zenyewe ni kama zifuatazo:
1-Qaaidatu adamu dhamaanul amiin illa ma’a taadiy wat tafriit. Kanuni ya
kutochukua dhamana alie wekeshwa amana isipokuwa ikiwa atafanya uchokozi na
kuzembea.
2-Qaaidatul itlaaf . Kanunim ya kuharibu mali ya mtu.
3-Qaaidatul iqraarul uqalaa alaa anfusihim jaaiz. Kanuni ya kuwa
wenye akili kukiri juu ya nafsi zao ni jambo linalo faa.
4-Qaaidatu alal yadi maa akhadha
hatta tuaddaa.
5-Qaaidatul ilzaam.
6-Qaaidatu man malaka shay’an
malakal iqraau bihi.
7-Qaaidatu Al-maghruuri yarjiu ilaa
man gharrahu.
8-Qaaidatu nafyus sabiil.
9-Qaaidatul jubbi.
10-Qaaidatul ihsaan.
11-Qaaidatul ishtiraak.
12-Qaaidatul ishtiraakil kuffar ma’al muuminina fit takliif.
13-Qaaidatu adamushartiyyatul bulugh fil ahkaamil wadh’iyyah.
14-Qaaidatu mashruuiyyatu ibaadatu swabiiy wa adamihaa.
15-Qaaidatu amaariyyatul yad.
16-Qaaidatul qur’aah.
17-Qaaidatu hurmatul iaanatu alal
ithmi.
18Qaaidatu hujjiyyatul bayyinah.
19Qaaidatu hujjiyyatu suuqul
muslimiin.
20-Qaaidatu akh’dhi ujrata alaal
waajibi.
34- KITABU TWAHARAH:
Kitabu hiki ni tahriiri ya masomo ya imam
Khomeiniy na kiko mbioni kuchapishwa.
JAAMIUL MASAAIL: (Kitabu hiki ni juzu
mbili)
35- Juzu ya kwanza: ina kurasa 640 pamoja na
mas’alala 2248.
36- Juzu ya pili: inakurasa 496 na mas’ala 1307.
Na kila juzu ina fat’wa zilizo chaguliwa kati ya fat’wa nyingi zielekezwazo kwa
mheshimiwa Shekh Faadhil pamoja na
majibu yake.
37- AL-ISTIFTAA AATI HAWLAL HAJJI WAL UMRAH:
Kitabu
hiki kinakurasa 144, na kimekusanya maswali yaliyo elekezwa kwa mheshimiwa
Shekh Mwenyezi Mungu amuhifadhi, na majibu yake juu ya maswali hayo.
38- AHKAAMUL HAJJI MIN KITAABI TAHRIIRUL WASIILAH:
Kitabu
hiki ni ufafanuzi wa mheshimiwa Shekh Faadhil – Mwenyezi Mungu amlinde - wa
kitabu Tahriirul wasiila cha Sayyid imam Khomeiniy –Mungu autukuze utajo
wake- wa sehemu ya hajji, na kina kurasa
144 na kina mas’ala mbali mbali kuhusu faradhi hii tukufu, na hadi sasa
imekwisha toka chapa ya tatu, na kituo cha Fiqhu aimmatul at’haar ndicho
kilicho simamia kuchapishwa na kusambazwa kwa kitabu hiki.
39- AL-FATAAWAL WAAFIYAH:
Juzu
ya kwanza, inakurasa 600 na kiko mbioni kuchapishwa. Na kimekusanya mswali
mbali mbali ambayo huelekezwa kwa mheshimiwa Shekh Faadhil Mungu amlinde pamoja
na majibu yake.
40- MANAASIKUL HAJJI: (Kwa lugha ya kiarabu)
Kitabu
hiki kuna kurasa 386.
41- AHKAAMUL UMRATUL MUFRADAH. ( Kwa lugha ya kiajemi)
Kitabu
hiki kina kurasa 256 na kimechpishwa mara sita.
IFUATAYO NI MIHADHARA YAKE
SHEKH ILIYO ANDIKWA.
1-TIBYAANUL USUUL:
Na
hiki ni tahriri ya mihadhari au masomo
ya Shekh Faadhil –Mwenyezi Mungu amhifadhi- kwa uandishio wa mmoja wapo kati ya
wanafunzi wake, aliyokuwa akiyatoa, na kwenye kitabu hicho kuna masuala ya Al-qat’i wadhanni,
Al-imaaratu wal- usuulul amaliyyah. Na kwa hivi sasa juzu ya tatu tu ndiyo
yenye kupatikana, na kina kurasa 354, chapa yake ya kwanza ilikuwa mwaka 1414
Hijiria.
Na
mheshimiwa Shekh amesema kuhusu kitabu hiki: Nimekikuta kikiwa ni chenye
kutosheleza malengo bila ya kuzidisha wala kurudia rudia kunako chosha wala si
mukhtasari wenye upungufu.
2- DUSTUURUL IDAARAH INDAL IMAM ALI (A.S).
Madhumuni
ya kitabu hiki ni kufafanua na kusherehesha usia ulio andikwa na imam Ali
kwenda kwa Maalik Al-ashtari walii wake kwenye nchi ya Misri. Na kimeandikwa
kwa kalamu ya mmoja kati ya wanafunzi wake na ni tahriri ya bahthi ya
mheshimiwa Shekh. Na chapa yake ya kwanza ilitoka mwaka 1366 Hijiria Shamsia,
kisha kikachapishwa tena mpaka ikafikia chapa ya saba mwaka 1379, na kina
kurasa 206, kitabu hiki kina bahthi
nzuri na makini sana.
3-7- IIDHWAAHUL KIFAAYAH:
Mheshimiwa Shekh Faadhil alisomesha daura
kamili katika sutuuh kitabu Kifaayatul Usuul. Na dauru ya mwisho imerekodiwa,
na mmoja kati wanafunzi wake aliiandika na kuichapisha kama kitabu kwa jina la
IIDHWAHUL USUUL.
Na kina mijjalladi mitano, na kitabu hicho ni
miongoni mwa sharhu mash’huri na iliyo makini kati ya sharhu za Kifaayatul
usuul kwa lugha ya kifursi. Na juzu zote
hizi tano zinakurasa 2560. 8- 23- ASSAYRUL KAAMIL FII USUULIL FIQHI: (Asili yake ni kiajemi)
Kitabu
hiki ni daura kamili ya bahthi za Shekh Faadhil Mungu amlinde alizo kuwa
akizitoa kwenye bahthi za kharijii (masomo ya juu ya Hawzah) kwa muda wa miaka
kumi, na kina mijjalladi 16 iliyo chapishwa hadi hivi sasa.
Kila
mujjalladi mmoja una kurasa 640, tisa kati ya mijjalladi hiyo inazungumzia
bahthi za Al-faadhi (maneno au Lafdhi), wakati ambapo mijaladi mingine
inazungumzia bahthi za Al-qat’u wa Adhannu na Ijmaau na Hujjiyyatu khabarul
waahid, kisha bahthi za Ussulul
amaliyyah.
24-28- TASHRIIHUL USUUL:
Vitabu
hivi ni sehemu nyingine ya tahriri ya masomo ya Shekh Faadhil katika Usuulul
fiqhi, kwa uandishi wa wanafunzi wake wawili walio kuwa wakihudhuria darsa
zake, mijalladi mitano iko tayari kwa ajili ya chapa, na tunataraji itafikia
mijalladi kumi.
29-30- KITAABUL HUDUUD: (Kwa lugha ya kiajemi)
Kitabu
hiki kina juzu mbili, juzu ya kwanza inakurasa 670, na juzu ya pili inakurasa
757, nacho kiko mbioni kuchapishwa.
VITABU VYA SHEKH VISIVYO
CHAPISHWA
1-Tafsiru
suuratul hamdu. Na hii ni tafsiri bora kabisa ya aya za sura hii tukufu.
2-
Ufafanuzi wa baadhi ya bahthi za Tahriirul wasiilah.
3-
Kitabul ijaarah, na hiki ni tofauti na kitaabul ijaara fii sharhi Tahriirul
wasiilah.
4-Qaaidatu
laa dharara, na hii ni tahriiri ya bahthi za sayyid imam Khomeiny.
5-
Risaalatun fii swalaatil jum’ah.
6-
Al-khumsi, ni tahriir ya masomo ya Sayyid Burujardiy.
7-
Al-khumsu min mawsuuah, kutoka kwenye kitabu (Tafsswiilu shariiah fii sharhi
tahriirul wasiilah).
8-
Ufafanuzi wa kitabu ( Atwaharah) kutoka kwenye kitabu Misbaahul faqiih cha
marhuum Al-muhaqiqul Hamadaniy Mungu amrehemu, na huyu ni miongoni mwa maulamaa
wakubwa walio pita. Na kitabu chake hiki kimezungumzia mas’ala ya twahara kwa
tahkiki ya Ayatullah Shekh Mohammad Faadhil Lankaraniy.
9-
Kitabu swaumu.
Mwanzoni
mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka 1405 Hijiria mheshimiwa Shekh Faadhil alianza kukiandika kitabu hiki, na
ame elezea bahthi nyingi zinazo husiana
na funga na bado hakijakamilika.
10-
Al-masaailul mustahdathah.
Kitabu hiki ni miongoni mwa tahriri ya
bahthi au masomo ya sayyid Khomeiniy. Na kitabu hiki kime elezea baadhi ya
bahthi mpya, kama dhamana na mikataba ……………….
11-
Kitaabul qadhaa.
Kitabu
hiki kimeandikwa na yeye Shekh mwenyewe, na msingi wa kitabu hiki ni masomo
ya mheshimiwa Ayatullah sayyid
Burujardiy katika utoaji hukumu
(Al-qadhaa), na jambo la kusikitisha ni kuwa mauti hayakumpa firsa ya kuweza
kukikamilisha kitabu chake hiki.
12-
Ufafanuzi wa kitabu Atwahara kutoka kwenye kitabu Sharaaiu cha muhaqiqi
Al-allamah al-hilliy Mwenyezi Mungu autakase utajao wake. Na kitabu hiki
kilicho andikwa kwa hati za mkono kina kurasa 135, na sharhu yake imekamilika
hadi kwenye mas’ala ya kurudia kupaka ( Tikraarul mas’hi).
13-
Ufafanuzi wa Fuuruu’ul ijtihaad wa taqliid kutoka kwenye kitabu Al-urwatul wuthqaa. Shekh Faadhil alianza
kukisherehesha kitabu hiki katika mwezi wa Jumaadul uulaa mwaka 1384 Hijiria,
na kime elezea mas’ala sitini na nane kati
ya mas’ala husianayo na bahthi ya ijtihadi na taqliid ambayo yametajwa
kwenye kitabu kiitwacho (Al-ur’watul wuthqaa) cha Sayyid Twabatwabaiy Al-yazdiy Mungu autukuze utajo
wake.
14-
Risaalatun fii ahkaamis swalaat fii libaasil mashkuuk.
Kitabu ni tahriri
ya mheshimiwa Shekh Faadhil ya bahthi za sala zilizo tolewa na
mheshimiwa Ayatullah al-udhmaa Sayyid
Buruujardiy, na alianza kukiandika tarehe 22 mwezi wa Safar mwaka 1371 Hijiria.
15-
Ismatul anbiyaa.
Hiki
ni kitabu kilicho andikwa kwa lugha ya kiajemi kinacho thibitisha Ismaa ya
mitume kulingana na aya za Qurani tukufu.
16-
Al-qawlu fil mushtaqq.
Ni tahriiri ya masomo ya sayyid Burujardi.
17-
Al-qawlu fil awaamir.
Pia ni tahriiri za masomo ya Sayyid
Biruujardiy mungu amrehemu.
18-
Al-qawlu fii shuhratil fat’waaiyyah.
Pia ni tahriiri ya bahthi na masomo ya Sayyid
Buruujardiy.
19-
Risaalatun fii qaaidati ( laa haraj) ya
kifiqhi.
20-
Ufafanuzi wa kitabu Al-mudwaarabah wal muzaara’a wal musaaqaat kutoka kwenye
kitabu Tahriirul wasiilah.
HARAKATI ZA SHEKH ZA KISIAS
Wakati
ambao nchi ya iran ilikumbwa na balaa la kutawaliwa na tawala mbaya na dhalimu
na watawala madikteta waovu na
mutakabbirina kwa muda mrefu wa historia ya nchi hiyo, na wa mwisho katika
utawala huo akiwa Mohammad Ridhaa pahlawiy na utawala wake muovu, na aliyekuwa
akifuata madola makubwa na jeuri ulimwenguni
yakiongozwa na Amerika, kutokana na tukio hili lenye kuumiza na lenye
kutesa watu kulijitokeza na kuamka harakati za ukombozi na zenye kuelewa mambo
vyema na vikajitokeza vikundi vya kuendesha mapambano makali, na baadhi ya watu
mashuhuri walio jitolea kwenye njia ya Mwenyezi Mungu kupambana na utawala
ule, na kupinga mambo ya kuhuzunisha na kusikitisha yaliyo wekwa na
utawala ule dhalimu na yaliyo acha kwenye nchi hii kilio na masikitiko makubwa
pia kilio cha muda mrefu kisicho koma kwa wananchi na watoto wa waislaam wa
nchi hii walio kuwa wakipigana kuondoa utawala huu, kutokana na sababu hii
maulamaa wengi na wanafikra wengi wa nchi hii
walipatwa na misukosuko mingi
kama kuuwawa na kuadhibiwa na kuteswa na kutiwa jela, pia kufukuzwa na kulazimishwa kwenda mafichoni, kwa sababu
wao walikuwa ndio kundi la vijana lililo kuwa na uelevu na ufahamu wa mambo
haya ya kisiasa na kundi lenye imani na lenye kupigana jihadi katika uwanja huu
na malumbano haya ya kisiasa na kiutawala yaliyo makali na upambanaji uliokuwa
mkali, na kati ya kundi hilo la maulamaa walio kuwa wakiendesha harakati hizi
ni mheshimiwa Shekh Mohammad Faadhil Lankaraniy, ambae alikuwa akitoa misimamo
yake mikali ya kisiasa dhidi ya utawala
wa Shaha na uendeshaji wa harakat, pia misimamo yake ya kisiasa ilikuwa ikitoa
na kuonyesha pia kutoa mchango wa aina ya pekee na nguzo ya msingi kabisa
katika maisha yake ya kijamii na kisiasa na kijihadi, mpaka misimamo hiyo
ikamfanya achukue hatua madhubuti na awe na msimamo madhubuti na hatari
kuuelekea utawala, na njia zake na mipango yake ya haraka ilikaribia kumlazimu
kutoa maisha yake.
Tangu
mheshimiwa Sayyid imam Khomainiy alipo anza
kwenye zama zetu hizi kufanya maandalizi yake na kujiandaa yeye mwenyewe
na wafuasi wake na wapenzi wake kupambana na utawala fasidi ulio wakalia watu kwa mabavu, na
kuondoa dhuluma na taabu kwenye umma huu wa kiislaam ulio dhulumiwa na wenye
kupigana jihadi, na kukata mikono ya
madhalimu kwenye mali ya watu wa nchi hii walio kandamizwa na kukaliwa kwa
mabavu, na kuupiga vita ukafiri wa kiulimwengu ambao unajiona kuwa ndio wenye
haki kutawala pakee na utawala wa kidikteta na ambapo shaa alie zikwa alikua ni
sehemu moja wapo ya kufru hiyo, na alikuwa ni mwenye kupita kwenye mzunguko huo
na mwenye kufuata mkia wa miundo yake na mikakati yake ya uovu.
Mheshimiwa
Shekh Mohammad Faadhil ambae alikuwa ni
miongoni mwa wanafunzi wa imam waliokuwa mstari wa mbele na akiwa ni kati ya watu wampendao kidhati na kiuhakika na walio kuwa tofauti na wengine, alikuwa akimfuatilia
ustadhi wake katika kila hatua za kijihadi na alifanya hivyo kutokana na imani
aliyokuwa nayo ya usahihi wa misimamo
yake na usahihi wa mwenendo wake na umakini pia umadhubuti wa rai zake zisizo
tetereka na zilizo simama juu ya msingi wa maarifa na ufahamu kamili wa mambo,
misimamo na ufahamu ambao ulitokana na jukumu la kisheria alilo bebeshwa na kupewa, Mungu amwie radhi.
Mheshimiwa
Shekh akawa ni miongoni mwa wale ambao waliungana naye na kuto muacha katika
mapambano yake yale ya kijihadi na ni miongoni mwa watu walio simama imara na
thabiti kwenye mfumo wake imam.
Na
akaendeleza mapambano yake ya
jihadi yaliyo kuwa makali na
kuumiza, sawa akiwa peke yake au akiwa
ameungana na ndugu zake wengine na wakiwa wameunda kikundi chenye kuitilia shindikizo
serikali tawala, na yeye alikuwa ni miongoni mwa jopo la Jamaaatul
mudarrisiin jopo ambalo lilikuwa na
harakati na nashati kubwa zilizoamsha ghadhabu ya utawala ule.
Na
wakati utawala ule ulipo waamrisha
vibaraka wake kumkamata Imam, na baada ya kazi hiyo kufanyika aliwekwa jela
mpaka itakapo kamilika kazi ya kumhukumu,
maulamaa kumi na mbili wa hawzah
na wanafunzi wao – na Shekh Faadhil akiwa ni mmoja wao - walitoa tamko
wakiutaka utawala na viongozo wake kumuachia huru Sayyid imam Khomainiy, na wakautaka kuto mhukumu, kwani yeye ni miongoni mwa
mamujtahidi wakubwa, na katiba ya nchi hairuhusu kumuhukumu mwanazuoni au
aalimu alie fikia kwenye daraja hiyo.
Na
pindi utawala ulipo hisi hatari inayo jengeka kwa kuwepo mheshimiwa Shekh ilitoa amri ya kukamatwa na kupelekwa
mafichoni na kumweka sehemu ambayo huhesabiwa kuwa ni sehemu mbaya zaidi katika
Iran, na alipelekwa kwenye sehemu
iitwayo ( Bandar langeh) kiasi kwamba joto la sehemu hiyo ni la hali ya juu
sana, na alimaliza muda wa miezi minne kwenye sehemu hii ya mbali.
Mheshimiwa
anasema kuhusiana na sehemu hii: (Hakika miezi hii mine ilikuwa ni sawa na
miaka arubaini kutokana na machungu yake na mitihani iliyo kuwa huko).
Kisha
utawala ukamhamishia kwenye mji wa Yazdi pia mji huo uko mbali na mji mtukufu
wa Qum na Hawza ya kielimu ambayo alikuwa akiipenda, na alimaliza kwenye mji
huo muda wa miaka miwili na nusu kati ya umri wake mtukufu akiyavumilia
matatizo na machungu ya mji huo.
Pamoja
na matatizo na machungu au maudhi yaliyokuwamo kwenye mji huo isipokuwa ni kuwa
mheshimiwa alikuwa akijishughulisha na kufanya tahkiki na utafiti wa kielimu na
uandishi, na akifaidika na nafasi hii ya kuwa faragha ambayo alilazimishwa
kuwamo kwa nguvu. Na hali hii ni katika upande mmoja.
Na
kwa upande mwingine alipokuwa Yazdi alijishughulisha na kujenga mahusiano
madhubuti kwa njia ya siri pamoja na shahidi wa mihraab Ayatullah Swaduuqiiy,
na walikuwa pamoja na kundi la waumini wakiwaandaa watu na wakiandaa njia ya
kufanya mapinduzi dhidi ya utawala dhalimu.
Na
kutokana na juhudi zao hizo watu wawili hawa na kutokana na ufahamu wa kina
ulio enea kwenye mji wa Yazdi ukianza na wale watu wa mwanzo walio itikia wito
wa mapinduzi na kutoa mashahidi wengi, kwani walikuwa wakipigana na utawala na
askai wake kwa nikono mitupu wakiwa hawana silaha na wakipambana na silaha zao
kwa nyoyo na vifua vlivyo jawa na imani na kupenda kufa shahid, mpaka Mwenyezi Mungu
akawathibitishia wao na wananchi wa Iran walio waislaam ushindi na kuweza
kusimamisha dola la kiislaam dola ambalo
kwa muda mrefu walikuwa wakiliota wote kwa pamoja.
UTAMBULISHO WA KITUO CHA FIQHUL AIMMATUL AT’HAAR ( A.S)
Kutokana
na kufahamu kwa mheshimiwa Ayatullah Al-udhumma Shekh Mohammad Faadhil
Lankaraniy Mwenyezi Mungu amlinde, umuhimu uliopo na faida nyingi, pia manufaa
mengi yapatikanayo kwenye taasisi na vituo vya kielimu, ni dalili ya kupevuka
na kuwa na ufahamu mkubwa, kama ambavyo hiyo ni dalili na muongozo wa kila
mfanya utafiti mwenye kufanya juhudi na mwenye kutafuta elimu akiwa na nia
safi ( Mukhlis) na mtu mwenye fadhila
na mkweli.
kutokana na maswaadir na vyanzo na za rejeo (referene)za
kifiqhi na harakati za kielimu, ukiongezea na mazingira uwanja unaoandaliwa na vituo hivyo vya kielimu pamoja na utafiti
na tahkiki mambo ambayo hayapatikani
isipokuwa kupitia taasisi hizo, basi haiwezekani Hawzah ya kielimu
kujisahaulisha na kujitosheleza na
kuufumbia macho umuhimu na ulazima wa
taasisi hizo, na hasa ukizingatia kuwa ni kituo kilicho sifika na sifa ya kuwa
ni kituo cha kisasa na cha takhassusi katika ulimwengu ambao maarifa na elimu zimepanuka na rai pia fikra mbali mbali kudhihiti na kudhihiri
waziwazi, takhassus ikawa ni jambo la muhimu sana ikiwa
hatukusema kuwa nila wajibu.
Kwa ufahamu wa Shekh wa mambo haya na
mengineyo, mheshimiwa Mungu amlinde
akachukua jukumu kwa kupitia juhudi za kundi fulani la waaumini wenye
ikhlas kati ya watu wenye kufahamu umuhimu wa kuyabeba majukumu haya , na
kuanzisha vituo vya kielimu vya takhassus.
Vituo
ambavyo - pamoja na vitabu mihimu
vilivyomo kwenye vituo hivyo na vyanzo mama vya kila madhehebu – vituo hivyo
vina harakati nyingine za kiutafiti, na
vimekuwa vikianzishwa na kundi la wanafunzi wake wakubwa, na walio na kiwango
cha juu kabisa ambao walipata kiwango kikubwa cha elimu na wakawa makini huku
wakifanya juhudi za kufuatilia masomo yao ya Hawzah, na pembezoni mwao kukiwa
na wafanyao utafiti na bahthi, na kukiwa na wahakiki watiliao umuhimu suala la
bahthi katika urithi wa kifiqhi na Usuul
na ambao wamesifika na kupambika na sifa ya uvumilivu na kuto kata tamaa katika
kazi na wasio acha kufanya kazi hizo, hata kama juhudi zao zitatoa matunda na
faida ndogo katika muda huu mfupi ispokuwa matarajio ni kwamba - kutokana na
tawfiqi ya Mwenyezi Mungu – juhudi hizo zitazalisha na kutoa matunda au faida
yenye manufaa .
Nataraji
sintakuwa nimezidisha katika kusifia-ikiwa nitasema ya kuwa: Hakika kituo hiki cha kifiqhi kinahesabiwa kuwa ni kituo
moja wapo cha pekee na cha aina yake katika uwanja huu, pamoja na tuliyo
yabainisha hapo kabla na haya yafuatayo, kinasifika kuwa ni kituo cha kisasa
katika utaratibu wake na mfumo wake, bali pia malengo yake yaliyo mema.
Na
hatuta kuwa mbali na ukweli ikiwa tutasema: hakika kituo hiki kinafanya utafiti
kuhusiana na fiqhi iliyo sambamba na zama hizi na misingi ya kufanya ijtihadi,
kikizingatia kwa makini kabisa zama hizi na matatizo yake, kikifaidika na
urithi wote wa fiqhi ya kiislaam na milango yake na bahthi zake zilizo nyingi
kulingana na madhehebu zake tofauti, na kikifanya juhudi kubwa kuyachukua
yaliyo sahihi au kuzichukua riwaya zilizo sahihi na kuziacha zilizo dhaifu na
zilizo pandikizwa, kwa kutumia dalili za kielimu zenye nguvu na imara na zilizo
mbali na taasubi (mapenzi tu yasiyo na dalili) yenye kuchukiza na
ujizuiliaji ulio pofu na wenye kufuata madhebu, na wenye kuchukia kuupima urithi wa kielimu kwenye vipimo vya
kielimu pekee na si vinginevyo, kikiitetea fiqhi na ufaqihi ambao unasifika na
sifa ya usafi na kuto kuwa na shubha ndani yake na unaochambua mas’ala kwa
undani kabisa, na ambao msingi wake
unakuwa ni kitabu kitukufu na sunna sahihi na rai za maimamu wakubwa wa
waislaam na mafaqihi wenye ikhlaasi, kikitoa neno zuri na fikra iliyo safi, na
kinafanya hivyo ili kuunda familia zenye uwezo wa kubeba majukumu na kizazi
chenye kufahamu majukumu yake ya kiislaam na kikiufanya umoja wa kiislaam kuwa
ndio lengo lake lenye kutarajiwa kufikiwa.
Na
ni uzuri ulioje wa kazi hii na juhudi hizi zenye kushukuriwa za kuchambu na
kuchekechwa urithi huu, ili kupata
urithi usio na kasoro na uchafu ndani
yake, na kuyatupilia mbali yanayo udhuru mwendo wa umma, umma ambao mwenyezi
mungu (ameuweka kati ili uwe shahidi juu ya watu na mtume awe shahidi juu
yenu)!
Kwa
ajili ya sababu hizi na malengo haya na huenda kukawa na malengo mengine yasiyo
kuwa haya, kituo hiki kiliimarisha nguzo zake kikifaidika na ushauriwa na
maelekezo ya mheshiomiwa Ayatullah al-udhmaa Shekh Faadhil Lankaraniy mwenyezi
mungu amlinde, na kikaweza kituo hiki
tangu miaka mitatu iliyo pita na huu ukiwa ni muda mfupi, kusimamia na kutekeleza baadhi ya mambo
machache na kufanya juhudi za kielimu huku kukitaraji harakati hizo kupanuka
zaidi na kuzama na kuwa ni zenye manufaa zaidi na zenye athari kubwa, kwa
tawwfiq na usaidizi kutoka kwake subhaanahu.
VITENGO VYA
KITUO HIKI.
Katika
kituo cha Fiqhul aimmatul at’haar (a.s) kuna vitengo vitano, na kila kitengo
kina majukumu maalum na mas’uliyya kiyatekelezayo.
KITENGO CHA KWANZA: KITENGO
CHA TAALUMA
Katika kitengo hiki kuna nyanja na harakati
mbalimbali za kielimu:
a- jopo la masuala ya Qadhaa utoaji hukumu au
uhakimu.
b-Jopo la masuala ya Hajji.
c- Jopo la uchumi wa kiislaam ( ukodishaji)
d- Jopo la Usuulul fiqhi.
e- Jopo la kanuni za kifiqhi.
Na kila jopo moja wapo kati ya majopo haya kina
wanafunzi watano walio bora na walio
chini ya uangalizi wa mwalimu mwenye uzoefu na mwanazuoni mwenye fadhila.
Na washiriki wote katika vitengo hivi, jukumu lao
ni kuzitafuta rai na kuzifanyia utafiti na kuzijadili kwa dalili za kielimu. Na
mpaka sasa wamemaliza mwaka wa tatu katika kazi hii, na tunataraji juhudi zao
hizi zitatoa matunda yenye kuwanufaisha watu wote, na Kitabu (Qaaidatul qur’ah)
kilicho andikwa na mheshimiwa hujjatul islaam wal muslimiina Al-haji Shekh
Hussein Kariimiy mwalimu wa jopo mojawapo kati ya majopo haya, ni matokeo na matunda ya utafiti huu, na
kilikamilika mnamo mwezi wa ramadhani mwaka 1419 Hijiria.
KITENGO CHA PILI: UTUNGAJI WA VITABU
Hakika majukumu ya
utendaji kazi wa kitengo hiki ni Fiqhi na Usuul, na kitengo hiki kina
idadi kadhaa ya wanazuoni wa Hawzah, ambao wanasifika kwa elimu na uvumilivu na
ustahamilivu katika kazi yao, na majukumu yao ni kama yafuatayo:
1-kuandika daura kamili katika maudhui ya Ussulul
Fiqhi kwa lugha ya kiajemi wakitumia mifumo ya bahthul khaariji katika elimu ya
Usuul ya shekh Ayatullah Al- udhmaa Faadhil Lankaraniy na hadi sasa daura hiyo
imevuka mijalladi kumi, na hadi hivi sasa mijallad mitano imekwisha kamilika
nayo iko mbioni kuchapishwa na kwa kuzingatia kuwa hakuna kitabu hadi sasa
kwenye bahthi hii na kilicho zungumzia kwa upana katika lugha ya kiajemi.
2- Kuandika daura kamili katika Usuulul fiqhi kwa
lugha ya kiarabu kwa kujitegemeza au kwa kutumia mifumo ya bahthi ya khariji
katika elimu ya Usuulul fiqhi ya Shekh Ayatullah Al-udhmaa Faadhil Lnkaraniy.
3- Kufanya bahthi ya kupingana kati ya Al-asli na
Adh-dhaahiri, na haya ni miongoni mwa maudhui muhimu katika elimu ya Usuul, na
bahthi hii inafanya uhakiki na utafiti katika sehemu za kupingana kati ya
Al-asli na Adh-dhahiir, na kazi hii imekamilika na kitabu chake kikombioni
kuchapishwa.
4- Kuandika Mawsuuatu ahkaamu swibyaan.
Hiki ni kitabu cha fiqhul muqaarin kinacho elezea kwa upana na kukusanya hukumu za madhebu zote
za kiislaam, zinazohusiana na watoto ambao hawaja balee, zinazo husu malezi
yao, ibada zao, ufanyaji biashara wao,
na haki zao… na kinazungumzia hukumu zote kwa ujumla zinazo husiana na
wao.
Na kazi hii imekabidhiwa kwa watu sita kati ya
wanazuoni wakubwa wa Hawzah ya kielimu, na juzu ya kwanza ya mausuua hii,
ambayo tunataraji kuwa itakuwa ni mijalladi kumi, iko kwenye hatua ya
kuchapishwa.
5- Kitabul huduud kwa lugha ya kiajemi, na kitabu
hiki ni tahriiri ya masomo ya khaariji katika fiqhi ya mheshimiwa muasisi wa
kituo hiki, na kina mujalladi mbili.
6- Kuandika kwa lugha ya kiarabu juzu ya kwanza ya
kitabu Jaamiul muasisi, na ambacho kina maswali mbali mbali yaelekezwayo kwa
mheshimiwa Shekhe muasis, na kitabu
hicho kina jina la ( Al-fataawaa Al-waafiyah) na kiko tayari kwa ajili ya
chapa.
KITENGO CHA TATU: UHAKIKI NA
USAHIHISHAJI
Hakika
majukumu ya kitengo hiki yana hatua tatu:
Hatua
ya kwanza: kutoa hadidi za rejea.
Hatua
ya pili: Kusahihisha na kuzitathmini dalili (Nusuus).
Hatua ya tatu: Kuziangali na kuzisahihisha.
Na baada ya kumalizika hatua hizi tatu huanza kazi
ya kuchapishwa kitabu. Na hadi sasa imekamilika kazi ya kuchapishwa vitabu vifuatavyo:
1-
Nihaayatut taqriir, kitabu hiki kina juzu tatu. Na kitabu hiki ni tahriiri ya
masomo ya khaariji ya mheshimiwa Ayatullahil udhmaa sayyid Burujardiy mungu
amrehemu kwa uandishi wa mheshimiwa Ayatullahil udhmaa Shekh Faadhil
Lankaraniy- Mwenyezi Mungu amzidishie umri- kwa muda wa miaka 11 aliyo imaliza akihudhuria kwenye masomo ya
mheshimiwa sayyid Ayatullah al-udhmaa Burujerdiy.
2-
Q aaidatul qur’pah.
Kitabu
hiki kimekamilika kwa juhudi za kundi la wanafunzi wa kituo hiki.
3-Na
kuna bitabu vingine vya mheshimiwa Shekhe muasis, ambavyo kazi ya kurejea
maswaadir na usahihishaji wake
umekamilika kwa juhudi za kundi
mojawapo la wanafunzi wa kituo hiki, na
baadhi tiyari vimekwisha chapishwa navyo ni kama vifuatavyo:
1-Kitaabul qadhaa.
2- Kitaabush- shahaadaat.
3-Kitaabul qiswaas chapa ya pili.
4-Kitaabu twalaaq wal mawaariithi.
5-Kitaabun nikaah.
Na vitabu hivi vitano vimeandikwa na Shekh muanzilishi na muasisi wa kituo hiki na
ukiwa ni ufafanuzi wake juu ya kitabu Tahriirul wasiilah cha mheshimiwa
Ayatullah Al-udhmaa sayyid imam Khomainiy mungu amrehemu.
Na
kunavitabu vingine vya Shekh muasisi ambavyo viko njiani kwa ajili ya uhakiki,
uchapishaji na usambazaji. KITENGO CHA NNE: MAKTABA YA KIFIQHI
YA TAKHASSUS
(فيها كتب قيمة)
Katika
ulimwengu ambao kila uwanja wa kielimu kitamaduni na kiamali unajifunga kwenye
mfumo wa takhassusi, hakika maktaba ya takhassus inajikuta kwamba nafasi yake
ina umuhimu mkubwa katika nyanja hizo na inaulazima mkubwa wa kuwa hivyo,
haiwezekani kwa harakati zozote za kielimu kujitosheleza na kutolitilia
umuhimu jambo hilo, kwa hivyo
kukianzisha kituo hiki ni kazi moja muhimu na iliyo elewa vyema umuhimu huu na
iliyo hisi mahitajio kama hayo hasa
kwenye jamii yetu ya Hawzah.
Kwa
sababu hii ndio maana ikaanzishwa maktaba hii kwa mara ya kwanza kabisa katika
Hawzah ya kielimu ya Qum, na maktaba hii
ikafanywa kuwa ni maalum kwa ajili ya Fiqhi na Ussul za madhehebu zote za
kiislaam: Fiqhi ya kishia, Fiqhi ya
shafiiy, Fiqhi ya Hanbaliy, Fiqhi ya Hanafiy, Fiqhi ya Maalikiy, na Fiqhi ya
madhehebu zingine kama Zaidiyya na Dhaahiriyyah… Usuulul fiqhi ya shia, Usuulul
fiqhi ya Ahlu sunnah, Uluumil qur’ani na ayaatul ahkaam kwa mashia na Ahli
sunnah, historia ya Fiqhi, Historia ya wapokezi wa hadithi kwa mashia na Ahli sunnah, hadithi za shia na Ahli
sunna, Al-fiqhul jadiid, Al-fiqhul muqaarin katika madhehebu za kiislaam, jarida la kifiqhi, na lugha.
Na
mheshimiwa Ayatullah al-udhmaa Shekh faadhil Lankaraniy aliamuru ya kuwa
milango ya maktaba hii ya takhassusi iwe wazi kwa watu wote wenye kufanya
tahkiik na wafanyao utafiti.
Na
maktaba imebeba jukumu la kuandaa vitabu vya rejea kadri ya uwezo wake, sawa
iwe ni ndni ya Jamhuri ya kiislaam ya Iran au nje ya jamhuri kwa
ajili ya kuitumikia elimu na maulamaa na wafanya utafiti.
KITENGO CHA
TANO: KITENGO CHA COMPYUTER
Jukumu
la kitengo hiki, pamoja na kuandaa maalumaati (elimu) ya lazima kwa ajili ya
wafanyao tahkiki, pia kinajukumu la kuandika na kuvitoa vitabu kwa njia ya
kifani, kitengo hiki kinahifadhi maalumati yote na maandishi yote kwenye (cd)
ili yabakie kwa ajili ya wale watakao taka kufaidika nayo na kwa ajili ya
kizazi kijacho.
KITENGO CHA SITA: KITENGO CHA SAUTI NA PICHA
Katika
kitengo hiki huhifadhiwa kanda zote za
audio na vidio za masomo ya mheshimiwa Shekhe muasisi, ili waweze kufaidika
nazo wafanya bahthi na wanafunzi na kila mwenye kutaka kufaidika nazo….. Na mheshimiwa Shekh anacho kituo kwenye
internet chenye vitabu vyote vilivyo andikwa na shekh na kituo hiki hupokea maswali na istiftaa ati kupitia kituo
hiki na majibu yake huwekwa kwenye kituo hiki.
[1]- Marjiu : ni mwanachuoni ambae amefikia
daraja fulani ya kielimu ijulikanayo kwa jina la IJITIHADI , inawezekana
mwachuoni akafikia daraja hiyo lakini bado asiwe MARJIU kwa
sababu neno MARJIU maana yake ni (mwenye kurejewa katika mambo
yanayohusiana na dini) kwa hiyo ili watu waweze kumrejea mwanazuoni katika
mambo yao ya kidini ni lazima awe ameandika kitabu kinachofafanua mambo hayo na
kitabu hicho hua kinaiitwa RISAALTUL-A’MALIYYAH, kwa hio kila
mwanachuoni aliyefikia daraja ya IJITIHADI akawa hajaandika kitabu hicho hua anaitwa MUJTAHID
na siyo MARJIU.
[2] RIJALI : ni elimu
ambayo inafanya kazi ya kuwasoma wapokezi wa hadithi, au kwa kauli nyengine
tutasema kuwa elimu hii inafanya kazi ya kukupa wewe mtizamo mzima wa maisha ya
wapokezi wa hadithi.
[3] MUKALLAF:ni mtu aliyefikia umri wa balegh
na akawa hajitoshelezi kielimu katika masuala yanayohusiana
na ibada au dini kwa ujumla bali akawa anamhitajia mwanazuoni fulani ili
amfuate.
|