Home Page
Maisha Ya Shekh
Vitabu Vyake
Hukumu Na Fat’wa
Wito na fikra za shekh
Vitabu Vya Mwanae
Maktaba Ya Kituo
Picha
Wasiliana Nasi


Affiliate Websites
Affiliate Websites

   E-Mail Listing:


 

FAT’WA ZENYE KUTOSHELEZA

MASWALI  NA  MAJIBU

KWA MUJIBU WA FAT’WA ZA KIONGOZI WA JUU WA KIDINI AYATULLAHIL UDHMAA SHEKH FAADHIL LANKARANIY

TAQLIID

  IJTIHAAD, TAQLIID, IHTIYAAT

SWALI 1: Katika risaalatul amaliayya mmesema ya kwamba: Haijuzu kufanya Taqliid katika usulud- dini) ( yaani katika misingi ya dini) je ni wajibu kulithibitisha hilo kwa dalili, au inatosha tu kuitakidi hivyo?

JAWABU: Inatosha kuitakidi hivyo kwa njia yoyote ile itakayo weza kuthibitisha hivyo.

SWALI 2: Je yawezekana kwa mtu asie kuwa mujtahid kufanya matendo yake kwa kutumia ihtiyaati na kuto fanya taqliid?

JAWABU: Kuna tofauti kati ya maulamaa katika suala la kujuzu kufanya matendo kwa mujibu wa ihtiyaat, kwa hivyo basi ni juu ya mwenye kutaka kufanya ihtiyaat awe ni mujtahidi au ni muqallid kwenye msingi wa kujuzisha kufanya amali kwa mujibu wa ihtiyaat au laa.

SWALI 3: Nini maana na makusudio ya ihtiyaat? Na ni nani ambae anaweza kufanya matendo yake kwa kutumia ihtiyaat?

JAWABU: Ihtiyaat ni mukallaf kufanya matendo akiwa na yakini ya kuwa ametekeleza jukumu alilo nalo la kisheria. Kwa hivyo basi mwenye kutaka kufanya amali kwa kutumia ihtiyaat katika mas’ala yoyote ni lazima awe ni Mujtahidi au karibu kufikia ijtihadi ili aweze kupambanua ni mas’ala gani yanapaswa kufanywa na yanayo wafikiana na ihtiyaat kati ya fat’wa za wanazuoni wa Fiqhi walio tangulia na waliopo kwa hivi sasa.

KUMFUATA ALIE KUWA AALAM ( MJUZI ZAIDI)

SWALI 4: Je kuwa Aalam (mjuzi zaidi) ni sharti kwa marjiu wa Taqliid (anae paswa kufuatwa)?

JAWABU: Ndio, ni wajibu kumfuata na kufanya taqliidi ya Aalam (mjuzi zaidi).

SWALI 5:Ikiwa haikuwezekana kujifunza fat’wa za Mujtahidi alie Aalam katika mas’ala Fulani, je inawezekana kurejea kwenye mas’ala hayo kwa Mujtahidi asie kuwa Aalam?

JAWABU: Ikiwa kutakuwa na udhuru na ikashindikana kuipata fat’wa ya Mujtahidi alie Aalam, italazimika kufanya amali kwa mujibu wa ihtiyaat.

SWALI 6:Ikiwa itashindikana kumuainishaalie Aalam kati ya Mamujtahidi, jukumu la mukallaf ni lipi?

JAWABU: Ikiwa atakuwa na ihtimali ya kuwa mmoja wapo ni Aalam- kama ambavyo akielewa ya kuwa Mamujtahidi wawili hawa wako sawa kielimu, au mujtahidi Fulani ni Aalam- ni wajibu kumfuata na kufanya taqliid yake.

SWALI 7: Ikiwa ushahidi wa ahlil khibra utapingana  katika kumbainisha na kumuainisha faqihi na mujtahidi alie Aalam kati ya mafaqihi, mukallaf atafanya nini katika mas’ala haya?

JAWABU: Ikiwa mmoja wao maalum inadhaniwa na kuna ihtimali ya kuwa ni Aaalam ni wajibu kumfuata huyo, laa sivyo itajuzu kumfuata yeyote amtakae kati yao, ndio lau kama mmoja wao ni mcha Mungu zaidi au ni muadilifu zaidi kauli ya ahwat ya wajibu ni kuwa atachaguliwa huyo na kufanyiwa taqliid.

SWALI 8: Je ni wajibu kumfuata Aalam? Na kama ni wajibu, je ujuzi unao takiwa kuwa nao una angaliwa ujuzi wa kifiqhi pekee au ni sharti awe ni mwenye kuelewa mambo yahusianayo na zama zake anazo ishi?

JAWABU: Kumfuata au kufanya taqliidi ya Aalam ni wajibu, na makusudio ya ujuzi ni kuwa awe ni mwenye maarifa mengine au ujuzi mwingine na mwenye uwezo kuliko mwingine katika kufanya istimbati (uchambuzi na utungaji wa sheria) ya hykumu za Mwenyezi Mungu kutoka kwenye vyanzo vyake vizingatiwavyo.

SWALI 9: Mwenye kumfuata Mujtahidi na akafanya matendo yake kwa mujibu wa fat’wa zake, kasha ikabainika baada ya muda ya kuwa kunamwingine alie kuwa ni mjuzi zaidi, je matendo yake yaliyo tangulia yatahesabiwa kuwa ni sahihi au laa?

JAWABU: Ikiwa katika taqliidi yake ya kwanza alitekeleza na kuheshimu vipimo vya kisheria, matendo yake yaliyo tangulia yatahukumiwa kuwa ni sahihi.

KUTENGANISHA KATIKA TAQLIID

SWALI 10: Je inasihi kwa mukallaf kufanya taqliid ya Mujtahidi Fulani katika baadhi ya matendo yake, na kumfuata Mujtahidi mwingine katika matendo yake mengine?

JAWABU: Ndio inajuzu ikiwa haikuthibiti ya kuwa mmoja wapo maalum ni Aalam au kukawa na ihtimali ya kuwepo Aalam.

SWALI 11: Je inajuzu kutenganisha taqliidi katika kitendo kimoja au laa? Kwa mfano ikiwa fat’wa mojawapo ya mmoja kati ya Mamujtahidi inasema kuwa ni wajibu kukaa kikao cha mapumziko (kati ya sajda mbili), na kuwa ni sunna kusoma tasbihi nne mara tatu, na fat’wa nyingine ni tofauti na hiyo, na je inawezekana kwa muqallid kufanya matendo kwa mujibu wa sunna inayo sema kuwa ni bora kusoma tasbihi nne mara tatu kwa mujibu wa fat’wa ya Mujitahidi wa kwanza, na katika sunna ya kikao cha mapumziko akafanya kwa mujibu wa fat’wa ya Mujtahidi wa pili?

JAWABU:Hakuna kizuwizi kamwe cha kufanya hivyo.

SWALI 12: Ikiwa mukallaf atakuwa na yakini ya kuwa matendo yake yako sambamba na fat’wa za mmoja wapo kati ya Maraajiut  watukufu wa taqliid alie timiza masharti ya kufanyiwa taqliid, je inatosha yakini hiyo katika kusihi kwa matendo yake au laa?

JAWABU: Ndio inatosha yakini hiyo.

KUHAMA KUTOKA KWA MUJTAHIDI ALIE HAI NA KWENDA KWA MUJTAHIDI MWINGINE ALIE HAI.

SWALI 13: Ikiwa itabainika –baada ya mukallaf kufanya taqliid ya Mujtahidi Fulani- ya kuwa kuna Mujtahidi mwingine alie Aalam na mjuzi zaidi kuliko huyu, je inajuzu kuhamia kwa Mujtahidi alie Aalam?

JAWABU: Inajuzu bali ni lazima kuhamia kwa Mujtahidi alie Aalam.

SWALI 14: Mmopja kati ya wafanyao taqliid ya shekh Araakiy (mungu autukuze utajo wake) –baada ya kufariki Shekh – alifanya taqliidi ya Mujtahidi mwingine bila ya kufanya uchunguzi na tahkiki. Je inawezekana kwa mtu huyu kuhamia kwa Mujtahidi mwingine?

JAWABU: Ikiwa Mujtahidi alie tajwa hakutimiza masharti ya kufanyiwa taqliidi ni wajibu kuhama.

SWALI 15: Ikiwa Mukallaf katika taqliidi yake atajitegemeza kwenye kauli za watu wawili waadilifu, lakini habario za sira zao hazifahamiki, je taqliidi hii itaswihi kwa Mukallaf huyu?

JAWABU: Haiswihi kujitegemeza kwenye ushahidi wa watu wawili hao kwenye mas’ala yaliyo tajwa.

KUBAKIA KWENYE TAQLIIDI YA MUJTAHIDI ALIEKUFA

SWALI 16: Katika maisha ya mheshimiwa Shekh ayatullahi Araakiy (mungu amrehemu) nilikuwa nimeazimia kufanya taqliidi yake, na ninajihesabu ni katika wafuasi wake, isipokuwa ni kwaamba mimi sikujifunza fat’wa zake, na nilikuwa nikifanya matendo yangu kwa mujibu  wa ihtiyaati, sasa ni ipi hukumu ya kubakia kwenye taqliidi yake katika hali kama hii?

JAWABU: Katika suala kama hili ulilo litaja, haijuzu kubakia kwenye taqliidi yake, kwani kumfuata na kufanya taqliidi yake- katika hali kama hii- ni sawa na kufanya taqliidi ya Mujtahidi alie kufa kwa mara ya kwanza.

SWALI 17: Nilikuwa ni mfuasi wa Imam Khomeini (mungu amrehemu), na baada ya kufariki Imam nikarejea kwa Ayatullahi Araakiy (mungu amrehemu) katika mas’ala mengine, je inawezekana kwangu kubakia kwenye fat’wa za Shekh Arakiy kwenye mas’ala hayo?

JAWABU: Ikiwa imethibiti kwenu kuwa Imam ni Aalam, ni wajibu kubakia kwenye taqliidi yake kwenye mas’ala yote.

SWALI 18: Je inajuzu kubakia kwenye taqliidi ya Mujtahidi alie kufa? Na  je inawezekana kuhamia kwa Mujitahidi alie hai au laa?

JAWABU: Inajuzu kubakia kwenye taqliidi ya Mujtahidi alie kufa katika mas’ala yote- hata mas’ala ambayo mukallaf hakuyatumia, na ikiwa Mujtahidi alie kufa ni Aalam kuliko Mujtahidi alie hai, ni wajibu kubakia kwenye taqliidi ya Mujtahidi alie kufa

SWALI 19: Ikiwa Marjiu atakufa, na akawa ni mjuzi zaidi kuliko walio hai, je ni wajibu kwa Mukallaf kubakia kwenye taqliidi yake?

JAWABU: Ndio ni wajibu kubakia kwenye taqliidi yake.

SWALI 20: Mukallaf ambae alibakia kwenye taqliidi ya Imam kwa mujibu wa fat’wa yenu, je inawezekana kwake kurejea kwenu katika baadhi ya mas’ala?

JAWABU: Hakuna kizuwizi ikiwa haikuthibiti kwake ya kuwa Imam ni Aalam.

SWALI 21: Nilikuwa mfuasi wa Imam Khomeini (mungu amrehemu), na baada ya kufariki kwake nikabakia kwenye taqliidi yake kwa kujitegemeza kwenye fat’awa ua Ayatullah Arakiy (Mungu amrehemu) isipokuwa kwenye mas’ala ya nchi kubwa.

Na baada ya kufariki kwa Ayatullah Arakiy nikarejea kwenu katika taqliidi, na hivi sasa kulingana na fat’awa yenu isemayo kuwa ni wajibu kubakia kwenye taqliidi ya Mujtahidi alie kuwa Aalam nimebakia kwenye taqliidi ya Imam (Mungu amrehemu), na wakati huo kuhusu mas’ala ya nchi kubwa nifuate fat’awa ya yupi kati ya Marjiu wawili hawa?

JAWABU: Ikiwa inafahamika kuwa Imam ni Aalam na ujuzi wake umethibiti kwako ni wajibu kubakia kwenye taqliidi yake bila kipingamizi.

SWALI 22: Mtu ambae amebakia kwenye taqliidi ya Imam kwa mujibu wa fat’wa yenu, je inawezekana kwake kurejea kwenu katika baadhi ya mas’ala?

JAWABU: Hakuna kizuwizi ikiwa haikuthibiti kwa Mukallaf kuwa Imam ni Aalam.

SWALI 23: Mimi nilikuwa nikifanya taqliidi ya Imam. Na baada ya kufariki kwake nikamuqallidi Ayatullah Sayyid Gulpaygani, na baada ya kufariki kwake nikafanya taqliidi ya Ayatullah Arakiy, je inajuzu kwangu kubakia kwenye taqliidi yao?

JAWABU: Ikiwa mnaitakidi ya kuwa mmoja wapo kati ya watatu hao walio tajwa ni Aalam, ni wajibu kubakia kwenye taqliidi alie Aalam kati yao, laa sivyo inajuzu kubakia kwenye taqliidi ya Mujtahidi wa mwisho ambae mlihamia kwake, kama ambavyo inajuzu kurejea kwa Mujtahidi alie hai.HUKUMU MBALIMBALI KUHUSIANA NA TAQLIIDI

SWALI 24: Ikiwa matendo yaliyo fanywa na Mukallaf kwa kujitegemeza kwenye fat’wa za mmoja kati ya Mamujtahidi wawili, na matendo hayo yakawa yakipingana na fat’wa za Mujtahidi wake wa kwanza, je ni lazima kwake kuyarudia matendo hayo?

JAWABU: Si lazima kwake kuyarudia.

SWALI 25: Je alie ajiriwa kufanya matendo fulani atafanya matendo yale kwa mujiobu wa fat’wa za Mujtahidi alie wa yule alie muajiri au alie ajiriwa?

JAWABU: Atafanya matendo yale kwa mujibu wa fat’wa za Mujtahidi anae mfuata muajiriwa isipokuwa amuajiri ikiwa ataweka sharti tofauti na hilo.

SWALI 26: Ikiwa mtu atamuuliza mwanazuoni wa dini kuhusu hukumu ya kisheria, je inajuzu kwa mwanazuoni huyo kumtajia muulizaji fat’wa ya Mujtahidi anae mfanyia taqlidi yeye mwenyewe?

JAWABU: Ikiwa anafahamu ya kuwa Marjiu wake na marjiu wa muulizaji ni mmoja, hakuna kizuizi kufanya hivyo, vilevile ikiwa atathibitisha kuwa Maujtahidi anae mfuata ni Aalam. Lakini ikiwa kutakuwa na ihtimali ya usahihi wa taqliidi ya muulizaji, na haikuthibiti  kwake kuwa Marjiu wake ni Aalam, ni wajibu kutaja fat’wa ya Marjiu ambae anafuatwa na muulizaji.

SWALI 27: Ni ipi hukumu ya mtu ambae amekuwa akitekeleza matendo yake ya kisheria tangu kubalee kwake bila ya taqliidi, na yeye kwa hivi sasa ni miongoni mwa wanao kuqallidi wewe mheshimiwa?

JAWABU: Matendo yake yatakuwa sahihi ikiwa yatakuwa sambamba na uhakika wa kisheria, au fat’wa ya Mujtahidi ambae alikuwa ni wajibu kwake kumfuata au kufanya taqliidi yyake wakati akifanya matendo hayo.

SWALI 28: Mtu alie kuwa akimfuata Mujtahidi Fulani, na akabakia kwenye taqliidi yake baada ya kufariki kwake kwa idhini ya Mujtahidi alie hai, sasa haki zake za kisheria atampatia nani?

JAWABU: Ni lazima haki hizo kumpatia Mujtahidi alie hai ambae alirejea kwake katika mas’ala ya kubakia kwenye taqliidi ya Mujtahidi alie kufa.

SWALI 29: Mtoto mkubwa ambae anataka kulipa kadhaa ya sala na swaumu zolizo mpita baba yake, je atazifanya ibada hizo kwa mujibu wa fat’wa za Mujtahidi alie kuwa akifuatwa na baba yake, au kwa mujibu wa fat’wa za Mujtahidi ane muqallidi yeye?

JAWABU: Atafanya kwa mijibu wa fat’wa za Mujtahidi wake.

SWALI 30: Mtu alihukua ujira kwa ajili ya kumlipia ibada mtu Fulani kama sala, swaumu na Hajji, je ni wajibu kwake kutenda ibada hizo kwa Mujibu wa fat’wa za Mujtahidiwake, au kwa mujibu wa fat’wa za Mujtahidi wa anae lipiwa ibada hizo?

JAWABU: Ikiwa katika makubaliano yao hawakuweka sharti ya kuwa afanye kwa mujibu wa fat’wa za Mujtahidi ane  lipiwa, ni wajibu kufanya kwa mujibu wa fat’wa za Mujtahidi ane muqallidi yeye, na bora zaidi- kama kuna uwezekano- kutenda matendo hayo kwa mujibu wa fat’wa za Mamujtahidi wote wawili. 

SWALI 31: Mtu ambae kazi yake na shughuli zake ni kusafiri, na alikuwa akimfuata Imam Khomeini (Mungu amrehemu) na baada ya kufariki kwake akafuata fat’wa za Ayaatul idhaam kama vile (Khoi Gulpaygani na Arakiy) katika suala la kubakia kwenye taqliidi ya Mujtahidi alie kufa, ni lipi jukumu la mtu huyo kwenye sala zake na funga au swaumu wake?

JAWABU: Ikiwa suala la kuwa Imam ndie Aalam litathibiti kwake itakuwa ni wajibu kubakia kwenye taqliidi yake kwa hivyo atapunguza sala kwenye safari yake, laa sivyo inajuzu kwake kurejea kwa Mujtahidi alie hai. Na kauli ya ahwat ya wajibu kwetu kwa mtu ambae kazi yake ni kusafiri  ni kukusanya kati ya matendo mawili kupunguza na kukamilisha, na inajuzu kurejea kwa Mujtahidi mwingine alie hai pamoja na kuzingatia masharti.

SWALI 32: Mukallaf mmoja alitekeleza ibada kwa makusudio ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, lakini ibada hiyo ilikuwa ni batili kwa mujibu wa fat’wa ya marjiu taqliidi wake (yaani anae mfuata), na baada ya kufariki kwake akarejea kwa Mujtahidi alie Aalam baada yake. Sasa ikiwa matendo yake kulingana na fat’wa ya Mujtahidi wa pili ni sahihi, je itakuwa ni wajibu kwake kuzirudia ibada hizo?

JAWABU: Si wajibu kuzirudia.

ALAMA ZA KUWA BAALIGHI (ZA KUBALEE)

SWALI  33: Ni zipi alama za kubalee? na niwakatikgani mmtu anakuwa mukallaf 

JAWABU: Kubalee kwa mwanaume kunathibiti kwa alama tatu zifuatazo:

1-  kuota nywele ngumu kwenye sehemu za siri (kinena) (juu ya sehemu za siri).

2-  Kutokwa kwa manii ; sawa katika usingizi kwa kujiote au akiwa macho.

3- Kukamilisha miaka kumi na tano ya qamaria (chini ya miaka (15) ya shamsia  kwa siku  (163) takriiban.

Na kubalee kwa mwanamke  kunathibiti kwa kupatikana moja wapo kati ya alama zifuatazo:

1-  Kuota kwa nywele ngumu juu ya sehemu za siri (kinena)

2- Kutookwa na manii; sawa awe katika usingizi kwa kujiotea au awe macho kwa kufanya kitendo cha kijinsia.

3- Kukamilisha miaka (9) ya qamaria (chini ya miaka (9) ya shamsia kwa siku 97 takriiban)

SWALI 34: Kijana alie tokwa na manii kabla ya kufikisha umri wa miaka (15) , na kwa sababu ya kutojua hukumu, hakuswali na wala hakufunga. Takliifu yake ya kisheria kuhusiana na ibada katika kipindi hiki ni ipi?

JAWABU: Mwenye kuwa na yakini ya kuwa manii yametoka anakuwa baaaligh (balee)  na mtu mzima (Rashiid), ikiwa atapitwa na sala au swaumu (funga) ni wajibu kwake kulifa ibada zilizo mpita, na ikiwa alikuwa katika mwezi wa ramadhani kwa kuto fahamu hukumu na hakufanya uzembe wowote katika kujifunza hukumu, hakuna kafara juu yake, na kauli ya ahwat ya wajibu ni kuwa atatoa kafara ikiwa kutofahamu huko kumetokana na uzembe wake.

SWALI 35: Zimeonekana alama za kubalee kwa motto alie fikia umri wa miaka (6) kama kuota nywele ngumu sehemu zasiri na kwapani, na kuwa na sauti nzito, kama ambavyo zimeonekana alama za janaba katika baadhi ya nyakati katika nguo zake, je ni wajibu kwake kusali na kufunga na kufanya mambo ya faradhi kama mukallafina wengine?

JAWABU: Pamoja na alama zilizo tajwa ikiwa ni mumayyizi (mwenye kupambanua mambo) ulio sawa na kubalee kwake basi huyo amekwoisha balee na ni mukallaf.

TWAHARA NA NAJISI
VITU VINAVYO TWAHIRISHA:

SWALI 36: Maji ya mabomba  mijini na vijijini wakati mwingine huwa meupe kwa sababu ya kuwekewa dawa ya Alkoliy, je katika hali kama hii maji haya yanakuwa ni maji mudhaafu au laa? na ni  ipi hukumu ya kutawadha na kutwahirisha vitu kwa maji haya tuliyo yataja?

JAWABU: Ikiwa itithibiti kuitwa kwa jina la amji bila kudhifiia kitu (yaani yakiwa ni mutlaq), katika hali hiyo hayatakuwa na hukumu ya maji ya mudhaafu, kwa hivyo itaswihi kuyatumia kutawadhia na kutwahirishia vitu, vilevile ikiwa kutakuwa na shaka ya kuwa maji hayo yamekuwa mudhafu au laa, yatahukumiwa kuwa ni maji mutlaq.

SWALI 37: Je kitu kilicho najisika kinatwahirika kwa miali ya jua kupitia nyuma ya kioo? na ni ipi hukumu ya kioo ikiwa ni najisi?

JAWABU: Kauli iliyo dhahiri nikuwa kioo kisiwe ni chenye kuzuwia  ikiwa ni safi, na kioo kitatwahirika kwa miali hiyo lakini kwa kuzingatia masharti katiukka kutwahirisha kwa jua.

SWALI 38: Je chini ya unyayo na chini ya kiatu kunatwahirika kwa kutembea juu ya ardhi iliyo tandikwa  ( muzaiiki au tazfiit)?

JAWABU: Dhahiri ni kuwa vina twahirika kwa kutembeea juu ya ardhi  iliyo tandikwa juu yake kwa (muzaiik), lakini jambo hilo hutiwa ishkaali ikiwa atatembea juu ya (tazfiit), isipokuwa ikiwa juu ya (tazfiityi) kuna mchanga, au kukawa na rami iliyo chimbuliwa kiasi kwamba changarawe hugusa chini ya kiatu chamwenye kutembea juu yake.

SWALI 39: Je (tinnar) ( mada itumikayo kuondolea rangi na uchafu) nayo inakuwa ni miongoni mw vitu vitwahirishavyo.

JAWABU: Nitar na mfano wa hiyo haviwi ni miongoni mwa vitu vinavyo twahirisha, na kwamba vitu mutwahirati ni vitu vilivyo tajwa kwenye kitabu chetu cha hukumu za kisheria (Risalatul amaliyah).

NAMNA YA KUTWAHIRISHA VITU VILIVYO NAJISIKA

SWALI 40: Je inawezekana kuzitwahirisha nguo zilizo najisi baada ya kuondoa najisi yenyewe kwenye nguo hiyo? kwa mfano kuziweka nguo kwenye chombo ambacho kina kiasi kidogo cha maji, lakini chombo hicho kimeungana na kuri kwa njia bomba la maji.

JAWABU: Ndio nguo zinatwahirika, lakini kauli ya ahwarti ni kuwa itabidi nguo hizo zikamuliwe  mpaka maji hayo yatoke kwenye nguo hizo.

SWALI 41: Ikiwa ardhi iliyo tandikwa kwa mawe au marumar  itanajisika, je inatwahirika kwa kumwagilia maji ya bomba juu yake, na kuondoa najisi yenyewe, au inalazimu kuondoa pia maji yaliyo tumiwa kuosha ardhi hiyo?

JAWABU: Ikiwa momba limeungana na maji ya kuri au maji yenye kutiririka, na mji hayo yakaenea sehemu yote iliyo najisika basi ardhi hiyo itatwahirika, na si sharti  kuondoa maji yaliyotumika kuoshea.

SWALI 42: Je ni shaarti katika kuyatwahirisha maji yaliyo najisika  kuchanganyika na maji ya kuri au maji ya mvua?

JAWABU: Kauli ya ahwat ni kuzingatia kuchanganyika maji hayo.

SWALI 43: Ni ipi njia ya kutwahirisha zulia lililo najisika na ambalo limeshikamana na  kugandia juu ya ardhi?

JAWABU: Lina twahirika ikiwa itaondolewa najisi yenyewe, na likamwagiwa maji ya kuri au yenye kutiririka  na kuingia maji hayo ndani ya zulia hilo, na kauli ya ahwat ya wajibu  ni kulikamua mpaka maji yaliyoko ndani yatoke.

SWALI 44: Mashine za kufulia nguo ambazo huosha na kukamua nguo, je zinatwahirisha nguo pamoja na kuwa wakati mwingine  hukatia maji  kisha kuingiza maji mengine?

JAWABU: Kama wasemavyo wataalamu wa mambo hayo: Maji yanapo kuwa yameungana na kuri, huenea kwenye nguo zote zilizo najisi, kwa hivyo basi ikiwa maji hayo yata zienea nguo zote mara tatu, kisha mashine katika kila mara ikatoa maji  nguo hizo zitatwahirika, ikiwa haikubakia najisi yenyewe kwenye nguo. 

SWALI 45: Je inawezekana kuitwahirisha najisi  iliyoko kwenye unga, unga ulio kandwa an maziwa?

JAWABU: Vitu vitatu hivi havikubali  kubali kutwahitishwa.

SWALI 46: Je Mswala na chombo vilivyo najisika vinatwahirika kwa kunyeshewa mvua?

JAWABU: Vitu hivi vinatwahirika ikiwa havikubakiwa na najisi yenyewe, na si lazima kuukamua mswala kwa ajili ya kutoa maji yaliyo oshewa.

SWALI 47: Ikiwa ngozi ya mbuzi itawekwa kwenye maji ya chumvi,  hali ya kuwa kafia panya kwenye maji hayo, itatwahirishwa vipi ngozi hiyo?

JAWABU: ikiwa itafahamika ya kuwa umaji maji umeingia hadi ndani ya ngozi hiyo, haiwezekani kuitwahirisha ndani yake, na juu yake kutatwahirika kwa kuimwagia maji.

SWALI 48: Ikiwa maji kiasi chake ni sawa na bomba dogo kama bomba la samaawar, je itathibiti kuwa yameungana naji hayo na mada au laa?

JAWABU:Ndio itathibiti kuwa yameungana na mada.

SWALI 49: Ikiwa maji mudhaaf yatanajisika au maji mengine kama juisi ya tende je inawezekana kuyatwhirisha?

JAWABU: Hapana, isipokuwa ikiwa yatamiminwa kwenye maji ya kuri au yakaungana na maji ya bomba, na yakachanganyika hadi kutoweka athari yake, na wakati huo huitwa maji mutlaq, katika hali kama hii yatakuwa twahara na hakuna shaka kuyanywa.

SWALI 50:  Ikiwa mchele , ngano, (almashi) na sabuni vitanajisika je inawezekana kuvitwahirisha vitu hivi?

JAWABU: Ndio vinatwahirishwa – kama vitu vingine- ikiwa vitanajisika juu yake. Ama ndani yake ikiwa kutanajisika kwa kufikiwa na umaji maji wenye kutiririka ulio najisi haiwezekani kuitwahirisha.

SWALI 51: Je nguo iliyo najisika ikiwekwa kwenye chombo chenye maji kidogo inatwahirika, lakini kwa kuzingatia kuwa imeungana na kuri?

JAWABU:Ndio inatwahirika.

SWALI 52: Nina meno ya bandia, na imetoka damu kinywani mwangu, kasha ikakatika na kuondoka athari zake, je maeno yangu hayo yatatwahirika?

JAWABU: Hukumu ya kutwahirika haiku mbali ( yaani yatahukumiwa kuwa ni twahara)  ikiwa yamegusana na najisi ndani yam domo kama swali  lisemavyo.

SWALI 53: Mimi nime ng’oa meno na mdomo wangu ukanajisika kwa damu ya ufizi, je sehemu iliyo ng’olewa  itatwahirika ikiwa damu itatoweka?

Jawabu:Ndio sehemu hiyo inahukumiwa kuwa ni twahara.

SWALI 54: Mtu asie weza kustanji kwa maji jukumu lake ni nini?

JAWABU: Si lazima  sehemu ya haja kubwa kuitwahirisha kwa maji, bali inajuzu kuitwahirisha kwa mawe na tishu, lakini sehemu ya kutokea haja ndogo inatwahirika tu kwa kutumia maji.

SWALI 55: Mgonjwa asie wezekana kutwahirishwa kwa mfano ( alie katika  nukhaau shawkiiy) nilipi jukumu lake kuhusia na sala?

JAWABU: Niwajibu kwake kuona kama inawezekana, na mwanamke atachukua jukumu la kumtwahirisha mumewe, laa sivyo jukumu la kujitwahirisha lita anguka.

NAJISI

SWALI 56: Ardhi iliyo najisika, na tumeweka juu yake blanketi, na blanketi hilo likaingiwa na unyevu nyevu wa sehemu hiyo na kufyonza umaji maji huo na likawa zito, je litahukumiwa kuwa limenajisika?

JAWABU:Ikiwa itafahamika ya kuwa umaji maji wenye kutiririka umeingia kwenye blanketi hilo  litahukumiwa kuwa ni najisi, laa sivyo litahukumiwa kuwa ni twahara.

SWALI 57: Unyevu nyevu imefikia kiasi cha mita moja katika ukuta wa  (  Al-mirhaadh), je ukuta huu unakuwa najisi au laa?

JAWABU: Ukuta huo haunajisiki, isipokuwa ikiwa itafahamika kuwa unyevu nyevu huo wenye kutiririka umefika kwenye ukuta huo.

SWALI 58: Je mvuke wa mkojo au  mvuke wa maji yaliyo najisika unakuwa najisi?

JAWABU: Mvuke ni twahara vyovyote uwavyo (mutlaq).

SWALI 59: Je moshi wa mafuta ya taa au dizeli ni najisi, au moshi wa ubao au mti na vitu vingine vilivyo najisika ni twahara ?

JAWABU : Ndio,  nitwahara.

SWALI 60 : Ni vitu vingapi vilivyo najisika ambavyo vikikutana na vitu twahara huvinajisisha ?

JAWABU : Kitu kilicho najisika kinakinajisisha kitu kingine kilicho twahara ikiwa ni kimoja au viwili, ama zaidi ya vituviwili kunajisisha kwake kumesimama kwenye msingi wa ihtiyaat.

SWALI 61 : Je inajuzu kwa mtu kukata ngozi yake amabayo ilikuwa mbioni kukatika na kutoka kwenye sehemu ya ngozi yake ambayo haiko mbioni kutengana na mwili wake ?

JAWABU : Inajuzu, lakini sehemu ambayo haikuw mbioni kutengana na mwili wake itahukumiwa kuwa ni najisi.

SWALI 62 : Je mbwa wa kuwinda au mbwa wa kuchungia ni najjisi kama mbwa wengine ?

JAWABU : Hakunatofauti kati ya mbwa katika suala la unajisi wake.

SWALI 63 : Je yai la kuku alie kula kinyesi na nyama yake vinakuwa najisi ?

JAWABU : Vitu hivyo si najisi, lakini niharamu kuvila.

SWALI 64 : Maziwa yanapo kamuliwa juu yake hukusanyika povu, ikiwa tone la damu iliyo kavu litadondokea kwenye povu hili, je maziwa yatanajisika ?

JAWABU :Ndio yana najisika, isipokuwa damu hiyo itatolewa pamoja na povu  lililo zunguuka au lililo juu yamaziwa hayo  kiasi kwamba haligusni na maziw hayo.

SWALI 65 : Je damu ya wanyama walio halali kuliwa ni najisi ?

JAWABU : Ndio, ni najisi ikiwa mnyama huyo ni mwenye mishipa itoayo damu kwa kuchupa pindi anapo chinjwa, lakini ikiwa damu hiyo ni ndogo zaidi kuliko kiwango cha dirham hakuna kizuizi kusalia nguo yenye kiwango hicho.

SWALI 66 : Ni ipi hukumu ya damu iliyoko kwenye yai la kuku ?

JAWABU : Ni twahara, lakini ni haramu kuila.

SWALI 67 : Je damu iliyoko kwenye maziwa ni najisi, na je maziwa yananajisika kwa damu hiyo ?

JAWABU :Ikiwa itathibiti kuwa damu iko kwenye mazi hayo, basi maziwa hayo ni najisi.

SWALI 68 : Je alkoli ya njano na nyeupa ni najisi ?

JAWABU : Alkoli inayo tengenezwa ( spirti) na Alkol itumiwayo katika matibabu na wakati wa kuchoma sindano na mfano wa hayo si najisi.

SWALI 69 : Je vyakula na vinywaji- kama siki ambayo hutengenezwa kwa kawaida ikiwa na kiwango cha  asilimia 2% au 3% ya Alkoli, je ni najisi au laa ?

JAWABU:  Kiwango hiki cha Alkoli – ambacho hudhihiri katika hali ya utafiti na uchambuzi wa kitaalam, na kiwango hicho kikiwemo kwa kawaida – vyakula hivyo si najisi wala sio haramu.

SWALI 70 : Je maji yatokayo kwenye mfuko w uzazi wakati wa kuzaa yanahukumiwa kuwa ni najisi, na ni vema kusema kuwa mfuko huo wa uzazi wakati mwingine kutoboka na kuchanika kabla ya kuzaliwa mtoto, na maji hayo kutoka kupitia sehemu za siri za mwanamke ?

JAWABU: Maji hayo ni twahara.

SWALI 71 : Je kugusana na maji ya mwili wa maiti- kabla maiti huyo haja poa, au baada ya kupoa- je yanasababisha kunajisika alie gus maji hayo au laa ?

JAWABU : Katika hali zote mbili hizo ikiwa umaji maji huo ni wenye kuhamia kwenye sehemu nyingine unakuwa ni wenye kusababisha najisi.

SWALI 72 : Gamba ambalo hutokea juu ya jeraha, na kwa kawida hutokana na damu na unyevu nyevu au umaji maji utokao kwenye jeraha, je gambvala hilo huhukumiwa kuwa ni najisi ?

JAWABU : Ikwa kwa kawaida huonekana  kuwa ni katika sehemu ya ngozi na haikuhesabika kuwa ni damu kwa kawaida basi haitahukumiwa kuwa ni najisi.

SWALI  73 : Ni ipi hukumu ya kuchukua baadhi ya viungo vya mnyama ambae ni najisul aini kama mbwa na kafiri na kuviweka kwenye mwili wa mtu ambae ni muislaam ?

JAWABU : Hukumu yake baada ya kuingiwa na roho ni sawa na hukumu ya mwili wa mtu alie muislaam.

SWALI 74 :  Je ( balaasima wal amswaal ) vitolewavyo kwenye damu kwa kufanya uchambuzi wa kitafiti ni najisi ?

JAWABU : Haithibiti juu ya vitu hivi wakati wa utafiti na uchambuzi kuwa ni damu kwa kawaida, na vitu hivyo kidhati yake ni twahara kwa sababu ya kubadilika kwake na kuwa vitu vingine, ndio ikiwa vitakusanyika kwenye chombo kilicho najisika pamoja na damu au kwenye chombo kilicho  kingine kilicho najisika hunajisika vitu hivyo kwa chombo hicho.

SWALI 75 : Ni ipi hukumu ya mkojo wa popo na kinyesi chake ? je popo ni ndege ?

JAWABU: Kutokana na kauli ya dhahiri ni kuwa popo ni katika jamii ya ndege na hukumu yake ni hukumu ya ndege kuhusioana na mkojo na kinyesi chake. Kwani kauli yenye nguvu zaidi inasema kuwa kinyesi na mkojo  ni twahara hata wa ndege ambao hi haramu kulia.

Amesema Amiirul muuminiin (a.s) mwishoni mwa khutba ya 155 katika Nahjul balagha,  kuihusiana na maajabu ya uumbaji wa popo : Na mwenyezi mungu akawawekea ( Mapopo) mbawa zitokanazo na nyama zao, hupaa kwa mbawa hizo wakati wa haja ya kupaa.. anazo mbawa mbili…. Hupaa huku mwanae akiwa amemgandia… nk.

Na katika  Majmaul bahrayni  amesema : Popo ni kama koma manga ni mwenye kupaa usiku.

Katika kitabu Al-urwatul wuthqaa  amesema katika kuelezea najisi : Kauli yenye nguvu ni kuwa wanyama walipo haramishwa si najisi ( yaani kinyesi na mkojo wao si najisi) lakini kauli ya ahwat ni kujiepusha na vitu hivyo, hasa popo na hasa mkojo wake. Ndio, imepokelew riwaya iliyo kuwa Mursalah ( katika kitabul Wasaail mlango wa 10 katika ya milango ya najisi juzu 4) katika hriwaya hii imeamrishwa kuosha nguo kutokana na mkojo wa mapopo, kwa sababu hiyo waktoa fatwa ya kuwa ni bora kujiepusha na kinyesi chake na mkojo wake, kwa. kuyazingatia haya imedaiwa kuwa amefanyiwa popo majaribio, akakutwa ya kuwa si mwenye mishipa itoayo damu kwa kuchupa, na juu ya msingi huu suala hili linakuwa ni jepesi zaidi kuliko yaliyo tangulia.

UNAJISI WA KAFIRI

SWALI 76 :Kwanini wasio waislaam wanahukumiwa kuwa ni najisi pamoja na kuwa usafi wao ni mzuri sana kama tuonavyo ?

JAWABU : Kauli yenye nguvu kwangu ni kuwa Ahlul kitabu (wenye kitabu kitokacho mbinguni) yaani mayahudi na wakristo na majusi wao ni twahara, ama makafiri wasio kuwa na kitabu wao nimnajisi, na kuhukumiwa kwao hivyo ni kutokana na hekima na maslaha, kati ya hekima na maslaha hayo ni : Kuto changanyika kwao na waislaam, ili waislaam wasiathirike na tabia zao na mienendo yao, na ili wajihisi udghalili na unyonge mbele ya waislaam, huenda kwa kufanya hivyo wakazindukana na kurudi kwenye njia ya sawa nayo ni njia ya kumuamini mwenyezi mungu. Na  maslahi mengineyo yaliyo thibitishwa kwenye hukumu za kiislaam. 

SWALI 77 : Je inajuzu kula chakula cha Ahlil kitaab (walio pewa kitabu) kama mayahudi na wakristo ?

JAWABU :  Kwa mtazamo wangu ni kuwa Ahlil kitaab ni twahara, kwa msingi huu chakula chao ni twahara, isipokuwa ikiwa ni nyama iliyo najisi au chakula kimenajisika kwa sababu ya pombe na vinginevyo, lakini anaesema kuwa ahlili kitabu ni najisi, anahukumu kuwa chakula chao ni najisi ikiwa atafahamu ya kuwa wamekigusa chakulahicho kwa umaji maji wenye kuhama.

SWALI 78 : Je majusi ni katika Ahlil kitaabu (walio pewa kitabu) ?

JAWABU :Inavyo dhihiri ni kuwa ni katika Ahlul kitabu.

SWALI 79 : Mimi nilikuwa nikifanya taqliidi ya Imam Khomeiniy (mwenyezi mungu amrehemu) na baada ya kufariki nakabakia kwenye taqliidi yake kwa ruhusa yako mheshimiwa, na nimesikia ya kuwa nyinyi mnasema ya kuwa ahlil kitaab ni twahara, je inawezekana nikakufuateni nyinyi katika mas’ala haya, ukifahamu ya kuwa mimi nina maingiliano na mahisiano sana na watu hawa ?

JAWABU : Hakunba kizuizi kufanya hivyo, ikiwa haikuthibiti kwako kuwa Imam Khomeiniy ni mjuzi zaidi.

SWALI 80 : Je kikundi kiitwacho ( Al-aliyyul ilaahiyyah) kinahukumiwa kuwa ni twahara ? na ni ipi hukumu ya kuoa kwao, na ni ipi hukumu ya kuchanganyika nao na kula nao ?

JAWABU : Ikiwa wanaitakidi ya kuwa Amiirul muuminiin (a.s)- mwenyezi mungu atukinge na hilo- ni mungu, au wanapinga kuwepo kwa marejeo ( kiama) au moja kati ya mambo ya dharura na ya lazima katika dini kama sala  na funga, kiasi kwamba wanarejea katika kupinga upweke wa mwenyezi mungu  an ujumbe wake, watahukumiwa kuwa ni makafiri na kuwa ni najisi, na haijuzu kuoa kwao na kuchanganyika naona kula pamja nao, kwa sababu wao ikiwa watagusa vitu kwa mkono wenye umaji maji vitu hivyo vina najisika, ikiwa hawako kama vulivyo eleza basi wao ni waislaam na twahara, kwa hivyo inajuzu kuoa kwao na kuchanganyika nao na kula pamoja nao.

SWALI 81 : Mtu alikuwa kwenye hali  ya ghadhabu ( Amechukia) -mwenyezi mungu atukinge na hali hiyo- akamtukana mwenyezi mungu na Mtume (s.a.w) kisha  baadae akajuta kwa tendo lake, je kutukana huku na kutusi huku kunasababisha mtu kuritadi na kuwa najisi ?

JAWABU :Ikiwa ghadhabu yake imefikia kiwango cha kumtoa kwenye hali ya hiari hawi murtadi wala najisi. na ikiwa haikufikia kiwango hicho hapo kuna utata, na niwajibu kwake kutubia.

SWALI 82 : Je makundi mengine kama Suufiyah na Darwiish na hata Shaykhiyyah pamoja na kufanya kwao mambo ya bidaa (uzushi) ni twahara ?

JAWABU : Wanahukumiwa kuwa ni twahara, nabora zaidi kuto ingiliana nao sana.

SWALI 83 : Je mkono wa muislaa wenye maji maji una najisika  ukigusa milango au kuta au vitu vitumiwavyo na Hindosi (Baniani) ?

JAWABU : Inahukumiwa kuwa ni twaharaikiwa haikufahamika kuwa wamegusana na sehemu hizo au vitu hivyo wakiwa na umajimaji wenye kuhama.

SWALI 74 : Ni lipi jukumu la walimu wa kiislaam ambao huwafundisha wnafunzi wa madhehebu ya Bahai, je inajuzu kuwapa Qur ani tukufu ?

JAWABU :Wanahukumiwa kuwa ni najisi, ni wjibu kujiepusha nakitu walicho kigusa wakiwa na umajimaji wenye kuhama na haijuzu  kuwapa Qur ani tukufu isipokuwa ikiwa atafahamu ya kuwa haotavunjiwa heshima yake wala haita najisiwa.

SWALI 85 : Mtu ambae ameacha sala kwa makusudi, lakini hapingi sala yenyewe, je anahesabiwa kuwa ni kafiri au najisi ?

JAWABU : Mtu huyu ambae ahipingi wala kuikataa  uwajibu wa sala ni faasiki na mwenye madhambi, na hahukiumiwa kuwa ni kafiri wala najisi.

SWALI 86 : Je muislaa anakuwa ni murtadi (alie toka kwenye dini) ikwa ataitukana Qur’ani (mwenyezi mugnu atukinge na hilo) ? na ni ipi takliifu ya wale mabao wanamshuhudia akifanya hivi na iakiwa  katika hali kama hii kwa mara kadhaa ?

JAWABU : Ikiwa kuitukana kwake kumetokana na ghadhabu iliyo vuka kiwango cha kawaida, ni wajibu kwake kutubia. Ama ikiwa kutukana kwake kumetokana na uadui na chuki binfsi kwa Mtume (s.a.w) na maimau (a,s) mtu huyo anahukumiwa kuwa ni najisi, na ikiwa kutukana kwake kutapalekea kukataa ujumbe wa mwenyezi mungu basi anahukumiwa kuwa ameritadi na kuwa ni najisi, alaa ayi hali hukumu ya wtu ambao wanafahamu elimu ya mtu huyu, ni kukataza maovu, na kujiepusha nae, mpaka haakimusharii atoe hukumu yake kuhusiana na mtu huyu

SWALI 87 : Je anae itakidi maimamu sita kati ya maimamu watwahirifu (a.s) ni muslaam ?

JAWABU : Ndio ni muislaam.

SWALI 88 : Mtu ambae hatoi Khumsi wala Zaka na wakati mwingine huzichezea shele na kuzidhihaki, bali haitakidi utoaji wa Khumsi wala Zaka, je matendo yake na ibada zake ni batili ? na je anahukumiwa kuwa ni najisi na ni wajibu kujitenga nae ?

JAWABU : Haijuzu kuitumia mali yake ambayo inajulikana kuw ndani yake kuna fungu la khumsi au Zaka, lakini ibada zake ambazo hazihusiani na mas’ala haya ni sahihi, ikiwa kupinga kwake Khumsi na Zaka hakuta rejea kwenye upingaji wa uungu au upweke wa mwenyezi mungu au ujumbe wa mwenyezi mungu, kiasi kwamba akavipinga vitu hivyo pamoja na kufhamu ya kuwa ni faradhi au vitu vilivyomo ndani ya uislaam.

MAS’ALA MENGINE YAHUSIANAYO NA NAJISI NA TWAHARA

SWALI 89: Je sosege ziletwazo nchini kutoka kwenye nchi za kikafiri ni twahara?

JAWABU: Ikiwa zimechanganywa na vitu vya wanyama walio haramu kuliwa, au wanyama walio chinjwa kwa njia isiyo kuwa ya kisheria ya kiislaam basi ni haramu.

SWALI 90: Ni ipihukumu ya samaki wa makopo na maruta yaletwayo kutoka nchi zingine, je ni twahara na ni ipi hukumu ya kula samaki hao?

JAWABU: Ikiwa itathibiti ya kuwa samaki hao wamekufa kwa kuvulia ima wamefia nje ya maji au kwenye mtego watahukumiwa kuwa ni twaharana kwamba ni halili kuwala, lakini halithibiti hilo kwa kutoa ushahidi kafiri peke yake.

SWALI 91: Je mabaki ya chakula ya paka ni najisi?

JAWABU : Si najisi.

SWALI 92 : Je madawa yauzwayo na kununuliwa kwenye masoko ya waislaam yanahukumiwa kuwa ni twahara, wakati yametengenezwa kwenye nchi za makafiri ?

JAWABU : Madawa hayo yanahukumiwa kuwa ni twahara.

SWALI 93 : Ni ipi hukumu ya vitu mbali mbali viletwavyo kutoka kwenye nchi za kikafiri kama viatu na majaketi, ambavyo katika kutengenezwa kwake zimetumika ngozi za wanyama ?

JAWABU : Ikiwa kutakuwa na ihtimali ya kuwa ngozi hiyo ni ya wanyama walio chinjwa kisheria vitu hivyo vitahukumiwa kuwa ni twahara, lakini hajuzu kuvitumia kwenye sala isipokuwa ikiwa vitanunuliwa kwenye mikono ya muislaam na kukawa na ihtimali ya kuwa amethibitisha kuchinjwa kwake kisheria.

SWALI 94 : Ni ipi hukumu ya kufuga na kurefusha nywele za sehemu za siri ( yaani nywele za kwenye kinena) na nywele za kwapani ?

JAWABU :Si wajibu kuziondoa au kuzikata, bali inawajibika kuangalia zisiwe ni kizuizi cha cha kutwahirisha mahala hapo au ni kizuizi cha kuoga n kufika maji mahali hapo.

SWALI 95 : Ni ipi hukumu ya kula samaki ambao kwenye ngozi yake kuna vitu vinavyo fanana na magamba madogo, na kuna shaka ya kuwa ni magamba au laa ?

JAWABU :Ikiwa mashahidi wawili watashuhudia ya kuwa  samaki huyo  anamagamba itakuwa ni hali kuliwa, bali kauli ya dhahiri ni inajuzu kumla pamoja na kuwepo shaka.

SWALI 96 : Ikiwa pesa ya sarafu iliyo andikwa juu yake jina la Imam alie maasuum (a.s) ita angukia chooni, na hakuna choo kingine katika nyumba, na kuitoa sarafu hiyo inahitajia kutumia mali nyingi na hakuna uwezo wa kuzipata pesa hizo,je itajuzu kukitumia choo hicho?

Jawabu :Inajuzu kukitumia katika mahgala pa  swali hili pekee.

SWALI 97 : Ni ipi hukumu ya mtu mwenye wasiwasi sana kuhusiana na twahara na najisi ? na je kuwa na wasiwasi mwingi kunatatizo la kisheria ?

JAWABU : Kwa uhakika wasiwasi mwingi ni sawa na kuto kubali hukumu za mwenyezi mungu na Mtume wake katika sehemu za utwaharifuwa vitu, na wakati mwingine wasiwasi husababisha kubatilika kwa udhu, kwa hivyo basi kisheria na kiakili inamlazimu mukallaf au mwenye tatizo kama hili kujiepusha na fikra hizi za kishetani, na kuto zitilia umuhimu au kuto zijali indivyo unaweza kuishinda na kuighilibu hali hiiya kinafsi.

SWALI 98 :Ni ipi hukumu ya mafuta uzuri au pafyum ziletwazo kutoka kwenye nchi za zisizo za kiislaam, na hatufahamu ya kuwa ni twahara au najisi ?

JAWABU : Ikiwa hufahamu ya kuwa zimetengenezwa kwa kutumia vitu najisi, au zimegusana na vitu vilivyo najisi, yatahukumiwa kuwa ni twahara.

SWALI 99 : Ikiwa mkono waote ni najisi hadi kwenye kiwiko, kisha mukallaf akaosha kitanga cha mkono pekee kwa maji kidogo au kwenye kuri, je kitanga hicho kinatwahirika pamoja na kuwa kimeungana na sehemu ya juu ya mkono ulio najisi ?

JAWABU :Ndio kinatwahirika.

SWALI 100 : Ikiwa sehemu ya ( Ruqiyyii) au tikiti maji itanajisika, je sehemu zingine nazo zitanajisika kwa sababu sehemu hizo zimeungana na sehemu hiyo iliyo najisika ?

JAWABU : Haita najisika isipokuwa ikiwa maji ya sehemu iliyo najisika yatahama na kuingia kwenye sehemu zingine.

SWALI 101 : Ikiwa vitu hivi viwili nguo na kitambaa vitanajisika vyote, je inawezekana kuosha nusu ya nguo hiyo au kitambaa hicho na nusu nyingine kubakia ikiwa najisi, na je kunatofauti katika sehemu hii kati ya kuitwahirish kwa maji kidogo au kuri au maji yenye kutiririka ?

JAWABU : Ndio inatwahirika, na hakuna tofauti kati ya maji kido na mengi, kwa sababu kigezo kwenye najisi ni kule kuhamia kwenye sehemu nyingine na si kuungana kati ya vitu hivyo.

UDHU

NAMNA YA KUTAWADHA

SWALI 102 : Je kuosha katika udhu kunathibitika kwa kumwagia au kumimina maji kwa kitanga mara moja kwa kila kiungo kama uso na mikono miwili mpaka mchoto au umwagiaji wa tatu  uwe ni haramu ?

JAWABU : Hakuthibiti kuosha mara moja kwa kumimina maji mara moja, bali kunathibitika kwa kuosha kiungo chote, Ikiwa mukallaf atamwagilia au kumimina maji kwa mara kadhaa kwa nia au kukusudia kutawadha mpaka akaosha kiungo chote hiyo huhesabika ni mara moja, na hivyo hivyo katika mara ya pili, ikiwa ataosha mkono wa kushoto zaidi ya mara mbili kisha akapaka itahesabika kuwa amepaka kwa maji yasiyo kuwa ya udhu, na kufanya hivyo kunasababisha kubatilika kwa udhu.

SWALI 103 : Ikiwa mukallaf ataosha uso na mkono wa kulia mara tatu, na mkono wa kushoto mara mbili ili isijitokeze ishkaali kwenye kupaka, je udhu huu utakuwa sahihi ?

JAWABU :Udhu wake ni sahihi isipokuwa kufanya hivyo kutatia kasoro katika makusudio ya kujikaribisha kwa mwenyezi mungu, kama akikusudia kutekeleza amri ya kisheria ihusianayo na udhu wenye uoshaji mara tatu katika kila kiungo.

SWALI 104 : Ikiwa mukallaf kwa muda mrefu alikuwa akiosha mikono yake na uso wake katika udhu mara tatu, na hakuwa akifahamu ya kuwa njia hii inasababisha ish’kaali katika kupaka, je sala zake  alizo zisali kwa udhu huu zinabatilika ?

JAWABU :Ikiwa mkono wake wa kushoto pekee  alikuwa akiuosha mara tatu udhu wake ni batili na sala zake alizo zisali kwa udhuu huo, na ni juu yake kuzirudia sala hizo na kuzilipa ( kufanya kadhaa).

SWALI 105 : Ikiwa mikono miwili tutaiweka chini ya bomba au tukaizamisha na kuitumbukiza kwenye maji kwa nia ya kutawadha na bila kupitisha vitanga kwenye mikono hoyo, je udhu huu utahesabika kuwa hi sahihi ?

JAWABU : Hakuna shaka kwa kufanya hivyo, na umajimaji wa vitanga vya mikono utautumia kupaka kichwa na miguu. Ndio wakati inapokuwa imetumbukizwa kwenye maji  mikono  hiyo huzingatiwa wakati anaitoa mikono hiyo kwenye maji awe amenuia kutawadha. 

SWALI 106 : Baadhi ya wanazuoni wamesema wazi kuwa ( Naz’atayni) si katika uso, nazo ni pande mbili za uso zilizo karibu na kichwa zisizo na nuwele, kwa hivyo  si wajibu kuziosha katika udhu, je hukumu hii inakubaliwa na maulamaa wote ( ni Ij’maa), au  mfano wake ni sawa na kuingia au kujitokeza kwa sababu kwenye uso na nisehemu yenye tofauti ?

JAWABU :Wamekubaliana maulamaa wa Imamiyyah ya kuwa (Naz’atayni) ziko nje ya mipaka ya udhu na si wajibu kuziosha, bali baadhi ya maulamaa wa Ahli sunna wanasema kuwa ni wajibu kuosha sehemu hizo.

SWALI  107 : Mgonjwa ambae hawezi kuvitingisha baadhi ya viungo vya udhu kutokana na sababu za kiafia, au kutokuwa na uwezo au kutokana na ugumu fulani, inawezekana vipi kutekeleza au kufanya  twahara tatu kwenye sehemu mbili zifuatazo :

1-Ikiwa mkono wa kushoto hauwezi kutikisika.

2-Ikiwa mikono yote miwili haiwezi kutikisika.

JAWABU : 1- Namna ya kuoga iko wazi, ama kwenye udhu, ataosha uso wake kwa kutumia mkono wake wa kulia, na mkono nao atauosha kwa uoshaji wa kuzamisha au kudumbukiza, ikiwa hakuweza kufanya hivyo atasaidiwa na mtu mwingine, na atauosha mkono wa kushoto kwa kutumia mkono wa kulia, na atapaka kichwa na mguu wa kulia kwa mkono wa kulia, na atapaka mguu wa kushoto kwa mkono wa kushoto akiweza kufanya hivyo hata kama kwa kusaidiwa na mkono wa kulia, laa sivyo atapaka kwa mkono wa kulia. Na ata tayammamu kwa mkono wa kulia kwa kuupiga juu ya ardhi, ikiwa ataweza atapiga kwa mkono wa kushoto kwa kusaidiana na mkono wa kulia juu ya ardhi, na kupaka paji lake la uso kwa mikono yote miwili, ikiwa  hakuweza  atapaka kwa mkono wa kulia  uso wote, na baada ya hapo atapangusa mkono wa kuli juu ya ardhi, kisha juu ya mkono wa kushoto kwa kutumia mkono wa kulia.

2-Tujaalie kuwa mikono yote miwili haitikisiki, ataosha uso kwa kuzamisha kwenye maji (irtimasi) au chini ya bomba, na ataomba msaada kwa mtu mwingine amsaidie kuosha mikono miwili na kupaka, na atafanya hivyo hivyo kwenye tayammam kama ilivyo tangulia.

SWALI 108 : Ikiwa juu ya kichwa na miguu miwili kuna unyevu nyevu au umaji maji kidogo, je inatosha kupaka sehemu hizi katika hali hiyo, au ni wajibu sehemu mbili hizo ziwe zimekauka ?

JAWABU : Ikiwa unyevu nyevu huo au umaji maji huo ni kidogo kiasi kwamba baada ya kupaka husemwa kuwa : Unyevunyevu uliopo ndio unyevunyevu au umajimaji wa mkono, katika hali hiyo si wajibu kukausha, laa sivyo ni wajibu kupunguza umajimaji huo kwa ajili ya kupaka.

SWALI 109 : Ni ipi hukumu ya udhu wa mtu alie funga bomba la maji kabla ya kupaka kichwa chake, hali ya kuwa juu y bomba kulikuwa na matone ya maji ?

JAWABU :Ikiwa umajimaji au matone ya maji yaliyo kuwa juu ya bomba ni kidogo kiasi kwamba umepotelea kwenye umajimaji wa kwenye mikono  hauna taaba yoyote.

SWALI 110 : Ikiwa tutapaka juu ya unyayo katika udhu mara moja, lakini maji hayakuenea sehemu yote ya mguu vizuri, nilIpi jukumu letu ?

JAWABU : Ikaushe sehemu mliyo paka na mpake tena, na hakuna taabu kupaka sehemu iliyo kavu kwa kuanzia kwenye ncha za vidole hadi sehemu ya muinuko kwenye  mguu huo.

SWALI 111 : Ikiwa nywele nyingi zitakusanyika sehemu ya mbele ya kichwa, je inasihi kupaka juu ya nywele hizo au laa ?

JAWABU : Zitatenganishwa nywelel hizo zilizoko mbele ya kichwa na kupaka kwenye maoteo ya nywele.

SWALI 112 : Je udhu unakuwa sahihi ikiwa mkono wa kupakia kichwani utafika kwenye paji la uso wakati wa kupaka ?

JAWABU : Kupaka kichwa ni sahihi, lakini atapaka miguu miwili kwa kutumia maji ya ndani ya kitanga cha mkono ambao haukugusana na kuchanganyika na maji ya uso.

SWALI 113 : Ikiwa juu ya unyayo kutanajisika, na hakuna uwezekano wa kupatwahirisha ili aweze kupaka juu yake, ni lipi jukumu lake ?

JAWABU : Ni wajibu kutayammam kwa jili ya sala.

KUONDOA  KIZUIZI  KATIKA  UDHU

SWALI 114 : Je wino ulio kaukia kwenye mkono ni wenye kuzuwia kutawadha au ni kizuizi cha  kuweza  kunizuwia kutawadha, vile vile wanja na vipodozi vitumiwavyo na wanawake ?

JAWABU :Ikiwa vitu vilivyo tajwa vina mada  izuwiayo kufika maji mwilini udhu ni batili, na ikiwa ni rangi pekee bila kuwa na mada izuiayo maji kufika mwilini kama mafuta hakuna taabu yoyote.

SWALI 115 : Je udhu unasihi ikiwa kwenye viungo vya udhu kuna mafuta ?

JAWABU : Hakuna taabu ikiwa mafuta hayakufikia kiasi kwamba inadhaniwa kuwa yanazuwia kufika maji kwenye mwili.

SWALI 116 : Ikiwa mukallaf atatawadha na baada ya kumaliza akagundua ya kuwa kuna kitu kidogo kilicho gandia mwilini mwake, lakini kitu hicho ni kidogo sana, je ni juu yake kurudia udhu ( yaani kutawadha tena) ?

JAWABU : Ikiwa kitu hicho kiligandia kabla ya kutawadha, na kina mada izuwiayo maji kufika kwenye mwili vyovyo kitakavyo kuwa kidogo, ni wajibu kukiondoa kitu hicho kilicho gandia na kutawadha tena.

SWALI 117 :  Je mafuta ya nywele za wanawake yanazuwia maji kufika mwilini au laa ?

JAWABU : Ikiwa mafuta hayo yana mada izuwiayo maji kufika mwilini  basi mafuta hayo ni kizuwizi, na hakuna taaabu ikiwa ni rangi pekaa.

USAIDIZI  KATIKA  UDHU

SWALI 118 : Ikiwa mukallaf atajiandaa kwa ajili ya udhu, na mtu mwingine akamsaidia kumfungulia bomba la maji, au akamshikia bomba  au mpira wa maji ili aweze kutawadha, je udhu huu unasihi ?

JAWABU : Ikiwa udhu wenyewe utafanywa na mukallaf mwenyewe kama ilivyo kwenye swali hakuna ishkaali yoyote katika udhu huo.

SWALI 119 :  Wagonjwa wa moyo katika kipindi ambacho wanakuwa katika mapunziko, hawawezi hata kutikisa mikono yao, je udhu wao utakuwaje ?

JAWABU : Ikiwa mgonjwa ataweza kuinua au kuutiikisa mkono wake, hatakama ni kwa kusaidiwa na mtu mwingine, ni wajibu kuutia maji mkono wake na kuutumia kuosha uso wake na mikono yake, na kupaka kichwa chake na miguu yake, ikiwa hakuweza kufanya hivyo, au kukawa na tatizo au madhara kwa mgonjwa atatawadhishwa na mtu mwingine kwa utaratibu ufuatao :

Atailowesha mikono yake kwa maji na kuosha uso wa mgonjwa na mikono yake kwa kukusudia kutawadha au kwa nia ya kutawadha, na huyo mwenye kumtawadhisha  mgonjwa atampaka kwa mkono wa mgonjwa kichwa na miguu yake.

Na ikiwa udhu kwa utaratibu huu haiwezekani, au kukawa na matatizo kwa mgonjwa, atafanya tayammam kwa utaratibu ufuatao : Mgojwa atauweka mkono wake juu ya ardhi au mchanga au juu ya kitu chochote kinacho sihi kufanyia tayammam, na ikiwa haikuwezekana kufanya hivyo  yule msaidizi atapiga kwa mikono yake juu ya ardhi kisha kupaka juu ya paji la uso wa mgonjwa na kwenye mikono  yake. 

SWALI 120 : Ikiwa mtu atamwagilia kwenye mikono ya mwenziwe maji yaliyoko kwenye birika kwa ajili ya kutawadha, je udhu huu unasihi ?

JAWABU : Hakuna taitizo katika udhu huo.

KUTAWADHA KABLA YA WAKATI WA SALA

SWALI  121 : Je inasihi kutawadha kwa nia ya kutaka kusali kabla ya kuingia wakati wa sala ?

JAWABU : Udhu unasihi ikiwa ni kwa nia ya kuwa kwenye twahara au kuwa mtwaharifu, vilevile ikiwa wakati wa sala utakaribia kwa nia ya kujiandaa kwa ajili ya sala.

KUJADDIDI UDHU (KUTAWADHA TENA WAKATI UNA UDHU)

SWALI 122 : Ikiwa mukallaf atatawadha kwa nia ya kujadidi udhu wake na kusali kwa udhu kisha ikabainika kuwa alikuwa na hadathi kabla ya udhu huo, je sala yake aliyo isali kwa udhu huo  itakuwa sahihi ?

JAWABU : Sala yake ni sahihi, na  anaweza kutekeleza matendo mengine  ambayo ni sharti kuwa na udhu katika kufanyikake  kwa matendo hayo.

KUTAWADHIA MBELE YA WATU WASIO KUWA MAHRAM

SWALI 123 : Ni ipi hukumu ya udhu wa mtu alie tawadha hali yakuwa akiangaliwa na mwanamke asiekuwa mahram wake ( yaani mwana mke awezae kumuoa) ?

JAWABU : Udhu wake ni sahihi, lakini haijuzu kwa mwanamke kumuangalia mwanamume huyo.

SWALI 124 : Je udhu wa wanawake wanao tawadhia mbele ya wanaume ambao ni mahramu wao unasihi ?

JAWABU : Ni juu ya wanawake hao kufunika miili yao kwa watu wasio kuwa mahram wao, alaa ayyi hali udhu wa wanawake hao ni sahihi.

UDHU WA JABIRA (BANDEJI AU PIOPIO) 

SWALI 125 : Je sala ya mtu mwenye jeraha au kidonda alie weka mkono wake kwenye nailoni na akatawadha udhu wa irtimaasi (kuzamisha kwenye maji), au akaosha bandeji badala ya kupaka ni sahihi ?

JAWABU : Udhu ulio tajwa ni batili na ni juu yake kurudia sala hiyo.

SWALI 127 : Mtu ambae mkono wake  wote wa kulia umetiwa piopio, atatawadha vipi ? 

JAWABU : Kwanza ataosha uso- ima kwa kuuweka chini ya bomba, au kwa kuuzamisha kwenye maji, au kwa kutumia mkono wa kushoto- kisha atapaka juu ya piopio katika mkono wa kuli, kisha atauingiza mkono wa kushoto kwenye maji na kuutoa kwa nia ya kutawadha, au atauweka chini ya bomba la maji kwa ajili ya kutawadha, na kwa kutumia unyevunyevu wa mkono wa kushoto atapaka kichwa na miguu miwili.

SWALI 127 :  Mtu  ambae mkono wake umejeruhiwa na jukumu lake ni kufanya udhu wa jabira, je inawezekana sehemu iliyo jeruhiwa hadi kwenye zandi au kwenye kiwiko kuiweka kwenye mfuko wa nailoni na kutawadha ?

JAWABU : Hakuna tatizo, lakini ni wajibu mfuko huo usiifunike sehemu ambayo inawezekana kuoshwa, na atapaka kwa mkono mwingine- kwa nia ya udhu wa jabira- juu ya mfuko, na haitoshi kutosheka na kuuosha pekee.

SWALI 128 : Ni lipi jukumu la mgonjwa ambae ametawadha udhu wa jabira kwa kuogopa maradhi, kisha ikabainika baada ya sala ya kuwa hofu yake (kuogopa kwake) haikuwa na maana ?

JAWABU :Kauli ya ahwat ya wajibu ni kuwa atarudia sala.

JERAHA LILILOKO  KWENYE  KIUNGO  CHA  UDHU

SWALI 129 : Ni lipi jukumu la mtu alie taka kutawadha hali ya kuwa juu ya mkono wake au usoni kwake kuna jeraha ambalo linatiririka damu na hadhuriki kwa kutumia maji ?

JAWABU :Ataosha sehemu ya jeraha kwenye maji ya kuri au chini ya bomba hadi damu itoweke, na ataweka mkono wake kwenye jeraha ili damu isitoke,  na atanuwia kwa haraka kutawadha na kumwagia maji juu yake, kisha baada ya hapo ataendelea na viungo vingine. 

UDHU WA MGONJWA NA ALIE KATIKA MOJA KATI

YA VIUNGO VYAKE

SWALI 130 : Ni ipi hukumu ya udhu na sala ya mtu alie ziba sehemu za kutokea haja kubwa, na tiyari amekwisha fanyiwa opresheni ya kuunganisha utumbo wake  kwa  kuweka mfuko wa nje  kupitia kwenye ngozi ya tumbo  na mwili ?

JAWABU : Ikiwa haja kubwa inatoka bila kukoma, kiasi kwamba hawezi kutawadh na kusali lau kwa kufanya baadhi ya matendo akiwa na twahara itajuzu kwake kusali kwa kutia udhu mara moja.

SWALI 131 : Mtu ambae amekatika mkono wake wa kulia kuanzia kwenye kiwiko, je una anguka wajibu wa kupaka mguu wa kulia ?

JAWABU: Kwanza atapaka kwa mkono wa kushoto mguu wa kulia, kisha atapaka mguu wa kushoto.

SWALI 132 : Ni ipi njia ya kutawadha  kwa mtu alie katika mikono yake miwili au miguu yake yote au mojawapo kati ya viungo hivyo ?

JAWABU :Ikiwa atakatika mikono yake kwa kuanzia juu ya kiwiko, ikiwa itawezekana kuosha uso wake yeye mwnyewe, kwa mfano kwa kuingiza uso wake kwenye maji, au kwa kuweka uso wake chini ya bomba na kunuwia kutawadha pmoja na kuchunga utaratibu, yaani kwa kuanzia juu hadi chini, na kwenye kupaka kichwa na miguu anatafuta msaidizi wa kumpaka kiasi kwamba msaidizi atampaka kichwa chake na miguu yake kwa umajimaji wa uso wake. 

Na ikiwa hakuweza kuingiza uso wake kwenye maji- kwa mfano maji yakiwa kwenye birika- katika hali hii msaidizi ata chukua jukumu la kumuosha uso wake na kumpaka kicha chake na miguu yake, na ikiwa katika mikono  yake kutabakia sehemu  chini ya kiwiko ataosha yeye mwenyewe sehemu iliyo bakia, na atapaka miguu yake kwa kutumia sehemu ile iliyo bakia.

Na kauli ya ahwat ni kuwa pia atafanya tayammam, na itakuwa kama ifuatavyo :  Atapaka paji lake la uso juu ya ardhi, na msaidizi atamsidia kwenye kupiga juu ya ardhi, na kupaka kwenye paji lake.  Na ikiwa miguu yake yote imekatika kuanzia kwenye maungio kati ya unyayo na muundi hapo hukumu ya kupaka ita anguka, na ikiwa kunasehemu iliyo bakia kwenye miguu atapaka kwenye sehemu iliyo bakia.

Na ikiwa mkono wake mmoja utakatika kuanzia juu ya kiwiko wajibu wa kuosha mkono huu utaanguka.

Na atafanya udhu kwa mkono ulio bakia kama tulivyo elezea hapo kabla, na kwa mkono huo huo atapaka  kichwa na miguu. Na ikiwa kutabakia sehemu kabla ya kiwiko ataosha sehemu iliyo bakia kwa nia ya udhu kama ambavyo ataosha mkono mwingine.

Ama kuhusiana na kupaka, ikiwa mkono wa kulia ni kigutu atapaka kwa sehemu iliyo bakia kichwani na mguu wa kulia, na kwa mkono wa kushoto atapaka juu ya mguu wa kushoto. Na ikiwa katika nyayo kutabakia sehemu ( sehemu ya juu ya unyayo), atapaka sehemu iliyo bakia, na kama hapakubakia sehemu yoyote kwenye unyayo  wajibu wa kupaka unaanguka.

SWALI  133 : Ikiwa mkono wa mgonjwa umefungwa kwa bomba la plastiki, ambalo huwekwa ndani ya mishipa ya damu, vipi ataweza kutekeleza aina tatu hizi za twahara ?

JAWABU :Ikiwa mikono yake yote miwili imefungwa atamtafuta mtu wa kumsaidia katika udhu na kumtawadhisha, na ikiwa jukumu lake ni kutayammam pia atamsaidia katika tayammam. Na ikiwa anatakiwa kuoga kwa ajili ya kusali, na hawezi kuoga atafanya tayammam kwa kusaidiwa na yule naibu badala ya kuoga.

SWALI 134 : Katika mas’ala yaliyo elezwa hapo juu, kutokana na kuwa mara nyingi damu hukusanyika ndani na katika  sehemu nyingi za mabomba hayo ya plastiki  na hata sehemu ya nje ya mabomba hayo, je inaswihi kusali pamoja na kuwepo damu hii au laa ?

JAWABU : Ndio sala yake ni sahihi pamoja na kuzingatia utwahara wa mwili wake kwa kiwango kinacho wezekana.

MAS’ALA MBALI MBALI  KUHUSIANA NA  UDHU

SWALI 135 : Kabla sija anza kutawadha, niliosha mikono yangu na uso wangu, je ni wajibu kwangu kuvikausha viungo hivi kabla ya kutawadha ?

JAWABU : Si wajibu kuvikausha.

SWALI  136 : Mtu mmoja alivuta bomba la maji kutokea kwenye nyumba ya jirani yake- bila ya idhini  ya shirika lihusikanalo na masuala ya maji- na malipo ya maji hutoa kwa jirani yake, je inajuzu kutumia maji haya kwa ajili ya kutawadha au kuoga ?

JAWABU : Ikiwa kufanya hivyo ni kinyuma cha kanuni na sheria haijuzu kufanya hivyo, na ikiwa anafahamu hivyo haiswihi kuyatumia maji hayo kwenye udhu au kuoga.

SAWLI 137 : Ikiwa kutajengwa hodhi la maji pembezoni mwa makaburi ya watoto wa maimamu (a.s) na sehemu za makaburi zingine, ni ipi hukumu ya  kutawadha kwenye mahodhi hayo ?

JAWABU : Ikiwa kwa kawaida kila mwenye kutaka  hutawadha kwenye mahodhi hayo  bila ya kuzuiliwa na yeyote, kauli ya dhahiri ni kuwa inajuzu kutawadha kwenye mahodhi hayo kutokana na kudhihiri kuwa kuna idhini ya watu wote kutumia sehemu hizo.

SAWALI 138 : Ikiwa mukallaf ataona damu usoni kwake baada ya kutawadha, na hajui je damu hiyo imetoka wakati akitawadha au bada ya kutawadha, je udhu wake huo utasihi ?

JAWABU :Ndio udhu wake ni sahihi, na kuwepo ihtimali ya kuwa damu hiyo inazuwia maji kufika kwenye ngozi au kwenye mwili  hukumu yake kusihi kwa udhu wake inategemea ikiwa aligundua wakati akitawadha.

SWALI 139 : Je niwajibu maji ya kutawadhia yawe ni maji yaliyo safishwa na kuchujwa chumvi ?

JAWABU :  si wajibu, bali hapana budi yawe ni maji mutlaqa ( halisi)

SWALI 140 : Ni ipi hukumu ya mtu mwenye kutawadha hali ya kuwa kavaa viatu vya ghasbi ?

JAWABU : Udhu wake ni sahihi.

SWALI 141 : Ni ipi hukumu ya  shaka katika kusihi kwa udhu ?

JAWABU : Ikiwa mukallaf atatia shaka baada ya kumaliza kutawadha hatoitilia maanani shaka yake hiyo, pamoja na kuwepo ihtimali ya kugundua hilo wakati wa kutawadha, na udhu wake ni sahihi, lakini ikiwa atatia shaka katikati ya udhu inamlazimu kuitekeleza sehemu aliyo itilia shaka, na kutimiza udhu wake. 

SWALI 142 : Ni lipi jukumu la mtu alie tia shaka akiwa kwenye sala ya kuwa ametawadha au hapana ?

JAWABU : Atakata sala na kutawadha kisha kusali tena, na bora zaidi nikuikamilisha sala yake kisha atawadhe na kuirudia sala yake. Ndio ikiwa atafahamu ya kuwa hali yake kabla ya kusali  ni kuwa alikuwa ni twahara ataendelea na sala yake, na haitokuwa ni wajibu kurudia.

SWALI 143 : Je udhu wa mtoto ambae haja balee unasihi, na je inawezekana kupewa Qur’ani na kuishika ?

JAWABU : Ndio udhu wake ni sahihi, na hakuna kizuizi cha kumpa au kuishika Qur’ani.

GHUSLI (KUOGA) NA HUKUMU ZAKE

SWALI 144 : Mtu alie na jeraha lililo wazi atafanya vipi ghusli na sala yake, kama ambae amejeruhiwa tumbo lake na sehemu hiyo hutoa damu bila kukatika ?

JAWABU : Ikiwa  hawadhuriki kwa kutumia maji hukumu yao ni sawa na hukumu ya watu walio wazima, na itakuwa ni wajibu kuoga  kama inavyo julikana, na ikiwa wanadhurika kwa kutumia maji itakuwa ni wajibu kuosha sehemu za pembezoni mwa majeraha kwa nia ya  ghusli ya kisheria. Na Kauli ya ahwat ni kuwa atapaka juu ya jeraha kwa mkono wake wenye majimaji ikiwa hadhuriki  kwa kufanya hivyo, la sivyo ataweka kipande cha kitambaa kilicho twahara kwenye sehemu ya jeraha na kupaka juu yake kwa mkono wenye majimaji pia, na ikiwa kiwango hiki kinadhuru pia au jeraha lina najisi na haiwezekani kukitwahirisha, ni wajibu kuosha pembezoni mwa jeraha kwa utaratibu ulio zoeleka, kwanza ataanza kwa kuosha kichwa na shingo, kisha upande wa kulia kisha upande wa kushoto, na kauli ya ahwat ni kuwa atafanya tayammam badala ya ghusli pia. 

SWALI 145 :  Wakati mwingine hutokea kwa sababu ya uzee, au kwa sababu ya baadhi ya magonjwa ya mwili baadhi ya sehemu (vitu vionekanavyo juu ya mwili) kufichika chini ya ngozi, je ni wajibu kuosha sehemu hizo zilizo fichika, au huhesabiwa kuwa ni sehemu ya ndani ya mwili ?

JAWABU : Ndio ni wajibu kuosha sehemu ambayo hapo mwanzo ilikuwa ikkihesabika kuwa ni juu ya mwili ikiwa haikufahamika kuwa imekuwa ni sehemu ya ndani.

SWALI 146 : Je kuoga ghusli fulani ya wajibu inatosheleza katika ghusli nyingine za wajibu ?

JAWABU : Ndio inatosheleza ghusli fulani ya wajibu kwenye ghusli nyingine ya wajibu.

SWALI 147 : Je ghusli ya wajibu inatosheleza katika ghusli ya sunna na kinyume chake ?

JAWABU : Ndio, ghusli ya wajibu inatosheleza katika ghusli ya sunna, lakini ghusli ya sunna haitoshelezi kunako ghusli ya wajibu kutokana na kauli ya ahwat, isipokuwa ikiwa atanuwia ghusli zote mbili.

SWALI 148 : Je inatosha ghusli ya sunna kunako ghusli nyingine ya sunna ?

JAWABU : Ndio.

SWALI 149 :  Ikiwa mgonjwa ataoga ghusli ya jabira kwa kuogopa madhara, na ikabainika baada ya sala ya kuwa hapakuwa na madhara ni lipi jukumu lake ?

JAWBU : Kauli ya ahwati ni kuwa ni lazima kurudia.

HUKUMU ZA WANAWAKE

SWALI 150 :  Mwanamke  ambae damu yake  ya mwezi imekatika na akaoga, na damu hiyo ilikatika baada ya siku tano ya ada yake, kisha akaona tone la damu katika siku ya nane ni ipi hukumu ya damu hii ?

JAWABU : Damu hii ni hedhi na niwajibu kwake kuoga tena.

SWALI 151 : Mwanamke ambae damu yake  ya mwezi imekatika baada ya kumaliza siku za ada yake ambayo huchukua siku sita au saba, kisha akaona damu ya njano, na mwanamke huyo ni mwenye shaka kuhusu damu hiyo, je ni damu ya hedhi au laa ? na je inamalizika kwenye muda wa siku kumi au laa ? ni lipi jukumu lake ?

JAWABU :Ikiwa atathibitisha ya kuwa ni damu na haikuvuka siku kumi basi itahukumiwa kwa hukumu za hedhi.

SWALI 152 :Mwanamke ambae amepatwa na janaba, na kabla ya kuoga ghusli ya janaba akatokwa na hedhi, je inaswihi kwake kuoga ghusli ya janaba katika hali hiyo kabla ya damu ya hedhi kukatika au hapana ? na ghusli zingine atazifanya vipi ?

JAWABU :Ndio ghusli yake inaswihi, na itaondoka athari ya janaba, kama ambavyo ghusli zingine nazo ni sahihi kama ghusli ya ijumaa na ghusli zingine.

SWALI 153 : Mwanamke ambae damu yake  ya hedhi imekatika baada ya siku sita, na haoni tena damu  yoyote, na katika siku ya tisa akaona damu kidogo sana na siku iliyo fuatia damu hiyo ikakatika kabisa, ni ipi hukumu ya damu hii ?

JAWABU : Damu  aliyo iona katika siku ya tisa ni hedhi, kama ambavyo atahukumiwa kuwa ni mwenye hedhi siku ambazo alikuwa hatokwi na damu hadi siku ya tisa. 

SWALI 154 : Mwana mke ambae alitokwa na hedhi katika siku ya kwanza, na katika siku ya pili  akafanya opresheni na kutoa mfuko wa kizazi, na siku za hedhi yake hazikufikia siku tatu, je ni wajibu kwake kuoga ghusli ya hedhi ?

JAWABU : Si wajibu kwake kuoga ghusli ya hedhi, kwa sababu  hukumu ya hedhi hutumika pale damu itakapo toka kwa muda wa siku tatu, na kutokana na swali hili ni kuwa atawajibika kuoga ghusli ya istihadha.

SWALI 155 :  Mwanamke ambae kafanyiwa opresheni na kutolewa mfuko wa uzazi, ni ipi hukumu ya damu ambazo zitatoka baada ya kutolewa kizazi ?

JAWABU : Ikiwa hajawa yaaisah ( yaani haja fikia umri wa kuto ona damu), kauli ya ahwat ni kuwa atazingatia na kuchunga hukumu za hedhi kama ilivyo  kuwa kabla hajatoa kizazi hicho.

SWALI 156 : Je inawezekana kwa mwanamke mwenye hedhi kuhudhuria kwenye vikao na majlisi za kusoma Qur’ani, ambavyo hufanyika katika mwezi  mtukufu wa ramadhani, na kusikiliza Qur’ani hiyo, hali ya kuwa anafahamu ya kuwa watu katika vikao hivyo husoma sura zenye sajda ya wajibu pia ?

JAWABU : Hakuna kipangamizi kufanya hivyo, lakini haijuzu kwake kusoma sura yenye sijda ya wajibu, ama kusikiliza inajuzu kwake kufanya hivyo, na nilazima kwake kusujudu akisikia aya za sajdah.

SWALI 157 : Wakati mwingine akina mama hushiriki kwenye vikao vya kusoma al-fatiha vifanyikavyo misikitini katika hali ya hedhi, wakiwa hawajui kuwa kufanya hivyo ni haramu sasa katika hali kama hii jukumu lao ni lipi ?

JAWABU : Ni wajibu kuwafahamisha kuwa ni haramu wao kuingia misikitini. 

SWALI 158 : Je inajuzu kwa wanawake wakiwa katika ada zao za mwezi kuingia kwenye haram na sehemu walipo zikwa watoto wa maimamu (a.s) ?

JAWABU : Kauli ya ahwat ni kuwa wasiingie.

SWALI 159 : Mwanamke ambae amefanyiwa opresheni na kutolewa mtoto kwenye mfuko wa uzazi na mtoto huyo hakupitia sehemu ya kawaida, lakini damu ikatoka kwa kupitia sehemu za kawaida, je damu hii itahukumiwa kuwa ni damu ya nifasi ?

JAWABU : Ndio, itahukumiwa kwa hukumu za nifasi.

SWALI 160 : Je inajuzu kwa mwenye hedhi na mwenye janaba kuingia kwenye sehemu zilizo ungana na haramu ya imamu Ridhaa (a.s) ?

JAWABU : Inajuzu kuingia, ikiwa sehemu hiyo si msikiti, na ikiwa ni msikiti haijuzu kuingia sehemu hiyo isipokuwa kwa kukatiza na kupita tu.

SWALI 161 : Mwanamke ambae alitokwa na hedhi na akasahau kuoga ghusli ya hedhi, na akasali kwa muda kadhaa bila kuoga, na alikuwa akitawadha kila anapo taka kusali sala za faradhi, ikiwa katika kipindi hiki ataoga ghusli ya sunna, je ni juu yake kulipa Sala zilizo mpita ?

JAWABU : Kutokana na kuwa ghusli ya sunna haitoshelezi katika ghusli ya wajibu kwa kauli ya ahwat, ni wajibu kwake kwa kauli ya ahwat kuoga ghusli ya hedhi, na kulipa sala ambazo alizisali bila kuoga ghusli ya hedhi.

SWALI 162 : Mwanamke ambae alitokwa na hedhi na akasahau kuoga ghusli ya hedhi, na akasali kwa muda kadhaa bila ya kuoga, na alikuwa akitawadha kwa ajili ya sala je sala yake inasihi ?

JAWABU : Ni wajibu kwake kulipa sala ambazo alizisali akiwa katika hali hiyo. Ndio ikiwa katika kipindi hicho kilicho tajwa  alioga ghusli ya wajibu  iliyo sahihi sala zake zitasihi ambazo alizisali baada ya kufanya ghusli hiyo.

SWALI 163 : Ni ipi hukumu ya damu imtokayo mwanamke wakati akitoka mtoto asie timia ?

JAWABU : Ikiwa damu hiyo ni damu iliyo toka wakati wa kuzaa basi damu hiyo ni damu ya nifasi.

SWALI 164 : Ikiwa kuna shaka ya kuwa hii ni damu ya nifasi au damu ya jeraha :

(a)- Ni upi wajibu wa mwanamke katika hali hii ?

(b)- Ikiwa nguo ya mwanamke alie mgonjwa imetapakaa damu hiyo na damu ikawa ni ndogo kuliko dirham, (kiasi cha ncha ya kidole cha shahada) je inajuzu kusalia nguo hiyo?

JAWABU:  A- kauli ya ahwat ni kuwa itahukumiwa na kutumika kwenye damu hiyo  hukumu za damu ya nifasi.

B- Haijuzu  kusalia nguo hiyo kwa kuli ya ahwat.

SWALI 165: Mwanamke ambae ametumia chombo cha ( I-U-D) cha kuzuwi kubeba mimba, ni lipi jukumu lake la kisheria ikiwa ataona damu akiwa kwenye hali iliyotajwa?

JAWABU: Ikiwa atakuwa na yakini ya kuwa damu itokayo ni damu ya jeraha, ni wajibu kwake kujitwahirisha kwa ajili ya sala, na damu hiyo haina hukumu maalum, laa sivyo ikiwa damu hiyo imetoka kwa muda wa siku tatu  kisha kukapita kipindi bila kutoka damu kati ya damu hiyo na damu ya hedhi ya mwanzo  na kwa muda mchache wa kuwa na twahara basi damu hiyo ni hedhi, laa sivyo ni damu ya istihadha.

SWALI 166: Ni ipi hukumu ya damu itokayo kwenye sehemu za kawaida za mwanamke ambae amefanyiwa opresheni kwa ajili ya kutoa mimba?

JAWABU: Ikiwa damu hii ni damu ya uzazi na mtoto akatoka bila kufika muda wake, itahukumiwa sawa na damu ya nifasi.

UMRI WA KUKOMA KWA HEDHI

SWALI 167: Tafadhali tupeni ufafanuzi, hadi umri gani wanawake huona  damu ya hedhi? na vipi tuta hesabu miaka ya Qamaria hijiria? kwa kufahamu ya kuwa tarehe ya kuzaliwa imeandikwa kwa miaka ya shamsia kwa kawaida?

JAWABU:  Wanawake wa kikuraishi wanatokwa na hedhi hadi miaka sitini ya Qamaria, na ni sawa na miaka 58  ya shamsiyyah na siku 77 takriiban. Na wanawake wasio kuwa Qarashia ( wasio makuraishi) hutokwa na hedhi hadi kwenye miaka khamsini (50)  ya Qamaria, ambayo ni sawa na miaka 48 na siku 179 takriiban.

SWALI 168: Mwanamke ambae anatia shaka katika kufikia kwake miaka ya yaasi (kuto tokwa na hedhi), na akaona damu na hafahamu ya kuwa damu hiyo itaendelea kwa muda wa siku tatu, ni ipi hukumu ya sala zake na funga zake katika hali kama hii?

JAWABU:  Atajengea kuwa hajafikia miaka ya kukoma kwa hedhi, na ikiwa damu inatoka kwenye siku za ada yake, au inasifa za damu ya hedhi itahukumiwa kuwa ni damu ya hedhi ikiwa haija bainika kuwa imekatika kabla ya siku tatu, na katika hali tofauti na hii atafanya ihtiyaati kati ya kuacha mambo yaachwayo na mwenye hedhi  na kufanya matendo ya mwenye istihadha mpaka imbainikie ya kuwa inaendelea kwa muda wa siku tatu, na hapo huhukumiwa kuwa ni  mwenye hedhi.

 

SWALI 169: Mwanamke ambae ametumia vidonge vya kuzuwia hedhi kisha akaacha kutumia vidonge hivyo, na akatokwa na damu kidogo na damu ikakatika kabla ya kutimiza siku tatu, je damu hii  iliyo toka itahukumiwa kuwa ni damu ya hedhi, kwa kuzingatia kuwa imetoka katika siku za ada yake?

JAWABU: Ikiwa damu hiyo haikuendelea na kutoka kwa muda wa siku tatu mfululizo, haitahukumiwa kuwa ni damu ya hedhi.

SWALI 170: Baadhi ya wanawake hutumia vidonge vya kuzuwia kutoka kwa hedhi kwa ajili ya mwezi wa ramadhani, au katika hajji kwa ajili ya kutekeleza ibada na matendo ya hijja, pamoja na kufanya hivyo huona damu katika siku za ada zao kwa muda wa siku moja au siku mbili, ni ipi hukumu ya damu hii?

JAWABU: Ikiwa damu hiyo itaendelea kwa muda wa siku tatu haitahukumiwa kuwa ni damu ya hedhi hata kama zimetoka katika siku za ada, na swaumu yake ni sahihi, na inawezekana akatekeleza matendo ya hajji, na damu hii itahukumiwa sawa na damu ya istihadha.

KUGUSA  MAJINA YA MWENYEZI  MUNGU  NA  AYA  ZA QUR’ANI TUKUFU  NA MAJINA YA MITUME NA MAIMAMU 

(A.S)

SWALI 171: Je inajuzu kugusa majina ambayo ndani yake kuna  neno  (Allah) kama Abdallah na Habibu llah na mfano wa hayo bila ya udhu, na ni ipi hukumu ya cheni iliyo nakishiwa kwa neno (Allah) ambalo ni tukufu na ambacho huvaliwa na wanawake bila ya kuwa na twahara, na wakati mwingine lafdhul jalaalah ( yaani neno Allah) hugusana na miili yao, pia ni ipi hukumu ya majina ya mitume na maimamu (a.s)?

JAWABU: Kauli ya ahwat ni kuwa haijuzu kugusa jina la mwenyezi mungu mtukufu- bila ya kuwa na twahara- vyovyote iwavyo, na sehemu yoyote na wakati wowote, na kwa lugha yoyote iwayo. Vilevile majina ya mitume na maimamu  (a.s), ama ikiwa kufanya hivyo itakuwa ni sababu ya kuvunja heshima yao, haijuzu bila ishkaali yoyote.

SWALI 172: Je inajuzu kugusa baadhi ya maneno( mfano wa ibliis) yaliyopo kwenye Qur’ani bila ya kuwa na udhu au laa?

JAWABU: Ikiwa neno hilo limo au ni katika Qur’ani haijuzu kufanya hivyo.

SWALI 173: Je inajuzu kwa mtu mwenye janaba kuweka mkono wake kwenye nembo ya jamhuri ya kiislaam, au vitu vingine vilivyo chorwa juu yake jina la mwenyezi mungu mtukufu, pia pesa za karatasi na vitambulisho vilivyo chapishwa juu yake jina la mwenyezi mungu, na ni ipi hukumu ya majina ya maimamu  na mitume (a.s)?

JAWABU:  Ni haramu kwa mtu mwenye janaba kugusa jina la mwenyezi mungu mtukufu kwa kutumia sehemu yoyote ya mwili wake, na kwa kujengea juu ya ihtiyaat ya wajibu majina ya mitume na maimamu (a.s) huunganishwa na jina hilo pia.

SWALI 174: Mwanamke ambae ametokwa na damu ya hedhi wakati ambapo amevaa cheni iliyo andikwa juu yake  jina la mwenyei mungu mtukufu, na wakati mwingine bila ya kutaka kwake cheni hiyo hugusa mwili wake, je inajuzu kuvaa cheni hii na mfano wake?

JAWBU: Haijuzu kufanya hivyo kwa kauli ya ahwat ikiwa anafahamu ya kuwa jina la mwenyezi mungu mtukufu litagusa mwili wake.

SWALI 175: Ni ipi hukumu ya mtu alie chora kwenye mwili wake majina ya mwenyezi mungu na aya  tukufu za Qur’ani  kuhusiana na twahara na janaba, na kugusa sehemu zilizo tajwa bila ya kuwa na udhu?

JAWABU: Ikiwa aya za Qur’ani zimechorwa mwilini mwake, haijuzu kuzigusa bila ya kuwa na udhu wala twahara, na niwajibu kuzifuta kwanza kisha kutawadha, bali hukumu ya kulazimika kuzifuta aya hizo kabla ya kupatwa na hadathi haiko mbali, na pia akiwa na janaba, na wakati wa kuoga, ni haramu kugusa majina matukufu ya mwenyezi mungu, na ikiwezekana ni kujiepusha kuyaondoa, au kuoga kwa kumiminia maji juu ya mwili bila ya kupitisha mkono juu yake. Na ikiwa michoro iko chini ya ngozi, na kuigusa hakuhesabiwi kuwa ni kuvunja heshima basi hakuna kizuizi kufanya hivyo. 

SWALI 176: Ni ipi hukumu ya  wanafunzi wa shule ya msingi kugusa Qur’ani tukufu, wanafunzi ambao wanajifunza Qur’ani,  isipokuwa ni kwmba wao hawajui kutawaadha vizuri, na ni lipi jukumu la mwalimu wao?

JAWABU: Kitendo chenyewe hakina ishkaali, lakini ikiwa kwa kawaida kitaonekana kuwa kinavunja heshima ya Qur’ani ni wajibu kwa mwalimu wao kuwafundisha njia ya kujilinda ili wasiiguse, au awaamrishe kutawadha, na ikiwa kugusa inahesabika kuwa  ni kuvunja heshima yake ni wajibu kwake kuwakataza kufanya hivyo.

  TAYAMMAM

SWALI 177: Mtu mwenye janaba ambae hawezi kupata maji kwa wakati wa usiku, je inajuzu kwake kutayammam kwa ajili y sala  wakati wa usiku?

JAWABU:Ndio inajuzu kwake kutayammam ikiwa anafahamu ya kuwa hato weza kuoga hadi kuchomoza kwa alfajiri.

SWALI 178: Tubainishieni namna ya kutayammam kwa kusaidiwa na  mtu mwingine (naibu au msaidizi)?

JAWABU:Msaidizi au naibu ataushika mikono ya  mgonjwa na asie weza kutayammam yeye mwnyewe, na kuipiga kwa pomoja juu ya ardhi au juu ya kitu chochote kinacho juzu kukitumia kwenye tayammam, kisha atapaka juu ya paji lake la uso na juu ya mikono yake, na ikiwa hakuweza kutikisa mikono yake  basi naibu atachukua jukumu la kupiga juu ya ardhi kwa mikono yake, na kupaka juu ya paji la uso la yule anefanyiwa kwa niaba yake na juu y mikono yake.

SWALI 179: Je inasihi kutayammam juu ya marumaru au changarawe?

JAWABU : Inasihi kutayammam juu ya mchanga na jiwe na changarewe, na kauli ya ahwat inasema kuwa ni bora kuto tayammam juu ya maru maru ikiwa vitapatikana vitu vilivyo tajwa.

SWALI 180 : Mgonjwa mwenye matatizo na ambae analazimika kutayammam kutokana na ugonjwa, na kabla ya sala udhuru wake ukatoweka, jukumu lake ni lipi ?

JAWABU :Ikiwa kizuizi kitatoweka  cha kutawadha na kuoga kabla ya kuanza kusali, tayammam ni batili.

SWALI 181 : Mtu ambae hawezi kutumia maji ya baridi kwa kutawadha na kuoga kwa sababu ya ugonjwa, na hakupata maji ya moto. Ni lipi jukumu lake katika sehemu hizi mbili zifuatazo baada ya kupata maji ya moto :

(a) Kabla ya sala ya subhi ?  (b) Baada ya sala ?

JAWABU : (a) Tayammam ni batili. (b) Sala yake ni sahihi.

SWALI 182 : Mgonjwa ambae ametayammam akiwa na jabira kwa kuogopa madhara, na baada ya sala ikabainika kuwa kuogopa kwake kulikuwa hakuna maana na hapakuwa mahali  pake, atafanya nini ?

JAWABU :Kauli ya ahwat ni kuwa atarudia sala. 

SWALI 183 : Je inasihi kisheria kufanya matendo kwa mujibu wa maelekezo ya daktari na muuguzi (nesi) kuhusiana na madhara ya kufunga na harakati za viungo, na kutumia maji kwa ajili ya udhu na ghusli ?

JAWABU : Ikiwa atapata khofu ya madhara yaani akiogopea kupata madhara kutokana na chanzo cha kiakili hata kama itakuwa ni kuelezwa na daktari au muuguzi atatosheka na habari hiyo

SWALI 184 : Je inasihi katika hali ya kutayammam badala ya ghusli ya janaba  kuingia msikitini  au kuhudhuria kwenuye sala ya jamaa ?

JAWABU :Maadamu udhuru bado upo inajuzu kuingia msikitini na kuhudhuria katika sala ya jamaa. Lakini ikiwa atatayammam kutokana na wakati kuwa finyu tu inajuzu kwake kubakia msikitini kwa kiwango cha kutekeleza sala ya wajibu.

SWALI 185 : Tuna shuhudia katika badhi ya fat’wa zikiwa zimeambatanishwa na neno (dharura) na ( uzito na matatizo) tubainishieni makusuio ya anwani hizi au maneno haya ?

JAWABU :Neno (Ad-dharuuatu) dharura lina maana : Ni kutokuwa na uwezo kwa hali ya kawaida au kutatizika kwa ajili ya kuihifadhi nafsi ili isiiangamie au isipatwe na madhara na mfano wa hayo. Na ( Al-haraj wal Usri) inamaana ya : Matatizo na mashaka ambayo kwa kawaida hayawezi kustahamilika.

HUKUMU ZA MAITI

GHUSLI, KAFAN (SANDA), MAZISHI

SWALI 186 : Mmoja kati ya mukallafiin amefariki, na hakuwa akisali wala kufunga, lakini yeye havipingi vitu viwili hivyo, je zitatumika kwake hukuwa za muislaam kama waislaam wengine ?

JAWABU : Ndio atahukumiwa kwa hukumu zote wahukumiwa nazo waislaam wengine hata kama alikuwa ni fasiki (muovu).

SWALI 187 : Mtu ambae alikuwa na jukumu la kuoga ghusli ya kumgusa maiti, je inajuzu kuosha maiti mwingine ?

JAWABU : Ndio, inajuzu kuosha maiti mwingine.

SWALI 188 : Mtu ambae alifariki kabla ya kuusia, na aliacha mtoto mdogo, na alijiwekea sanda ambayo ilikuwa na vipande vya ziada na vitambaa vya sunna, je  itatosheleza kumkafini kwa vipande vya sanda vya wajibu, kutokana na kuto usia kwake na kwa sababu ya kuwepo mtoto mdogo, au inajuzu kukafiniwa kwa kutumia vipande vilivyo zidi na ambavyo ni sunna ?

JAWABU : Kuiainisha sanda na kuiandaa ni sawa na kuusia, na ikiwa haikuzidi  theluthe ya mali yake hakuna taabu kutumia sanda hiyo ikiwa na vipande vya sunna. Bali inajuzu kutoa sanda ya kawaida na inayo lingana na hadhi yake na heshima yake hata kama kutumia sanda ndogo haitakuwa  ni sababu ya kuvunja heshima yake.

SWALI 189 : Mwanamke ambae amefariki, na mtoto  tumboni pia akafariki, je inajuzu kumtoa mtoto alie tumboni na kumuosha peke yake ?

JAWABU : Ni wajibu kumuosha mama akiwa katika hali hiyo bila ya kumtoa mtoto, kisha kumvisha sanda na kumzika kama wanawake wengine wasio kuwa waja wazito (wasio kuwa na mimba), na haijuzu kumtoa mtoto  kwenye tumbo la mama yake.

SWALI 190 : Mukallaf  ambae amefariki na alikuwa akitumia meno ya bandia, je ni wajibu kuyatoa meno yaliyo tajwa mdomoni mwake, au ni wajibu kumuosha na kumzika katika hali hiyo hiyo ?

JAWABU :Inajuzu kutoa meno hayo ikiwa haikulazimika kufanya tendo la kumkarahisha maiti, laa sivyo ataachwa na kuoshwa katika hali yake hiyo.

SWALI 191 : Mtu mmoja alivunjika mguu wake kutokana na ajali ya gari, na katika kufanyiwa opresheni akawekewa plastiki mguuni mwake, je inajuzu kutoa plastiki hilo baada ya kufariki kwake ? na ni ipi hukumu ya kifuniko cha meno  cha dhahabu au kuweka meno ya bandia ya dhahabu ?

JAWABU : Haijuzu kutoaplastiki hiyo ikiwa kufanya hivyo kutawalazimu kupasua mguu wa maiti huyo, vilevile haijuzu kung’oa meno ya dhahabu aliyo nayo. Ndio inajuzu kuyatoa meno ya bandia ikiwa kuna urahisi wa kufanya hivyo.

SWALI 192 : Mwanamke amefariki wakati akijifungua, na kichwa cha mtoto kilikwisha toka kwenye mfuko wa uzazi, yule mama akafariki pamoja na  mtoto akiwa katika hali ile, vipi ataoshwa na kuvishwa sanda yule mama na mtoto wake ?

JAWABU : Katika hali ambayo mtoto hatakuwa na ……… au mama yake mtoto atatolewa kwenye tumbo la mama yake na ataoshwa na kuvishwa sanda kila mmoja peke yake,  na katika hali tofauti na hii iliyo tajwa mama wa mtoto ataoshwa akiwa na mtoto wake na kuvishwa sanda na kuzikwa pamoja na mwanae, na kauli ya ahwat ni kuwa kichwa cha mtoto kitaoshwa peke yake pia.

SWALI 193 : Ikiwa mwanamke atafariki akiwa na uja uzito, na sisi hatufahamu hali ya mtoto ya kuwa amekufa au yuko hai nilipi jukumu letu ?

JAWABU : Ni wajibu kusubiri mpaka ithibitike hali ya mtoto, ikiwa kuna ihtimali ya kiakili ya kuwa mtoto ni mzima haja fariki, atapasuliwa tumbo leke mama huyo na kutolewa mtoto wake.

SWALI 194 : Je inajuzu kumkafini maiti kwa sanda zilizo andikwa juu yake sura ya Qur’ani kama suratu Yaasiin na zinginezo,  na kuna ihtimali ya kuwa sanda hizo zitaweza kunajisika ?

JAWABU : Ndio, inajuzu kufanya hivyo.

KUMUOSHA  ALIE PATWA  NA  AJALI  NA ALIE JERUHIWA

WALI 195 : Mtu alie kufa kwa ajali ya gari na damu ikaendelea kutoka bila kukatika ataoshwa vipi ?

JAWABU : Kama kuna uwezekano atasubirishwa mpaka damu ikatike, ikiwa haikukatika basi sehemu itokayo damu kutabandikwa kitu kama gundi na mfano wake mpaka ikatike damu hiyo kisha kumuosha. Na ikiwa haikuwezekana ataoshwa katika hali yake hiyo kwa kutumia maji yenye kutiririka au maji ya kuri, na kwa njia hii : sidri na kaafuri zita wekwa kwenye chombo na kuunganishwa na maji ya bomba- ambayo hukumu yake ni hukumu ya maji ya kuri- na watamwagia maji na kumuosha, au sidri  na kaafur itawekwa kwenye maji ya kuri kwa kiasi amabacho inathibitika kuwa ni maji ya sidri na maji ya kafuur bila kufikia kuwa ni maji mudhaaf, kisha ataoshwa maiti kwa maji hayo,  na ataoshwa kwa utaratibu kama tulivyo elezea katika kitabu chetu cha hukumu. Na ihtiyaat ni kuwa sehemu za kutayammam zita kaaushwa baada ya kumuosha, kisha atatayammamishwa baada ya kumuosha pia.

SWALI 196 : Mtu ambae amejeruhiwa na kufariki, hakuna kitu chochote kama bandeji au kitu kingine cha kumgandishia ili kuzuwia kutoka kwa damu, je mwili kama huu inajuzu kuuweka kwenye mfuko wa plastiki, na kuvishwa sanda kwa kutumia vipande vyake vitatu juu ya mfuko huo wa plastiki,  kwa sababu bila ya mfuko huu damu ita tapakaa kwenye plastiki vyovyote itakavyo kuwa ?

JAWABU :  Hutumika njia hii, lakini baada ya kuoshwa au kutayammamishwa.

SWALI 197 : Ni ipi hukumu ya mtu ambae kutokana na ajali kichwa chake kifua chake na tumbo lake vimetengana na kutawanyika kutokana na ajali hiyo ya gari ?

JAWABU : Itaoshwa sehemu ambayo imeshikana na mifupa, na itafungwa kwenye kitambaa na kuzikwa, na ikiwa kifua kipo na kimeshikamana na moyo, ataswaliwa pia baada ya kuoshwa na kuzikwa.

SWALI 198 : Mtu ambae amefariki katika tukio la ajali ya gari, na kichwa chake kimetawanyika na mwili wake wote, na akawekwa kwenye mfuko, ataoshwa vipi ?

JAWABU : Ikiwa viungo vyake havikutawanyika ataoshwa kama kawaida, na katika hali tofauti na hii, ikiwa mikono yake ni mizima atafanyishwa tayammam, laa sivyo ghusli na tayammam  kwake vita anguka, na katika sura kama hii atasaliwa akiwa kwenye mfuko na kuzikwa.

SWALI 199 : Mtu ambae amefia kwenye maji na akabakia kwenye maji kwa muda mrefu kiasi kwamba mwili wake ukatuna na kuvimba kwa maji vipi itawezekana kuoshwa ?

JAWABU : Ikiwa mwili wa maiti haukuchanika chanika kwa kuoshwa  na kusambaa ataoshwa kama kawaida, laa sivyo ata tayammamishwa.

SWALI 200 : Ni ipi hukumu ya mtoto alie fia tumboni, ambae umri wake ni  zaidi ya miezi minne, na ilibidi kumkatakata kwa ajili ya kumtoa tumboni mwa  mama yake ?

JAWABU : Vipande vya nyama vitafungwa kwenye kitambaa na kufukiwa, na vipande ambavyo vimeshikamana na mifupa na kifua na moyo huoshwa na kuvishwa sanda na kuzikwa.

SWALI 201 : Mwili wa maiti  ambao ulipasuliwa kisha ukashonwa, katika hali ya kushonwa baadhi ya sehemu ya mwili au ngozi ikaingia ndani, na ukashonwa kwa namna ambayo katika kuoshwa maji hayakufika sehemu yote ya mwili, jukumu ni lipi katika kumuosha ?

JAWABU :  Maiti huyo ataoshwa katika hali yake hiyo, na kauli ya ahwat ni kuongezea tayammam.

NAMNA YA  KUMTAYAMMAMISHA  MAITI

SAWLI 202 : Katika sehemu ambazo ni wajibu maiti kutayammamishwa ni vipi ata tayammamishwa ?

JAWABU : Mtu ambae anamtayammamisha maiti, niwajibu kwake kupiga juu ya ardhi kwa mikono yake na kupaka uso wa maiti na juu ya vitanga vyake vya mikono, na kauli ya ahwati  ya wajibu ni kuwa ikiwa itawezekana atapiga kwa mikono ya maiti kisha kumtayammamisha kwa mikono yake.

KUMSALIA MAITI

SWALI 203 : Ikiwa litaletwa jeneza lingine katikati ya sala ya maiti wa mwanzo je inajuzu kumshirikisha pamoja na maiti wa kwanza katika takbira za sala zilizo bakia ?

JAWABU : Ndio, inajuzu, lakini ni wajibu kwa kila mmoja kumsomea dua kati ya maiti hao inayo mhusu, kwa mfano ikiwa ataletwa kabla ya takbira ya tatu atatoa takbira na kutekeleza wadhifa wa sala ya maiti wa kwanza yaani dua kuwaombea waumini wa kike na kiume, na kusoma shahada mbili kwa ajili ya sala ya maiti wa pili na kuendelea, na baada ya kumaliza sala ya jeneza la kwanza atafanya  takbira zilizo bakia na dua zihusianazo na jeneza la pili.

SWALI 204 : Ikiwa maiti hajafikia balee imam khomainiy (mungu amrehemu) anasema katika kitabu  cha mas’ala kwamba : baada ya kusoma takbira ya nne husomwa dua ifuatayo : ( اللهم اجعل لأبويه ولنا سلفا وفرطا وأجرا) je mheshimiwa ana rai kama hiyo?

JWABU : Mkitoa takbira ya nne kama swali lisemavyo, mtasoma dua iliyo tajwa, kisha mtatoa takbira ya tano, na hapo sala itakuwa imemalizika.

HUKUMU ZA KUZIKA, KUFUKUA KABURI NA KULIJENGEA

SWALI 205 : Je inajuzu kumzika maiti kwenye kaburi alipo zikiwa maiti mwingine kwa miaka kadhaa iliyo pita, pamoja na kuwa kuna ihtimali yenye nguvu ya kuwa maiti yule wa mwanzo nyama yake imekwisha toweka na kumebakia mifupa  pekee ?

JAWABU : Haijuzu kumzika maiti katika kaburi la maiti mwingine ikiwa kufanya hivyo kutawalazimu kufukua kaburi lake na kudhihiri kwa kiwiliwili chake na kuvunja heshima yake, na kabla ya kufahamu ya kuwa mifupa ya  maiti wa kaburi la kwanza imegeuka na kuwa mchanga na kutawanyika haijuzu kufukua kaburi lake, ndio, ikiwa  kazi ya kufukua kaburi lake itafanyika japokuwa kwa kuasi, wakati huo inajuzu kumzika maiti mwingine katika kaburi la maiti wa mwanzo bila ya kuwa na karaha yoyote.

SWALI 206 : Maiti ambae kishazikwa- inavyo onekana amefariki kutokana na athari ya kupigwa au  kushambuliwa- je inajuzu kufukua kaburi lake kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa sababu ya kufariki kwake ?

JAWABU :Hakuna kizuizi ikiwa kuithibitisha haki ya maiti itasimama na kutegemea kufukuliwa kwa kaburi lake, na mujtahi alie timiza masharti akatoa fatwa ya ulazima wa kufukuliwa kaburi lililo tajwa.

SWALI 207 : Ni kipi kigezo katika uharamu wa kufukua kaburi la maiti ?

JAWBU : Hakika kigezo na dalili ya uharamu wa kufukua kaburi la maiti ni kudhihirisha kiwiliwili chake au kuvunja heshima yake, hakika kuchukua kiasi fulani cha mchanga wa kaburi na bila kudhihiri kiwiliwili cha maiti, huko hakuhesabiwi kuwa ni kuvunja heshima yake kwa kawaida, na wakati huo huko si kufukua wala hakuna uharamu kufanya hivyo. Na kwa muhtasari ni kuwa : Hakika kigezo na dalili katika uharamu wa kufukua kaburi ni kule kudhihiri kwa kiwiliwili au kuthibiti anwani ya kuvunja heshima ya maiti kwa kufanya tendo hilo, na inawezekana mambo haya mawili yakakusanyika, vilevile inawezekana sababu ikawa ni kudhihirisha kiwiliwili cha maiti pekee, na kuvunja heshima yake pekee.

SWALI 208 : Kaburi lenye tabaka mbili, katika tabaka ya kwanza amezikwa mwanamke, je inajuzu kumzika mwanaume katika tabaka la juu, kwa kufahamu ya kuwa si mahramu wa mwanamke huyo ?

JAWABU : Ndio inajuzu, ikiwa kufanya hivyo hakutalazimu kufukua kaburi la maiti wa tabaka la chini yake.

SWALI 209 : Yamegunduliwa makaburi katika kijiji kimoja kilicho maarufu kwa jina la ( Piir ghiib) na wazee wanasema : hakika makaburi haya yalikuwa yamejengewa na kulikuwa na jengo kwenye makaburi hayo, na hakuna mti wa nasabu ya mwenye kaburi hilo ?

JAWABU : Hakuna kizuizi cha kujenga jengo juu ya makaburi hayo yaliyo tajwa, ikiwa wazee hao wanauhakika ya kuwa kaburi hilo ni mmoja wapo kati ya watoto waa maimau wema (a.s).

SWALI 210 : Je kuyapamba makaburi kwa mawe ya marumaru nyeupe na nyeusi kuna ishkaali ?

JAWABU : Hakuna ishkaali kufanya hivyo.

SWALI 211 : Makaburi yamebomolewa kwa sababu ya kujenga bustani ya kupumzika watu wote na  kwa sababu ya ramani ya kupitisha barabara  sehemu hiyo,  na kaburi moja likaathiriwa na kubomoka kwenye sehemu ya kupitia ramani ya  bomba la maji katika upande mmoja wa barabara, je inajuzu kufukua sehemu ya kaburi hilo iliyo bakia na kuihamishia kwenye makaburi ya watu wote, kwa sababu kubakia katika hali kama hii kutasababisha kuvunjiwa heshima yake ?

JAWABU : Inajuzu kufanya hivyo ikiwa haikuwezekana kubadilisha sehemu lipitapo bomba au ramani iliyo tajwa.

SWALI 212 : Je inajuzu kutekeleza usia wa mtu alie usia kukihamishia  kiwiliwili chake baada ya kuzikwa kwenye sehemu takatifu walipo zikwa maimamu ?

JAWABU : Hakika kwa mtizamo wangu kufukua kaburi kwa lengo la kumhamishia maiti kwenye sehemu tukufu za maimu tendo hilo linapingana na ihtiyaat, hata kama maiti atakuwa ameusia hivyo. Ndio ikiwa atausia kuhamishiwa  jeneza lake kabla ya kuzikwa kwenye mashaahidi musharrafah ( sehemu takatifu walipo zikwa maimamu), na kwa makusudi usia wake haukutekezwa au kutokana na sababu fulani, katika hali kama hii inajuzu bali ni wajibu kwa mtu alie usiwa kufukua kaburi na kulihamisha jeneza ili likazikwe sehemu iliyo usiwa, isipokuwa ikiwa nyama ya mwili wake  itakuwa imetawanyika, au kulifukua kaburi  itakuwa ni sababu ya kuvunja heshima ya maiti alie tajwa, wakati huo haita juzu kulihamisha.

MAS’ALA MBALI MBALI KUHUSIANA NA HUKUMU ZA MAITI

SWALI 213 : Je inajuzu kumuweka maiti ndani ya msikiti kabla ya kuoshwa au hapana ?

JAWABU : Inajuzu ikiwa hato unajisisha msikiti.

SWALI 214 : Ni ipi hukumu ya matumizi ambayo hutolea na watu wa karibu au jamaa wa maiti katika siku tatu za msiba na usiku wa saba na siku ya arobaini ya maiti, wakati ambapo  wakati mwingine  wao huwa ni katika tabaka la mafukara ?

JAWABU : Hakika matumizi hayo si ya wajibu, bali kunashubha ya kisheria wakati mwingine, na pengine huwa ni sababu ya kuwatia kwenye matatizo wale mafukara, na pengine  kutoa kwao kukahesabika ni sababu ya kujihini na kujidhalilisha.

SWALI 215 : Ni kazi gani ambayo ni wajibu kuifanya watu wa karibu au jamaa wa maiti  katika siku ya saba na siku ya arobaini, na je zawadi za maua waridi na mafungu ya maua yenye thamani ya hali ya juu huhesabiwa kuwa ni israafu ?

JAWABU : Ni bora kwa jamaa wa maiti na watu wa karibu kumpa zawadi ya mambo ya kheri na mambo mema kwa niaba ya roho wa marehemu, na kujizuwia kufanya matendo yasiyo na faidi (kwa maiti).

SWALI 216 : Wakati wa kupita  kwenye makaburi ya mayahudi na wakiristo, je inajuzu kusoma alfaatiha ?

JAWABU ; Haijuzu ikiwa ni kwa nia ya kuwasomea wao.

SWALI 217 : Maiti asie fahamika amezikwa kwenye makaburi fulani, na baada ya kuzikwa maiti yule jamaa zake na walii wake wakamtambua, na kwamba maiti huyo anaishi kwenye mkoa mwingine, ambapo ni vigumu kwenda na kurudi kwa ajili ya kuzuru kaburi lake ziara ambayo hupunguza majonzi ya msiba kwa mama wa maiti na watu wake wa karibu, wao wanataka kuzuru kaburi hilo la ndugu yao wakati wote, je inajuzu katika hali kama hii iliyo tajwa kufukua kaburi  lake na kulihamishia jeneza hilo kwenye mji wao au laa ?

JAWABU : Ikiwa kufanya hivyo hakusababishi kuvunja heshima ya maiti hakuna tatizo kufanya hivyo.

HUKUMU ZA MISIKITI NI KITU GANI KITHIBITISHACHO KUWA HUU NI MSIKITI ?

SWALI 218 : Ardhi ambayo imeungana na msikiti, wamiliki wa ardhi hiyo wameamua ya kuwa iunganishwe na jengo la msikiti, na mmoja wao alisali rakaa mbili kwenye ardhi hiyo ili kutekeleza uamuzi wao huo na ili wasijute hapo baadae. Je kwa kufanya hivyo ardhi hii inakuwa ni sehemu ya msikiti au laa ? na je inawezekana kujenga nguzo kwenye tabaka la chini katika ardhi hii, au kujenga jengo lingine kwa ajili ya kukodisha wachuuzi kwa mapato ya msikiti ?

JAWABU : Inathibiti kuwa ardhi hii  imekuwa waqfu pale tu mwenye ardhi atakapo sema kuwa ardhi hii ni waqfu kwa ajili ya msikiti na kuikabidhi au kuitoa kwa ajili ya matumizi ya watu wanao sali ili waweze kuitumia kwa kusalia kwenye ardhi hiyo na wakati huo haijuzu kuitumia ardhi hiyo kwa kitu kingine tofauti na msikiti, haijuzu kujenga nguzo  na vitu vinginevyo chini yake, isipokuwa ikiwa tabaka hilo limetolewa kwenye waqfu hiyo tangu mwanzo wa kuwekwa waqfu, na ikiwa mtu alie weka waqfu hatatoa ruhusa ya kusali kwenye ardhi hiyo bado anwani ya waqfu haija thibiti, kwa hivyo hiari ya kuitumia inakuwa bado iko mikononi mwa alie iweka waqfu. Kwa hivyo anaweza kutoa tabaka moja na kuliweka waqfu kwa ajili ya msikiti, na tabaka la chini kwa ajili ya manufaa mengine na vinginevyo.

KUUKARABATI  MSIKITI  NA KUUJENGA UPYA KWA KUUPANUA  NA KUUPUNGUZA

SWALI 219 : Msikiti umebomoka kutokana na tetemeko la ardhi, na watu wa maeneo hayo wamehamishiwa sehemu yenye umbali wa kilometa mbili kutokea kwenye msikiti huo na wakaanzisha msikiti mpya sehemu hiyo, na ule msikiti wa mwanzo una vitu vilivyo wekwa waqfu ambavyo nilazima kuvitumia katika kuukarabati, je inawezekana kuvitumia vitu hivyo katika kukarabati msikiti mwingine ?

JAWABU : Ni wajibu kuukarabati msikiti ule ule wa mwanzo, na kutumia vitu vilivyo wekwa waqfu katika sehemu ileile ambayo kwa ajili yake vimewekewa waqfu.

SWALI 220 : Wakati wa kujenga madrasa au msikiti au husayniyyah ilionekana chini ya ardhi hiyo mifupa ya maiti, je kuwepo kwa mifupa hii ni dalili ya kuwepo makaburi ya muda mrefu kwenye sehemu hiyo ?

JAWABU :  Ile tu kuonekana kwa mifupa haiwi dalili ya kuwa sehemu hiyo ni sehemu ya makaburi, na kulingana na swali lilivyo mifupa hiyo itazikwa sehemu hiyohiyo au sehemu nyingine.

SWALI 221 : Katika kujenga upya msikiti ni lazima kuusogeza nyuma ukuta wa msikiti kwa mita kadhaa, ili mita hizo ziwe ni sehemu ya barabara kulingana na kanuni za mji, je inajuzu kufanya hivyo ?

JAWABU : Haijuzu ikiwa hakuna ulazima wa kufanya hivyo.

SWALI 222 : Msikiti na Huseiniyyah vimeungana, na baada ya kuujenga upya msikiti sehemu fulani ya Huseiniyyah iliyo tajwa ikawa katika sehemu ya msikiti, je hilo linajuzu ? na tujaalie ya kuwa inajuzu je sehemu hii itahukumiwa sawa na hukumu za msikiti ?

JAWABU : Huseiniyyah kuiunganisha na msikiti kuna ishkaali. Na sehemu iliyo tajwa kuiunganisha na msikiti hakuifanyi iwe ni sehemu ya msikiti, kama ambavyo haita hukumiwa kwa hukumu za msikiti.

SWALI 223 : Kwenye umbali wa mita mia moja kutokea kwenye masjidul jaamiah, kuna msikiti ulio hamwa na kuachwa, na msikiti huo umeharibika na kubomoka, je inafaa kufanya nadhiri kwa ajili ya msikiti huo ?

JAWABU : Inajuzu kuukarabati msikiti huo  na kuujenga upya, na bora zaidi ni kusalia kwenye msikiti huo.

SWALI 224 : Ikiwa kukarabati msikiti ulio karibu na masjidul jaamiah kutasababisha kupunguza hali ya watu kuutilia umuhimu masjidul jaamiah, katika hali kama hii ni lipi jukumu la kuukarabati msikiti huo na kusalia kwenye msikiti huo.

JAWABU : Ni lazima kufanya juhudi ili hima ya watu kuuelekea masjidul jaamiah isipungue na kuto utilia umuhimu sana kutaaambatanishwa na kuudharau.

SWALI 225 : Msikiti unahitaji kupanuliwa na pembezoni mwake kuna barabara, na katika upande mwingine wa msikiti huo kuna nyumba iliyo nunuliwa  ili iwe ni sehemu ya msikiti, na kunapendekezo lilo tolewa ya kuwa barabara iliyo tajwa iwe ni sehemu ya msikiti, na kwa kufahamu ya kuwa wenye sehemu hiyo wameridhia pendekezo hilo, la kwamba nyumba iliyo nunuliwa iwe ni barabara badala ya msikiti, je jambo hili linajuzu au laa ?

JAWABU : Haijuzu kufanya hivyo isipokuwa njia ikiwa ni finyu, yaani njia hiyo iwe imezingirwa na majumba pande zote tatu, hakika njia hiyo ni milki ya wenye majumba ambayo milango yake inaelekea kwenye njia hiyo, na inajuzu kuifanya kuwa ni sehemu ya msikiti kwa kuridhia wamiliki wa majumba yale.

SWALI 226 : Msikiti ambao unahitaji sana kukarabatiwa, je inawezekana kutumia zakaatul fitri kuukarabati msikiti huo ?

JAWABU : Kilicho bora ni kuitoa zakatul fitri kwa mafukara wa mahala hapo, na hakuna taabu yoyote kuitumia zaka hiyo kwenye matumizi ya msikiti na mfano wa hayo pia.

 KUBADILISHA MSIKITI

SWALI 227 : Msikiti ambao inadaiwa kuwa umejengwa na madhalimu, na msikiti huo ndani yake kunabaridi sana kutokana na hali ya hewa ya msikitini hapo na haiwezekani kusalia msikitini humo kutokana na baridi kali baada ya kutoka kipindi cha kiangazi (kipindi cha joto), kama ambavyo haiwezekani kuweka vitia joto, na umejenga msikiti mwingine mzuri kwenye umbali wa mita mia mbili kutoka kwenye msikiti huo, je inajuzu kuuharibu na kuubomoa msikiti wa kwanza na ardhi yake kuifanya ni ardhi ya kilimo, na kutumia mapato yake kwa ajili ya msikiti mpya ?

JAWABU : Haijuzu kuuharibu na kuubomoa msikiti huo  kwa anwani na kwa sababu yoyote ile, na bora zaidi kama inawezekana kuukarabati na kusalia ndani yake, na hilo linatokana na kauli yake mwenyezi mungu ( إنما يعمر مساجد الله من آمن بالله واليوم الآخر)  Hakika misikiti ya mwenyezi mungu huimarishwa na kujengwa na watu wenye kumuamini mwenyezi mungu na siku ya mwisho.

SWALI 228 : Je inajuzu kubomoa msikiti kwa lengo la kujenga bustani ya watu wote, na bila kuwepo ulazima wowote wala mahitajio yoyote, wakati ambapo hakutakuwa na ukinzani kati ya kuwepo msikiti na mpango ulio tajwa ?

JAWABU : Haijuzu kufanya hivyo, kwa kutokuwepo ulazima wa kufanya hivyo.

SWALI 229 : Kijiji ambacho hakina maji safi na salama kwa ajili ya kunywa, na viongozi wa kijijini hapo walifanya juhudi na kuchimba kisima sehemu hiyo, kisha baadae ikabainika ya kuwa sehemu hiyo ilikuwa ni msikiti ambao uliharibika na kubomoka kwa sababu ya tetemeko la ardhi, na kwa sasa hivi hautumiki, je inajuzu kutumia kisima hicho ? na ikiwa inajuzu je inawezekana  kukijengea ukuta kwa ajili ya kukihifadhi ?

JAWABU : Hukumu ya kujuzu kutumia maji haiko mbali, lakini ardhi ya msikiti haitoki kwenye anwani ya kuwa ni msikiti, na itahukumiwa kwa hukumu za msikiti, ama kuhusiana na kuvuta mabomba na kuweka mashine ya kuvuta maji na chombo cha kuvuta au kutekea maji kwenye ardhi hiyo na kwenye kisima hicho itabidi kurejea kwa haakimus- shar ‘ii katika hilo.

SWALI 230 : Wakati wa taghuuti (SHAHA) waliubadilisha msikiti na Huseiniyyah na kuvifanya madrasa, ni ipi hukumu ya tendo hili ?

JAWABU : Ni wajibu kuurudisha msikiti na huseiniyyah kwenye hali yake ya mwanzo. 

KUINGIA MTU MWENYE JANABA NA HEDHI MSIKITINI

SWALI 231 : Kutokana na uchache wa kumbi za kufanyia mitihani katika baadhi ya sehemu au vitongoji, mitihani  ya watoto wa kike hufanyika misikitini, pamoja na kuwa baadhi yao huwa katika hali ya hedhi, na wao wanalazimika kushiriki kwenye vikao vya mitihani laa sivyo watafeli na kupata hasara kwenye mitihani hiyo, je inajuzu  kuteua misikiti iwe ni sehemu ya mabinti hao kufanyia mitihani ? na ikiwa mtihani utafanyika msikitini je inajuzu kwa mabinti ambao wako kwenye hali ya hedhi kushiriki kwenye mtihani huo ?

JAWABU : A- ni lazima kwa viongozi au wasimamizi wa mitihani kuzingatia na kuangalia kwa makini mahala palipo tajwa, na kuchagua huseiniyyah kwa ajili ya mitihani badala ya misikiti.

B- Inajuzu  kuingia msikitini wakati wa dharura ambayo moja kati ya vielelezo vyake ni sehemu iliyo tajwa. 

SWLI 232 : Mtu mwenye janaba ambe hawezi kuoga, je inawezekana kwake kutayammam na kuingia msikitini kwa ajili ya kusali sala zake kwa jamaa ?

JAWABU : Ikiwa- ni kwa sababu ya udhuru wa kisheria kama maradhi na kuto kuwepo maji na mfano wa hayo- jukumu lake ni kutayammam na inawezekana kwake kuingia msikitini kwa tayammam ile na kubakia msikitini kama watu wengine.

KUINGIA MSIKITINI MTU ASIE KUWA MUISLAM

SWALI 233 : Je inajuzu kwa Ahlul kitab kuingi msikitini, kwa ajili ya kushiriki kwenye kikao cha kusoma Alfatiha kwa ajili ya marehemu ambae ni rafiki yao na kwa kuzingatia kuwa ni  watu wanao mfahamu, au ni lazima kuwazuwia ?

JAWABU : Si wajibu kuwakataza, ikiwa kuhudhuria kwao si kuvunja heshima ya msikiti.

SWALI 234 : Ardhi yenye kumilikiwa na muislaam na mkiristo lakini hisa ya kila mmoja haieleweki na kwa kuridhia wote wawilii ardhi hiyo imekuwa msikiti, na mkiristo yule anashiriki kwenye vikao vifanyikavyo kwenye msikiti ule hata kikao cha kumbukumbu za baba yake hufanyika msikitini hapo, je kisheria inajuzu kufanya hivyo, na je hilo halisababishi kuvunja heshima ya msikiti ?

JAWABU : Haijuzu kufanyika vikao vya kumbukumbu za kifo cha mkiristo na mwinginewe asie muislaam msikitini.

VITU VILIVYO WEKWA WAQFU, NADHIRI NA VILIVYO 

TOLEWA ZAWADI  KWA AJLI YA MSIKITI

SWALI 235 : Je inajuzu kuuza vyombo vilivyo wekwa waqfu kwa ajili ya husainiyyah na msikiti, kwa sababu  vitu hivyo ni vikuu kuu na haiwezekani tena kutumika, na je inajuzu kuvibadilisha kwa kuchukua vitu vingine vilivyo vizuri zaidi au kununua vifaa viliyo vipya ?

JAWABU : Ikiwa hakuna uwezekano wa kuvitumia inajuzu kuvibadilisha kwa vyombo vipya.

SWALI 236 : Mtu mwenye kufuata dini vizuri, amejenga msikiti na madrasa ndogo, na akaweka waqfu na  mali zenye kumilikiwa na mali zisizo hamishika kwenye msikiti huo, na baada ya kufariki, mtu mwingine akajenga msikiti na madrasa kubwa mahala pa msikiti na madrasa hiyo, je inawezekana kutumia vitu vilivyo wekwa  waqfu kwa ajili ya msikiti na madrasa hiyo kwa ajili ya msikiti na madarasa mpya au kwa ajili ya mafukara ?

JAWABU :Ikiwa msikiti na madrasa mpya ni  msikiti ule ule na marasa hiyohiyo ya zamani isipokuwa tu vimefanyiwa mabadiliko, ni wajibu vitu vilivyo wekwa waqfu  vitumike kwenye sehemu zilizo wekwa waqfu kwenye msikiti na madrasa hiyo. 

SWALI 237 :  Ardhi iluyo wekwa waqfu kwa ajili ya kuutia mwanga msikiti, na sehemu kubwa ya ardhi hiyo imekuwa sehemu ya barabara, ikiwa kutajengwa jengo la kibiashara au nyumba ya kuishi kwenye ardhi hiyo iliyo tajwa, je jengo hili linahesabiwa ni katika vitu vilivyo wekwa waqfu, au waqfu ni ardhi pekee ?

JAWABU :Waqfu ni ile ardhi pekee, na la wajibu ni kuitumi pesa ya kodi ya nyumba hiyo kwa ajili ya kuutia mwanga msikiti.

SWALI 238 : Vyombo na vitu vingine vilivyo tolewa zawadi kwa ajili ya msikiti kwa anwani ya nadhiri kama feni, taa, sahani na vikombe vya chai, ikiwa vitu hivyo ni vingi kuliko mahitajio, je inawezekana kwa mtu anae simamia msikiti huo kuviuza vitu hivyo na kutumi thamani yake kwa ajili ya matumizi ya lazima ya  msikiti.

JAWABU :Hakuna kizuizi kufanya hivyo ikiwa msikiti hauna mahitajio ya vitu vilivyo tajwa. 

SWALI 239 : Huseiniyya iliyo haribika na kubomoka, na watu wa sehemu hiyo hawana uwezo wa kuikarabati, je inajuzu kuikarabati kwa mali ya waqfu ?

JAWABU : Hakuna kizuizi ikiwa vitu vilivyo wekwa waqfu havikuwa maalum kwa ajili ya maombolezo ya msiba na matumizi yake, bali vitu vyote vitumikavyo kwa ajii ya imam Hussein (a.s), katika sura hii inajuzu kufanya ukarabati au kuijenga upya husiniyya kwa kutumi vitu hivyo vya waqfu. VITU VYA MSIKITI 

SWALI 240 : Tumebomoa msikiti kwa lengo la  kuujenga upya, na baada ya kuujenga upya msikiti huo ukawa ni wenye deni, je inajuzu kuuza sementi na chuma na mbao zilizo zidi na mikeka iliyo tumika ambayo msikiti hauihitajii ili kulipa madeni ya msikiti ?

JAWABU : Hakuna kizuizi cha kuuza vitu vilivyo zidi kwa lengo la kulipa madeni ya msikiti, lakini mbao na vyuma vilivyo tumika ni wajibu kuvitumia katika msikiti mwingine, na hakuna kizuizi kuviuza katika sura ambayo misikiti mingine haitakuwa na haja ya vitu hivyo 

SWALI 241 : Je inawezekana  kuuza  samawar (birika la kuchemshia maji)  litumialo  mkaa lililo wekwa na mtu mwema, kutokana na msikiti kuto lihitajia, na kununua mabusati badala yake ?

JAWABU : Ikiwa msikiti  mwingine utahitajia samaawar hiyo

( Birika hilo) lililo tajwa litatolewa kwenye msikiti ule, na katika sura ambayo hakutakuwa n msikiti unao hitajia litabadilishwa kuwa birika litumialo gesi na mfano wa hilo, laa sivyo thamani yake itatumika kwa mhudumu wa msikiti. 

SWALI 242 : Je inawezekana kuhamishia vyombo vya msikiti na husainiyyah na nyenzo zake sehemu nyingine kwa ajili ya matumizi ya watu wote ?

JAWABU : Ikiwa vitu hivyo ni waqfu kwenye msikiti au huseiniyyah haijuzu kuvihamisha na kuvitoa kwenye mahala pake.

SWALI 243 : Msikiti ambao  wakati mwingine hutumika kwa ajili ya sala ili usiharibike, je inawezekana kuhamisha vitu vya kwenye msikiti huo kama mabusati na miswala na vyuma, matofali  na kuvipaleka kwenye msikiti mwingine ?

JAWABU : Haijuzu, bali vitumike katika msikiti huo huo, na ni juu ya waumini kulinda na kuhifadhi heshima ya msikiti huo.

SWALI 244 : Masjidul jaamiah ulibomoka, na kwa hivi sasa tuna shughulikia ujenzi wake upya,  -katika hali hii- vitu na vifaa vya nsikiti huo havitumiki, je inawezekana kutumia vifaa vya msikiti huo katika husainiyyah ambayo iko karibu na msikiti huo ?

JAWABU :Ikiwa vitu hivyo ni waqfu kwenye msikiti huo haijuzu kuvitumia.

SWALI 245 : Mswala wa msikiti mmoja wapo umekuwa mkuukuu, na ikiwa utabakia msikitini utaharibika, je inajuzu kuuza au kuubadilisha kwa  ulio mzuri zaidi yake ?

JAWABU :Ikiwa ni waqfu kwenye msikiti huo, haijuzu kuubadilisha wala kuugeuza bila idhini ya kisheria, na ukiwa ni milki ya msikiti  inajuzu kuubadilisha kulingana na maslahi.

SWALI 346 : Vitu ambavyo hutolewa zawadi kwa ajili ya msikiti kwa mfano sukari na vyombo vya kuwekea sukari, na chai na vinginevyo wakati mwingine huvitumia baada ya kupita muda mrefu, je inawezekana kuviuza na kutumia thamani yake kwenye msikiti huohuo, au ni wajibu kuvihamishia vitu hivyo kwenye msikiti mwingine ?

JAWABU : Inajuzu kwa msimamizi kuviuza kulingana na maslahi ayaonayo katika kufanya hivyo na kutumia thamani yake kwenye mambo mengine ya msikiti huo.

SWALI  247 : Kabla ya miaka hamsini iliyo pita kulijengwa msikiti,  na kwa hivi sasa inaogopewa kuukarabati kwa kuwa uko kwenye njia ya mafuriko, je inawezekana kujenga msikiti mwingine, na kutumia mali za msikiti huo kwenye msikiti mpya ?

JAWABU : Ikiwa haikuwezekana kubailisha njia ya mafuriko ambayo yanautishia msikiti huo, inajuzu kutumia mali ya msikiti huo kwenye msikiti mwingine.

SWALI 248 : Je inajuzu kubeba turba kutoka msikiti kwenda kwenye msikiti mwingine na kuitumia kusalia ?

JAWABU : Haijuzu.

  KUZUWIA SEHEMU KWA AJILI YA KUSALIA 

SWALI 249 : Mtu ambae amezuwia mahala kwa ajili ya kusalia katika msikiti na akatoka kwa ajili ya kutawadha, na mtu mwingine akaja na kukunja mswala wa mtu wa mwanzo nae kukaa na kusalia mahala pale, je sala yake inasihi ?

JAWABU :Kauli ya ahwat ni kuwa airudie sala yake kwenye sehemu nyingine. HUKUMU MBALIMBLI  KUHUSU MSIKITI

SWALI 250 : Je inajuzu kuandaa masomo ya kiangazi, na kuonyeshea filam za senema msikitini ?

JAWABU :Ni wajibu kulinda heshima ya msikiti, kuanzisha  masomo ya dini haipingani na heshima ya msikiti, lakini kuonyesha baadhi ya filimu za sinema hailingani na utakasifu wa msikiti.

SWALI 251 : Katika sikukuu za idi  za kiislaam na siku za kuzaliwa maimamu maasumiin (a.s) hufanyika hafla misikitini na kwenye huseiniyyah, na huimbwa kaswida za kidini, je inajuzu kupiga makofi katika mahfali haya na kwenye vikao vya kufurahikia au kusherehekea ?

JAWABU : Haijuzu kupiga makofi msikitini na kwenye huseiniyyah na sehemu takatifu kwa anwani yoyote ile.

SWALI 252 : Ni ipi hukumu ya vikao vya kusoma alfaatiha au hitima kuwa zaahim ( kuwasonga) wenye kusali au wenye kushughulika na kuvuta nyuradi ?

JAWABU :Haipasi kufanya hivyo, isipokuwa ikiwa nyuradi hizo zita vuka kiwango cha kawaida, na haijuzu kuwa zaahim wenye kusali. 

SWALI 253 : Hufanyika baadhi ya mambo ya kitamaduni na michezo kwenye baadhi ya misikiti, na imeanzishwa maktaba na kituo cha kanda kwenye tabaka ya chini ya msikiti, na kanda hizi hazizi tii ufinyu na kuzisonga songa  sehemu za waqfu wala walio wekewa waqfu hizo, na katika tabaka la chini na katika nyakati zingine tofauti na nyakati za sala,  wakati mwingine hutumika tabaka la chini kwa ajili ya mazoezi, tubainishieni mtazamo wenu kuhusu suala hili ?

JAWABU : Ikiwa kufanya hivyo hakuta sababisha kuvunja heshima na kuuhini msikiti hakuna kizuizi kufanya hivyo.

SWALI 254 : Je inajuzu kupiga makofi kwenye sherehe za kuzaliwa maimamu watwaharifu (a.s) na kwenye idi za kiislam,  tubainishieni mipaka yake ?

JAWBU : Inajuzu sehemu zingine tofauti na misikiti na huseiniyya, japokuwa bora zaidi kutofanya hivyo mutlaqa (moja kwa moja).

SWALI 255 : Katika sura ambayo haijuzu, ni ipi hukumu ya kwenda na kuhudhuria kwenye vikao au mahfali hizi ( bila kupiga makofi) ?

JAWABU : Hakuna kizuizi katika kuhudhuria kwenye misikiti na huseiniyyah bila ya kupiga makofi, na ikiwa kuna ihtimali ya kuwa kuwakataza kutatoa athari basi wakatazeni kupiga makofi kwenye sehemu kama hizi tukufu, kwa sababu kufanya hivyo inazingatiwa kuwa ni miongoni mwa kuvunja heshima na kuto uheshimu msikiti, na kunapingana na utakasifu wa msikiti na huseiniyyah.

SWALI 256 : Ni ipi hukumu ya kuweka picha ya mtu na wanyama msikitini ?

JAWABU : Ni makruhu kufanya hivyo, kutokana na  kuwa makruhu kusali kukiwa na picha hizo.

SWALI 257 : Umekamilika ujenzi mpya wa msikiti, na hadi hivi sasa hakuja tolewa malipo ya wajenzi na vibarua, na wao wanasema : haturidhii kusali kwenye msikiti huu ikiwa hatujalipwa malipo yetu, tunataraja kwako mheshimiwa kutubainishia hukumu ya suala hilo ?

JAWABU :Kusali msikitini hakuambatani na kuridhia kwa mtu yeyote, ikiwa msikiti una mali ya waqfu itatolewa kwenye waqfu hiyo na kuwalipa, na ikiwa msikiti hauna mali ya wqfu inapasa kwa ndugu waumini kulipa madeni ya msikiti.

SWALI 258 : Mtu mmoja alikuwa akisalisha sala ya jamaa msikitini, na baada ya yeye kufariki mwanae akashika  mahala pake kwa miaka kadhaa. Na imamu wa al-juma’a wa mji huo kutokana na maslahi ametoa amri ya kupanuliwa kwa msikiti na kumteua mtu mwingine kuwa imamu, na yule imamu wa mwanzo hakuridhika na kitendo hicho, ni ipi hukumu ya kusalia kwenye msikiti ulio tajwa ?

JAWABU : Kuhusiana na imamu wa msikiti hakuna yeyote mwenye haki katika jambo hilo, na  mas’ala ya mtu fulani kukubali au kutokubali kwake hayana iitibari kwa upande wa kisheria.

SWALI 259 : Ikiwa msikitini kuna kikao cha maombolezo, je inajuzu kutumia umeme wa msikiti katika vifaa vya kurekodia vya watu binafsi ?

JAWABU : Haijuzu, isipokuwa wakitoa malipo ya umeme ulio tumika, na wakati huo inajuzu pamoja na kuomba ruhusa kwa msimamizi wa msikiti. 

SWALI 260 : Nina miaka arobaini (40) nikitoa huduma za msikiti, je inajuzu kuusia nizikwe sehemu ya kuingilia msikitini ?

JAWABU : Usia huu si sahihi.

SWALI 261 : Ni jambo lililo zoeleka katika baadhi ya misikiti wakati wa vikao vya kusoma al-faatiah kuweka vipaza sauti nje ya msikiti, je kitendo hiki kinafaa, hasa ukizingatia kuwa kuna wagonjwa na watu wazima au wazee ambao huudhiwa na sauti za juu za viza sauti hivyo ?

JAWABU : Kitendo hicho kina ishkali.

SWALI 262 : Ni ipi hukumu ya kubomoa sehemu na majengo- ambayo yameandikwa juu yake aya za Qur’ani- kwa lengo la kuyakarabati ? na ikiwa majengo hayo yataharibiwa mchanga na vifaa zilivyo zidi vitafanyiwa nini ?

JAWABU :Hakuna kizuizi cha kufanya hivyo, na mchanga ule ulio bakia utawekwa sehemu na kuhifadhiwa heshima yake, au utamwagwa kwenye maji yenye kutiririka, au utachimbiwa shimo na kufukiwa.

SWALI 263 : Je inajuzu kufanya hafla na sherehe za harusi na kuoa misikitini na kwenye Huseiniyyah ?

JAWABU :  Inabidi kujiepusha kufanya hivyo.